MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 19, 2019

MAOMBI YA KUOMBA KUILINDA IMANI YAKO NA MOYO UNAOMPENDA MUNGU ILI KUDHIBITISHA IMANI YAKO.


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 


Yakobo 1:2-4, 12
1 Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu. Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. 12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Hauwezi kuilinda Imani yako na kuiombea pasipokujua kiwango cha Imani yako. Si kila mtu Mungu anaweza kumjaribu kuna sifa ambazo Mungu ameziweka ili akujaribu. Biblia inafananisha na dhahabu inayopita kwenye moto kwa hiyo si kila mchanga una pita kwenye moto ila dhahabu tu. Wengine wanakimbia moto lakini wapo ambao hawakimbii moto maana dhahabu safi inaonekana ikishapita kwenye moto. 

SIFA ZA WATU WANAOJARIBIWA 

Ayubu 1:1-5 
1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, ab inti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng’ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki. Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.

Maandiko yanasema Ayubu alikuwa mkamilifu na aliepuka uovu. Kwa hiyo mtu mkamilifu ndiye ambaye Mungu anamjaribu. Mungu hawezi kumjaribu au kujaribu Imani ya mtu mwovu. Ayubu alikuwa mkamilifu na Mungu aliachilia utajiri juu ya maisha yake na aliombea watoto wake na kuwatolea sadaka ili kama wamemkufuru Mungu miyoyoni mwao hawasamehe. 

TAMBUA UNAPOJARIBIWA KINACHOTAFUTWA NI IMANI YAKO. 

Unapookoka na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako, vita unayokutana nayo tambua kwamba shetani hatafuti utajiri wako, afya yako bali anatafuta Imani yako. Sasa shetani anajua kwamba mwanadamu akiguswa katika maeneo matatu Imani yake inayumba. 

     I.        UCHUMI 
   II.        AFYA 
III.        MAHUSIANO 

Wengi wamekaata tamaa baada ya kupitia hatua hizi na wanajua kwamba Mungu hayupo. Ndiyo maana mtu kabla ya kuokoka inawezekana kabisa ulikuwa na afya nzuri, mali pamoja na mahusiano mazuri lakini ghafla ulipookoka kila kitu kinakwenda vibaya. Shetani hawindi vitu hivyo bali ni Imani yako. Angalia kwa Ayubu alimuambia Mungu Ayubu akutumikii bure nikwasababu umemzingira pande zote 

Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.”

Angalia ambacho kilikuwa kinatafutwa kwa Ayubu AMKUFURU MUNGU, na aiache Imani. Elewa kinachotafutwa ndani ya maisha yako siyo mali zako bali ni Imani uliyonayo.  Imani yako ikisimama shetani ana mahali pa kushika. Yesu wakati anawafundisha wanafunzi wake alikuwa mkali sana juu ya swala la Imani. Waliporudi wanafunzi wake na walikuwa wanafurahi kwasababu ya mapepo kumtii Yesu aliwaambia furahini kwasababu ya majina yenu kuandikwa kwenye ufalme wa MUNGU. Unaweza kuhubiri kweli lakini kama hauna Imani hauwezi kuuona ufalme wa Mungu. Mungu anatenda yale kwaajili ya jina lake na utukufu wake. 

Mtu mmoja aliniuliza inakuwaje Mchungaji wewe unatuombea sisi lakini wewe unakutana na mambo mazito. Inakuwaje tunakuja kwako kwaajili ya WATOTO wetu lakini wewe na upako huo mtoto wako anaumwa vipi? Inawezekana na wewe una maswali kama hayo sikiliza nikuambia jambo mtoto wangu anaweza kufa kabisa nikwasababu ninapitishwa kwenye moto ili Imani yangu ithibitike ndani ya Kristo Yesu. Wakati fulani nilikuwa naombea wamama kwaajili ya uzao na wanapata watoto na kushuhudia mbele ya madhabahu lakini mimi mke wangu alikuwa ana uzao. Sasa watu wakaniuliza wewe hauoni aibu unaombea wengine na wanashuhudia lakini wewe auna uzao? Nami nikawajibu kama Mungu anaona aibu basi nitaona aibu kwasababu aibu hii siyo ya kwangu.

Shetani anasema Ayubu amezingirwa kila pande maana yake hakuna sehemu yakupita kumfikia Ayubu. Alikuwa mtu wa thamani mbele za Bwana ndiyo maana alikuwa na ulinzi pande zote.

Wengi hawaelewi wanaposakamwa mtaani mbingu inaandaa ulinzi kwa ajili yako. Ndiyo maana nimesema ikipita siku au wiki bila mimi kuwa na vita lazima nianze kuuliza Mungu huko wapi maana najua kuna mahali nimekosea. Sijasema vita kwaajili ya uovu nasema vita ukiwa kwenye maombi na umejaa upako lakini unapigwa vita kila eneo la maisha yako, iwe ni uchumi, afya au mahusiano. Nikipigwa vita nainua mikono juu na kumshukuru Mungu kwaajili ya vita hiyo kwasababu najua kuna mahali Mungu ananipeleka. 

Ayubu aliwaambia marafiki zake Elifazi, Mtemani pamoja na Bildadi Mshuhi kwamba wao ni wafariji wataabishaji, aliwaambia kwamba yeye ndiye ameguswa. 

Mtu mmoja alikuja ofisini kwangu na kuniambai anapitia majaribu na mimi nilimuambia Roho Mtakatifu ananiambai haujapitia. Akachukia na kuniambia Mchungaji wewe haujui tu nakuja kanisani sipati chochote ndiyo maana hata kuja kanisani nimeona siyo kitu tena. Akakaa nyumbani na muda si mrefu akapata biashara na baada ya muda akapata rafiki ambaye alimuambia ili biashara yako iweze kuwa nzuri tumlete mtaalamu hapa. Na ni mtu ambaye alikuwa mwanamaombi mzuri sana lakini ameijenga madhabahu ya shetani kwenye kazi yake, na bila kujua kwamba shetani anatafuta Imani yake. Wakaanza kutoa makafara, mtoto wa kwanza, wa pili, Baba, Mama akamuuliza Mganga hii ni kitu gani wakamwambia wazee wanataka damu ya mwanadamu maana hii ya kuku haiwafai. Amekuja kuacha mambo hayo huku amechelewa na kwasababu hakutoa kafara wakampiga yeye akapooza upande mmoja wa mwili. Sasa usipojua kwamba Shetani anatafuta Imani yako utakasirika kuomba, utakasirika kuja kanisani kwasababu ya vitu fulani fulani. 

Ayubu aliyekuwa tajiri ambaye kwa Tanzania tungesa Bakharesa lakini alisema sinta mkufuru Mungu wangu. Aliyekuwa mkuu ameketi kwenye majivu anajikuna tena ana kitu, mtu aliyekuwa na kondoo elfu sana. 

“Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.”

Jaribu kufikiri kama wewe ndiye ungekuwa Ayubu ambaye alikuwa na utajiri wote huo lakini ghafla ameshuka na kuwa masikini ambaye ana kitu hata kimoja, wala watoto wala wajakazi tena, lakini Ayubu alilinda Imani yake.

Ukipita kwenye majaribu tafuta kitabu cha Ayubu alafu anza kusoma, nisikile vizuri hayupo alikuwa mkamilifu mpaka anatoa sadaka kwaajili ya watoto wake, sasa wewe ambaye hata toba yako mara nyingine imekushinda. Ayubu alikuwa akiomba toba kwaajili yake na familia yake alikuwa mkamilifu mbele za Mungu. Siyo kwamba Ayubu aliacha kuomba pale ambapo alipita kwenye majaribu, aliendelea kuomba na Mungu alikaa kimya. Mungu alikuwa akimtizama Ayubu akiwa kwenye uwanja wa mapambano akiilinda Imani yake. Hauwezi kumpendeza Mungu kama auna Imani ndani yako.  

Hakuna kitu ambacho hakina gharama, usidhani kwamba utapata taji bila ya kuwa na gharama zozote hiyo haiwezekani, lazima kuna gharama zakulipa. Hauwezi kuwa na ndoa ambayo ina furaha bila kulipa gharama hiyo iko wazi kabisa.  

Lazima ujiulize kwanini Mungu akulinde usiku na mchana je unacho kitu cha kuibiwa. Kuna watu hawana kitu cha kuibiwa kabisa kwasababu shetani ameshikila vitu vyao sasa unaporejesha mara saba unarejesha nini? Hili ni swali la kujiuliza unataka kulindwa je una kitu cha kulindiwa? 

Fimbo ya Ayubu ilikuwa inaendana na Imani yake, sasa usiombe ukapigwa fimbo ambayo imekupita kipimo chako. Fimbo inayompiga Mchungaji siyo kama inayo piga kondoo, ile ya Mchungaji ikipiga kondoo nilazima atasagika. Ni muhimu kutizama sana wengine wanapigwa kwasababu ya kiburi wala si kwa sababu wanajaribiwa. 

Kuna watu wengine wamekosea kwenye maisha yao, ni wavivu na wala hawana mpangilio wa maisha yao. Hayo hatuwezi kuyaita majaribu. Kila kitu kina wekwa kwenye mpangilio na watu ukiwaambia kila unachopitia ni jaribu utashangaa kesho watu wote wanakuwa masikini. Mtu akishindwa kwenda kazini atasema ni jaribu lake hilo, akikosa kuwa na heshima anasema ni jaribu langu hili sikiliza mengine si majaribu ni kukosa kuwa na mpangilio kwenye maisha yako. 








No comments: