MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, June 03, 2014

WE NEED TO CHANGE

Asante Mungu ni siku njema tena yenye baraka tele , na tuko wazima wenye mawazo pevu na zaidi ya yote Ulinzi wa roho mtakatifu umekuwa pamoja nasi siku ya jana , juzi na leo vile vile .  katika hali ya kawaida na kusikia sikia story nilikutana na story hii ya ajabu na kudhibitika kuwa kuna mtoto Morongoro amekaa miaka 4 na nusu kwenye box .....


Nimesikitika sana na namuomba Mungu atuhurimie tena na tena maana binadamu tumekuwa wanyama kuliko wanyama wenyewe sina wa kumuhukumu ila nilikuwa , namaswali mengi sana juu ya jinsi mtoto alivyotolewa , mimi nilizani madaktari wangeliangalia swala hili kiundani zaidi kuliko walivyochukulia , Mtu kuwa kwa box miaka mitatu kwa haraka haraka mtu huyo alishazoe mazingira ya boxs na alitakiwa kuwepo kwa mazingira fulani yanayofanana na hayo ndipo matibabu yaanze sidhani , sidhani kama unaweza kumtoa samaki kwa maji na kisha kumuweka nchi kavu akaishi kwa muda mrefu huo ni mfano tu , na nimaoni na mawazo yangu kwa kile kidogo Mungu alichonijalia .

Again kwa baba mzazi huko na miaka minne ujamuona mwanao kweli wababu wasiku hizi mmekuwa hivyo jamani , hata mapenzi na damu yako aukuwa nao , au kuna imani za kishirikina katikati ya hili jambo juu ya baba na mama mkubwa , huruma yetu iko wapi wanadamu hata majirani miaka nenda rudi kweli awakujua kabisa , mtoto alikuwa analishwa vipi wapendwa . Mimi sina majibu lakini yeye aliye juu anayeangalia wote wenye mwili anatuona na sisi wanadamu na kwa nguvu zake atafanya maamuzi maana yeye ndiye hakimu wa wote .

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mdogo wangu mpendwa Nasra mvungi , naamini huko juu na malaika Nasra unaimba haleluya haleluya . Further tuonee huruma watu wako , tunahitaji toba kutoka kwako juu ya vizazi vyetu na juu ya Nyumba zetu na Taifa kwa ujumla .

No comments: