MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Saturday, October 19, 2019

FUNGUO AMBAZO ZINAWEZA KUFUNGUA MAISHA YAKO.


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila


15TH October 2019

Kuna funguo tano ambazo zinafungua maisha ya mtu na tunaanza somo ili la kutembelea funguo ambazo zipo. Bwana akamwambia Petro “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.” Mathayo 16:18-19


Na leo tunaangalia funguo wa kwanza.

NENO LA MUNGU

Yohana 1:1-5
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.


Hapo mwanzo hakukuwepo na kitu chochote kwasababu neno lilikuwa alijatoka kwa hivyo hakukuwepo na kitu chochote. Kwa mfano rahisi leo tunapoongelea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania au katiba yake. Sasa pasipo mtu kusingeweza kuwepo na sheria wala katiba kwasababu vyote vilikuwa ndani ya mtu na vilipotolewa ndipo vikawa sheria. Wabunge wanakaa na kujadili jambo kisha wanaliweka linakuwa sheria ambayo inaweza kumtia mtu hatiani au kumtoa hatiani. Unapojivunia katiba maana yake unajivunia maneno ya watu.

Mungu anapotamka ilo ni neno linaleta uzima kwako, afya kwako, utajiri kwako. Tofauti yako na shetani ni moja shetani analijua neno na wewe haulijui neno.

Kwa mfano unatenda dhambi na neno linasema “atendaye dhambi ni wa Ibilisi” 1Yohana 3:7a kwa hivyo unapotenda dhambi shetani anakushitaki kuwa huyu ni wa kwangu. Anatumia neno kukushtani kwasababu yeye ni mshitaki wetu. 1 Petro 5:8. Kwa hivyo basi hakuna lolote ambalo linaweza kufanyika pasipo kuwa na neno. Hakuna ambaye anweza kuishi Tanzania pasipokuwa na katiba na ndiyo maana hata mtu anapoweka sahihi kwenye mikataba inandikwa kwamba itaongozwa na sheria za nchi husika.


Maandiko yanasema neno la Mungu likae kwa wingi ndani yako kwanini kwasababu linapokaa ndani yako linatengeneza tawira ya KIMungu ndani yako, macho ya KIMungu ndani yako. Yesu anaposema ufanane na yeye anamaanisha neno lake ukiwa nje ya neno haufanan nay eye na ukiwa ndani ya neno unafanana na yeye. Maana yake ukiwa unaamini kila jambo neno linafanya “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” Wafilipi 4:13 maana yake kila unachofanya unaamini katika neno.


Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima


Ndani ya neno ndipo kulipokuwa na uzima na neno linasema kabisa kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 1 Petro 2:24 Neno linaposema usipayuke payuke maana yake usiombe bila neno kwasababu bila neno ni kelele tu Mathayo 6:7. Maandiko hayakuwa na tafsiri ya kupaza sauti bali ni kuomba bila neno.


Nisikilize ndiyo maana makanisa ni mengi na kila mmoja amepewa chakwake na Roho ni yule yule, sisi neema tuliyopewa ni ya kuamuru 1 Wakorintho 12:4. Ile sauti ya kuamuru inatoka kwa nguvu na wala si kwa unyenyekevu. Si unajua hakuna mwanajeshi anaweza kuongoza gwaride kwa sauti ya chini anaamuru kwa nguvu. Tunapoamuru kuhakikisha kwamba wanaturudishia vya kwetu. Ndiyo maana maandio yanasema “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote” Wakolosai 3:16a.


Ndiyo maana ni muhimu kujua madhabahu unayoiendea kabla ya kujiunganisha na hiyo madhabahu. Kama sisi ni wanajeshi na wewe ni raia mwema ukijiunga na jeshi uatapata shida. Ndiyo maana ukija kwetu tukiwa tunaomba tunaloa jasho kweli kweli sasa kama wewe ni shirika fulani utapata shida sana. Lakini pamoja na tofauti hizi zote lakini wote tunaongozwa na katiba moja ambayo ni neno la Mungu.

Neno la Mungu linapoingia ndani yako linaondoa upofu na kufungua ufahamu wako. Unapopita kwenye changamoto na ukakutana na neno ambalo linahusiana na changamoto yako linabadilisha hali yako kabisa.

Isaka alikuwa kwenye tabu na Nchi ilikuwa na njaa. Lakini neno la Bwana likamja yeye na akapanda mbegu na kuvuna mara mia kwa kimojai. Yote yalitokea kwasababu ya neno la Mungu. Isaka alikumbuka kila mabcho Bwana Ibrahimu kwa neno la Bwana. Mwanzo 26:12.


Mungu anaposema kuwabariki kwa Baraka zote za Rohoni anabarikia mtu ambaye anaamini eno lake anabarikia mtu ambaye neno lake ni taa ya miguu yake. Sasa utamtambuaje mtu ambaye hayuko kwenye neno utamjua kwa chuki zake, magomvi yake. Mtu yeyote anayeijua kesho yake hayuko kwenye mashindano kwa hiyo utamjua tu. Yeye anachojua kama kafanikiwa Fulani kesho ni zamu ya kwake. Unaishi kwenye tabu na umasikini lakini ni kama vile umeinuliwa ngazi na unapokuwa unataka kupanda kwenye ngazi hauwezi kuangalia nyuma yako bali unatizama hatua zako. Yule ambaye haoni hatua zake anakaa chini na kuona amemalizika. USIOGOPE ASEMA BWANA WA MAJESHI SIMAMA NA USONGE MBELE.

Mimi nilikuwa mtu wa kutukanwa kama wewe, nilikuwa nimeketi nyuma kama wewe na pengine kudharaulika kuliko wewe na likatokea neno moja tu ambalo Bwana alinipa Isaya 45:1-5. Kilichokulemea ni akili yako siyo Mungu. Mungu anasema fedha na dhahabu ni mali yake na yeye ndiye aliyeweka vyote. Mungu akikupa maono utashangaa namna ambavyo utakuw wa dhamani. Ili Mungu hakufunulie lazima hakufunulie katika neno lake siyo kwa maneno. Ukiishi kwa neno ushindi wako ni kamili lakini ukiishi katika wingi wa maneno kushindwa kwako ni Dhahiri Mithali 10:19 .


Hili neno la Isaya lilipotamkwa nilijigeuza kuwa Koreshi masihi wa Bwana. Mungu anapotiisha maisha mbele yako wala hautumii nguvu. Wakati naitwa kwenye huduma nilikuwa ni mfanyabiashara na wengine wakafikiri nimepotea kumbe hawajui baraka hauwezi kuitafuta na inamfuata mtu. Walipoona nimetoka kwenye biashara na kuingia kwenye huduma wakajua nimefilisika na wanachozani ni kwamba ukiwa eneo la biashara ndo mafanikio yanakufuata. Leo wanashangaa siko eneo la biashara lakini ninafanikiwa.

Neno la Mungu usilisome kama kitabu cha kawaida. Kama unavyoona watu wanatetemeka na kupata shida kwasababu ya katiba ambayo ni maneno ya wanadamu inavunjwa ni Zaidi kwa neno la Mungu. Lazima ulitetemekee na kuliishi neno la Mungu.


Wakati nilipopata neno langu na nikafika kwenye kipengele kinachosema “nami nitakupa hazina za gizani” Ndipo nikaanza kutafuta hazina ambazo ziko gizani. Katika familia yangu mimi ni wa pili kujishughulisha na mambo ya madini na hakukuwa na wengine waliojishughulisha na shughuli hiyo.  Tofauti ya kufanikiwa ni namna ya kupata ufunuo katika neno. (unaweza kupata somo langu la HATUA SABA ZA MAFANIKIO LIMEJAA HABARI HII KWA UREFU)

NENO LINAKUFUNULIA NMAADUI ZAKO NA MAOMBI NI HATUA YA KUPIGA ADUI ZAKO. Unapoomba bila neno unarusha silaha bila kumpata yeyote. Ndiyo maana usikubali kwamba siku imepita bila wewe kusoma neno. Ngoja nijaribu hii hakuna mwanasheria ambaye anakwenda mahakamani kushindana kwa hoja pasipokuwa na mapitio ya sheria, wale walio wanasheria wanaelewa ninachosema. Hauwezi kumuambia shetani toka tu bila kuwa na sheria ya kumtoa kwenye maisha yako.


Kila mmoja duniani anamahali ambapo hazina yeke ipo na ndiyo maana ulipokuja duniani haukuja na kitu chochote. Mungu anayajua maisha yako tangu tumboni. Usiridhike kwasababu ulitoka tumboni mwa mama ukiwa hauna kitu tafuta kufunuliwa hazina yako, usiridhike kutoka tumboni tu. Kuna wengine wanafunuliwa hazina zao mapema wakiwa na miaka ishirini wengine thelathini na wengine sitini.


Mungu anajua kwamba ulikuwa haujui kuomba lakini yeye amejifunua kwako na anasema hapana mwingine zaidi yako. Mungu anajua kwamba malango yako yamefungwa. Umezaliwa kwenye familia ambayo haimjui, Mungu hayo ni mapingo ya chuma. Lakini Mungu anapokuita kwa jina lako anakusimamisha.

Shika moyo wako anza kujitabiria juu ya neno ili jigeuze wewe kuwa Koreshi.

No comments: