MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Saturday, October 19, 2019

FUNGUO AMBAZO ZINAWEZA KUFUNGUA MAISHA YAKO.



Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

17th October 2019

Tunaendelea na funguo ya neno la Bwana ambalo tulianza katika somo letu. kwa hivyo maombi yetu ni juu ya neno.

Kwanini Mungu anasema neno lake likae kwa wingi ndani yetu, kwanini anasema neno lake ni taa ya miguu yetu.

Mithali 30:5 Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.

Zaburi 12:6 Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.

Neno la Mungu limehakikishwa kwa maana ya kwamba lina uwakika, ndiyo maana anasema ulituma neno ili kutuponya.

Mathayo 24:35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Yote unayoyaona Duniani yatapita na wanini yatapita kwasababu hapo mwanzo kulikuwepo na NENO naye alikuwepo kwa Mungu. Unapopata neno la Mungu umepata uzima ndani yako, umepata afya ndani yako. Magonjwa yatapita, misiba itapita lakini neno lake alitapita.

Nakupa maandiko haya ili uone namna ambavyo eno la Mungu linabadilisha maisha yako

Zaburi 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Unaposikia mtu amekwama na kuchoka au amekata tamaa maana yake anahitaji msaada wa Mungu kupitia neno lake na anapolipata anaanza kuona mwanga mbele yake. Biblia inasema neno la Mungu likae kwa wingi kwa sababu neno linapokaa kwa wingi ndani yako unakuwa na tumaini la kusonga mbele na nguvu ya kuvuka.

Ndiyo maaana Mungu ameachilia neno lake unapokuwa kwenye njaa neno la Mungu linakuwa chakula kwako. Unapokuwa umechoka neno la Mungu linakufariji na kuwa fimbo kwako katika jina la Yesu. Unapokuwa na kiu neno lake linakupa maji.

Shetani akuogopi kwa sababu ya miaka yako ya kuokoka au namna unavyoudhuria kanisani. Shetani anakuogopa kwa maarifa uliyonayo ndani yako na neno la Mungu. Ukiomba pasipokuwa na neno ni kazi bure tu. Kial mtu anaomba lakini tofauti iko kweye kile kilichomo ndani yako. Waliookoka tuna bidi ya kuomba lakii hatuna bidi ya kutafuta maarifa.

Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

Yatakuwa yenu ni tukio ambalo litafuata ndiyo maana maandiko yanasema ukiomba uamini utapokea na yatakuwa ya kwako. Wengi wanaishia kupokea lakini hayawi yakwao.

Kwa mfano umepewa cheki zile ni fedha lakini siyo tasilimu kwa hivyo basi fedha ni zako lakini bado hazijadhihirika kwa maana ya kuwa zakwako. Kumbuka hilo hata yule aliyekupa anaweza kukataa isiingie kwenye account yako kwa hiyo fedha ulipewa lakini bado hazijadhihirika.

Kwa hivyo unavyoomba hakikisha unaendelea kuomba na kuomba mapaka unamiliki siyo unapokea tu kisha haiwi ya kwako. Ndiyo maana wale ambao hawana maarifa wanaishia kuwalalamikia watumishi wa Mungu. Ni kweli Mungu anaonyesha kile amabacho kipo kwenye ulimwengu wa Roho kwa hivyo ni juhudi yako kuongeza mahusiano na Mungu wako. Sasa wewe unaambiwa kwamba nimesikia habari njema kutoa mbinguni kile ambacho Mungu anakuwazia alafu wewe kesho hauna mahusiano na yule anayetaka kukupa unategema utapataje.

Elisha aliposema kesho panapo majira kama haya chakula kitakuwepo Samaria alitamani wale wakuu wasikie neno lile. Na alitokea akida akisema neno lile alitatimia na akaambiwa ataona ila atakula chakula. Elisha alitamka haya lakini kulikuwa na njaa juu ya Nchi. Na Mungu ili kutimiza neno lake akatafuta wakoma ambao walikataliwa na kuwekwa nje ya mji na wakaliendea jeshi la washami na wao wakakimbia wakijua ni kishindo cha watu wa vita. 2 Wafalme 7:1-20

Sikiliza wakoma hawakusikai kishindo lakini adui zao walisikia kishindo. Unapoomba wewe hauoni ukiwakata adui zako lakini wao wanakatika, unapoomba hauoni adui zako wakianguka lakini wao wanaanguka.

Wale wakoma kilichowasababisha washinde haikuwa silaha, wala jeshi lolote bali walikuwa MAJASIRI. Ukiwa jasiri kwenye jambo lolote Mungu anakuwa pamoja na wewe.

TAFUTA ANDIKO KWENYE BIBLIA SHIKILIA ILO NA ANZA KUOMBA NA UMUAMINI MUNGU

SIKU YA IJUMAA, JUMAMOSI NA JUMAPILI TUTAKUWA KWENYE MAOMBI YA SIKU TATU ILI KUKAMILISHA MAOMBI YA SIKU KUMI NA NNE HAYATAKUWA YA MASAA KUMI NA MAWILI BALI MAOMBI YA SIKU TATU KAVU KUMBUKA NI KUFUNGA NA KUOMBA USIJE UKAJARIBU KUFUNGA BILA KUOMBA UTASHINDA NJAA BURE NA NI KUOMBA KWA NENO LA BWANA

No comments: