MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 19, 2019

UTENDAJI KAZI WA KANISA LA POWER OF GOD’S FIRE CHURCH



        I.        NENO LA MUNGU yaani Biblia 
Neno la MUNGU ndiyo lenye mamlaka ya mwisho hapa Duniani na lisemavyo neno ndivyo itakavyobaki kuwa hivyo. Tunaamini kuwa neno la MUNGUndiyo mwamuzi halali wa Mwisho wa mtu na hivyo ndivyo ilivyo Ufunuo 22:19, 2Timotheo 3:16, Yohana 1:1

Hivyo kama kanisa lazima washirika wote wafundishwe na kuhimizwa na kuishi katika neno la MUNGU na kuliishi kwa maana ni silaha ya ushindi dhidi ya shetani na dhambi MATHAYO 4:4 Yeremia 23:29, Zaburi 119:11 

      II.        ROHO MTAKATIFU NA UTENDA KAZI WAKE (NGUVU ZAKE) 
Ukitaka kufanya kazi ya MUNGU kwa usahihi kama kanisa, nguvu ya MUNGU inahitajika ili kufikia malengo ya Mega – Church (Kanisa la MaelfuMarko 16:15-19)na Nguvu hiyo ni Roho Mtakatifu kwa maana nyingine nguvu za MUNGUzinaitwa;
1.   Moto wa Mungu –Waebrania 12:29
2.   Nguvu za Roho Mtakatifu 1Korintho 2:4-5 
3.   Uweza ushukao juu. Luka 12:49 

    III.        UBATIZO (MAJI MENGI NA KWA MOTO)
Kuna Viwango kadhaa vya kuwa na Nguvu ya MUNGU, kujazwa Roho Mtakatifu, kubatizwa kwa Roho Mtakatifu, na katika ubatizo wa maji mengi, ili uweze kuujenga ufalme wa MUNGU kwa ujasiri.Mathayo 3:11 Yohana 3:3-6

    IV.        MIUJIZA / UPONYAJI NA ISHARA ZA MAAJABU 
Kanisa lolote la MUNGU wa kweli nilazima liwe na udhihirisho wa nguvu za MUNGU dhidi ya Shetani na kazi zake zote, kwa maana Yesu Kristo alidhihirishwa (aliletwa) ili azivunje kazi za Ibilisi 1Yohana 3:8.Pia yeye mwenyewe Yesu alijitambulisha kwamba amepakwa mafuta (wakfu) kwa kazi hizo Luka 4:16-22 Yohana 10:10
 Hivyo Yesu Kristo ndiye kichwa cha kanisa na pia ndiye kielelzo cha kila mwamini (Mwanafunzi wake) yeye mwenyewe alisema kuwa “Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.Yohana 14:12
Hivyo, Yesu alifanya miujiza, kuwaponya watu, kufufua wafu n.k, nasi kama kanisa tunaamini katika kazi zake, Marko 16:17 

      V.        KUNENA KWA LUGHA 
Hii ni nguvu ya Roho Mtakatifu, amabyo ni ishara ya nje kuwa mtu huyu amejazwa Roho mtakatifu na inamsaidia mwamini kujenga utu wake wa ndani (nafsi yake) kwani mtu anaponena nafsi yake inawasiliana na MUNGU kwa lugha ambayo haiwezi kusikiwa na chochote iwe ni shetani au Malaika bali yeye mtu na MUNGU wake, hivyo ni vizuri kila mtu apokee karama ya kunena kwa lugha 1Wakorintho 14:2 

FALSAFA YETU (OUR PHILOSOPHY) 
Ni muhimu kila mwamini kujua falsafa ya huduma kwa ufupi,” FALSAFA” ni namna unavyofikiri (The way of Thinking)ni vizuri kujua namna tunavyofikiri kwenye huduma kumtumikia MUNGU huku ukiendelea na utumishi katika taaluma yako (lay leaders) yaani ukafanaya kazi yako na muda unaokubalika ukamtumikia MUNGU.Kwa maneno mengine anaunganisha taaluma yako au shughuli yako binafsi na kumtumikia MUNGU mfano , utabaki kuwa kiongozi / Meneja / Mwasibu / Mwandishi / Daktari / Mfanyabiashara /Karani /Waziri /Mbunge /Polisi /Mwalimu katika shirika au serikalini na bado ukamtumikia MUNGU bila kuacha kazi yako, hii ndiyo falsafa yetu mfano waliofanaya kazi na kumtumikia MUNGU kwenye Biblia "Daniel" ambaye alikuwa makamu watatu wa Rais na ni mtumishi wa MUNGU / pia aliwahi kuwa uliwali (mbunge) wa jimbo la Babeli Daniel 2:48  pia tunaona "Luka" alikuwa ni mwanafunzi wa Yesu na ndiye aliyeandika kitabu cha Luka Matakatifu na Matendo ya mitume lakini pia alikuwa ni tabibu (Specialist in international medicine).Alimtumikia MUNGU na huku akiendelea na taaluma yake, Wakolosai 4:14.Lidya alikuwa mfanyabishara lakini ndiye aliyemsaidia mtume Paulo kuanzisha kanisa la Wafilipi Matendo 16:14.

2) Falsafa yetu nyingine ni kufunga milango ya kutumia fedha kwa matumizi yasiyo ya lazima, na kujifunza kutumia fedha zetu kwaajili ya ufalme wa MUNGUni muhimu kujua kwamba maisha ya kila mtu kuna miaka saba ya njaa na miaka saba ya shibe, wakati una kazi weka hazina zako kwa Bwana kwa kujenga ufalme wa MUNGU mfano, Kutoa fungu la kumi, kusaidia kazi ya MUNGU na Injili isonge mbele ili Bwana aje kukushika mkono wakati wa njaa, wakati hauna kazi, wakati wa uzee, au wakati una matatizo Mathayo 6:16-21, wekeza katika ufalme wa MUNGU ili uwe na ujasiri wa kumdai MUNGU wakati mambo hayaendi vizuri.


VIWANGO VYETU (Our Standard) 

Ni muhimu kwa kila muamini/aliyeokoka kujua viwango vyetu ikiwa ni pamoja na mavazi ya kumpa MUNGU utukufu yaani mavazi ya kusitiri mwili wako. Mavazi yasiyofaahayakubaliki mbele za MUNGU, na mbele za wanadamu pia, ni lazima kuwa na mipaka katika mahusiano kati ya Mwanamume na Mwanamke katika kuujenga ufalme wa MUNGU hapa Duniani.

Pia ni lazima kuwa na tofauti kati ya kiongozi mmoja na kiongozi mwingine, lazima tofauti zetu ziwe bayana na kuheshimiana ngazi zote. Hivi ndivyo viwango vyetu tunavyotakiwa kuvitunza 
1) Lazima tofauti kati ya ngazi moja ya kiongozi na nyingine iwe bayana.
2) Lazima kila anayevaa mavazi atimize lengo la mavazi (Kujistiri mwili wake).
3) Lazima kila tendo au maamuzi yafanywayo katika huduma yafanywe katika kiwango cha Biblia na siyo kimila / kikabila / jadi.
4) Ni hakika kabisa sisi hatuna matabaka ya kielimu, kifedha na kabila.
5) Tunasisitiza tukiwa pamoja tunazungumza lugha moja inayoeleweka kwa wote. 


MSISITIZO WETU (EMPHASIS) 
Ni muhimu kwa kila muumini wetu kujali msisitizo wetu, msisitizo wetu sisi Power of God Fire Churchni kurudisha vyote ulivyoibiwa na shetani. MUNGU alimuumba mwanadamu akamkabidhi Dunia mali na fahari yake, lakini Shetani akamwibiaYohana 10:10, ni mapenzi ya MUNGU kwamba kila kilichoibiwa kirudishwe ikiwemo afya, uchumi, mahusianao, nchi, na hata wanadamu walioibiwa lazima warudishwe Isaya 42:22, Isaya 61:1.Tunasisitiza kwamba kila alichokimeza Shetani ni lazima atapike Ayubu 20:15pia ni kusudi la Bwana wetu Yesu Kristo kuvunja ufalme wa shetani na kazi zake zote hapa Duniani na kujenga ufalme wa Mungu aliye hai 1Yohana 3:8

Hivyo na sisi ni wafuasi wa Yesu Kristo, ndiye kielelezo chetu, ikiwa alikuja kuvunja kazi za shetani na kufungua wote waliofungwa na kuibiwa basi hata sisi msisitizo wetu ndiyo huo. Luka 4:16-21
sss
MATARAJIO YETU 
Matarajioyetu ni kwamba tutasambaa mtaa kwa mtaa kata kwa kata wilaya kwa wilaya mkoa kwa mkoa, nchi kwa nchi mpaka ulimwenguni kote yaani kanisa la maelfu Mega - Church ambalo ndilo Kusudi la Kristo Yesu Ufunuo 7:9, 1Timotheo 2:3-4


Kwa hiyo katika kujenga kanisa la maelfu ya watu Mega- Church ni lazima kubadili nia na mtazamo wako kuhusu kanisa, Mfano wamissionary walioleta ukristo hawakuwa na maono ya kanisa la maelefu bali walikaa mahali pamoja kuabudu na kujifunza neno la MUNGU, Maono yao yalikuwa ni kufikisha Imani ya Kristo katika mataifa yenye giza hususani bara la Afrika na Ulaya kwa hiyo walianzisha makanisa yenye watu wachache wachache yaani micro- Churches ili ukristo ufike haraka haraka katika kila mji kwasababu hiyo tumeridhi ukristo usiokuwa na nia wala mtazamo wa kanisa la maelfu ambalo ndilo mpango wa MUNGU kukomboa ulimwengu wote. 

Kwa hiyo huduma hii ya Power Of God Fire Churchchini ya Askofu Dankton Rudovick Rwekila ikiwa katika kujenga Mega- Church inatoa mafundisho ya neno la MUNGU yenye kuelekeza watu kutubu dhambi zao na kuacha njia zao mbaya, Kwa kuamua kubadili nia zao na mitazamo yao ya Dunia ya kidini, kidhehebu kikabila, na kuwa na mtazamo uliokuwa ndani ya Yesu Kristo. Wafilipi 2:5 1Wakorintho 2:16, 2Petro 3:9ambayo ni kuurithi ufalme wa mbinguni. 

Pia kwa kuzingatia hilo kanisa hili la Power of God Fire Church limekwisha kusambaa kuanza kufungua baadhi ya matawi mikoani, hususa ni mkoa wa Kagera, na Mkoa wa Lindi, wilaya ya Luwangwa, na hapa Dar es salaam ambapo ndipo makao makuu yalipo. 

MAWAZO YA WANADAMU KUHUSU UAMUZI WAKO
Wanadamu wengi watakuambia umepotea. Ndivyo walivyoniambia mimi na hivyo haitakuwa ajabu ukikabiliana na maneno hayo maana anayefanya kazi ndani yao ni shetani anayeitwa mungu wa Dunia hii, ambaye ndiye aliyewapofusha fikra zao na wasijue kwamba wao ndiyo wamepotea kwa kuacha kuiamini injili ya wokovu. Shetani huyu hafurahii kabisa uamuzi wako huu na ndiyo maana atawatumia wanadamu kukuambia umepota ili urudi kumtumikia tena shetani katika dhambi. Biblia inasema juu yako 2Wakorintho 4:3-4 
Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

MAWAZO SAHIHI YA MUNGU JUU YA UAMUZI WAKO

Wewe ulikuwa umepotea sasa umeonekana kabla ya uamuzi huu wewe ndiye ulikuwa umepotea. Ulikuwa mwana mpotevu na tena kondoo aliyekuwa amepotea. Yesu Kristo Muda wote huu tangu uzaliwe, alikuwa anakutafuta. Wachungaji au viongozi mbali mbali wa dini awakukuambia ukweli na walizidi kukupoteza na hata ukasahau kuwa kwenye pumziko ni kwa Mwokozi Yesu Kristo. Yesu mwenyewe ikabidi akutafute na kukuokoa katika kundi la waliopotea. Sasa umeonekana. 
Yeremia 50:6
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.

Luka 19:10
Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Wewe Ulikuwa umekufa sasa umefufuka. Mtu yeyote anayeishi katika dhambi kwa kuzaliwa yaani kwa kuirithi dhambi, mtu huyu ni mfu mbele za Mungu. Mbele za wanadamu wenzie anaweza kuonekana maarufu lakini mbele za Mungu hauna umaarufu wowote, Umekufa katika Dhambi. Dhambi zinamfanya mtu awe mfu mbele za Mungu.Kawaida ya ulimwengu huu kutenda dhambi ni kumfuata mfalme wa uweza wa anga yaani shetani anayetenda dhambi katika watu wote wanaoasi maagizo ya MUNGU katika Biblia na huku wengine wakijiita wakristo. Mimi pamoja na wewe kabla yakuokoka tulikuwa wafu katika dhambi, wana wa kuasi ambao ni watoto wanaosubiri hasira ya MUNGU. Angalia haya katika biblia: 

Waefeso 2:1-3,
Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.”

Baada ya kukata shauri kuokolewa umekuwa hai.
Ulitubu dhambi zako pale ulipoongozwa sala ya toba ulihuishwa (kuhuishwa ni kufufuliwa, kupewa uzima na kufanywa hai) pamoja na Kristo.
Waefeso 2:4-5
Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya amakosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani mmeokolewa kwa neema”

Furaha baada ya Kutafutwa kuonekana
Siku ile ya uamuzi wako kuokoka, ni siku ya kuikumbuka mno. Mimi naikumbuka mno siku niliyokata shauri kuokoka. Ni siku ya furaha kubwa na shangwe. Lakini kama ungekuwa na macho ya kuona huko mbinguni, huko furaha na shangwe iliyopo kwa ajili ya kuokoka haifananishwi. Jina lako limeandikwa sasa katika kitabu cha uzima Mbinguni, na ni juu yako mwenyewe kuhakikisha linabaki katika kitabuhicho cha kwa kung’ang’ania wokovu. Maana ni wale tu walio katika kitabu cha uzima watakaoikwepa Jehanamu ya moto. Soma ufunuo 20:15. Kuacha wokovu ni kulifuta mwenyewe jina lako katika kitabu cha uzima. Mimi tangu niokoke nazidi kung’ang’ania! Ni furaha ya ajabu! Ulikuwa umekufa sasa umefufuka, ulikuwa umepotea sasa umeonekana. Someni pamoja mstari wa kukumbuka (mara mbili) Luka 15:32,“Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea naye ameonekana”. 

Jambo la mwisho
Hakuna haja ya kujadiliana na mtu yeyote au kumwuliza yeyote juu ya uamuzi wako huu kwamba ni mzuri au siyo mzuri. Hata kama ni ndugu yako wa karibu namna gani, usitake ushauri kwake! Kufanya hivyo ni sawa na mtu aliye hai kumwomba ushauri mtu aliyekufa. Weweulikuwa mfu lakini sasa wewe ni hai. Wote ambao hawajaokoka ni wafu. Mimi sikuhitaji majadiliano yoyote nao juu ya uamuzi wangu wa kuokoka! Ningefanya hivyo, nisingedumu katika furaha hii ya wokovu. Mtu ambaye yeye mwenyewe hajaokoka, hawezi kuupokea uamuzi wako kwa furaha. 
Ni wale tu waliojaliwa neema hii ndio wanafahamu kwamba katika wokovu kuna furaha ya ajabu! Mathayo 19:11, (Someni wote) Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa”. Kumbukadada/kaka- Wagalatia 6:5,Maana, kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.

Wokovu ni nini?
Kuokoka ni kumkiri na kumuamini Bwana Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako na kwamba alikufa na kufufuka kwajili yako, pia kuishi sawa sawa na neno la Kristo Warumi 10:9-10, Yohana 3:1-6, Marko 16:16 
1) Kumkiri kwa kinywa -unapata wokovu 
2) Kwamamini kwa moyo - Unapata haki 

Wokovu ni kuishi maisha yanayompendeza Mungu na Wanadamu pia (Neno la Mungu) na utakatifu.Wakolosai 1:13-15Wokovu siyo dini wala dhehebu bali ni njia inayompeleka mtu kwenye uzima wa milele. Yohana 14:6Mimi ndimi njia ya kweli na uzima. 

Toba Ya Kweli ni nini? 
Toba ya kweli ni uamuzi mgumu anaoufanya mtu toka ndani ya moyo wake unaoleta mabadiliko ya kifikra, nia na mtazamo wa ndani, na muonekano wa maisha yako ya nje kwa ujumla na kuanza kuishi maisha matakatifu, sawa sawa na neno la MUNGU bila kujali wala kujutia uamuzi huo, wala kutamani kurudi nyuma. Luka 15:17-21 Marko 1:4 Mathayo 3:1-2

Toba ya kweli ni mlango unamuingiza mtu katika wokovu kwani toba ya kweli humpatanisha mtu na MUNGU kupitia Damu ya Yesu kwasababu mtu anapotubu dhambi zake roho yake inahuishwa upya na kurejesha mawasiliano yake yaliyokuwa yamekufa kati ya wewe na MUNGU wako, na roho yako inapokea uzima au uhai, Waefeso 1:5

Hivyo unavyofanya toba ya kweli huwezi kujutia maamuzi yako wala kuanza kukumbuka na kutamani kurudi nyuma yaani kuipenda dunia na tamaa zake tena. Bali kuanzia ulipotubu dhambi zako unaanza kuisikia sauti ya Mungu ili ikuongoze maishani mwako. Maana umekuwa mtoto wa MUNGU tangu ulipookoka Yohana 1:12-13.
Hivyo Mungu anawajibika kwako kama mtoto wake kwa kila kitu iwapo kama utaendelea kumshika yeye na kushika maagizo yake na kutembea katika neno lake, 2 Petro 3:9, Matendo 17:30, Kumbukumbu la Torati 28:1-14














No comments: