MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Monday, June 02, 2014

TUMRUDIE ALIYE TUUMBA ANATUHITAJI TUMTUMIKIE

Shalom wapendwa katika kristo

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu lakini yote ni kukaa na kutafakari hukuu wa Mungu wetu ndani ya maisha yetu , katika kipindi kifupi kumekuwa na habari za hapa na pale utabiri wa hapa na pale na wengine wamefikia hatua ya kunukuu na kuonyesha kupitia maandiko ishara za siku za mwisho , nia na madhumuni yangu kwa leo si kuongelea siku za mwisho hila hili la wapenzi wa tasnia ya filamu na kizazi kipya cha bongo flavour

Kwanza napenda kutoa pole kwa wanafamilia mbali mbali waliofikwa na misiba hii kwa kipindi kifupi Mungu awafariji sana na kuwatia nguvu tuwaombee na tukiwa tunatafakari maisha yetu pia . Ni jambo la kutisha kupoteza ndugu zetu tena waliokuwa katika pick ya sanaa ya maigizo lakini Mungu anasema na sisi nini kuhusiana na hilo wapendwa , kila jambo linapotokea juu ya nchi kuna wakati kufungwa na mwingine kufunguliwa .

Tafakarri ya haraka haraka tukirudi nyuma na kuangalia Biblia zetu kwa makini kipindi sodoma na gomora inaangamizwa uovu ulizidi juu ya nchi na Bwana akafutilia mbali taifa lile lililo msahau Mungu na kukengehuka kabisa , swali la kujiuliza mimi na wewe je kwa sasa taifa liko salama than before , ama maovu ndo yamezidi juu ya nchi je ? taifa la Tanzania na wasanii wake liko sawa , Je ? wasanii ni mfano wa kuingwa au kioo cha jamii . Majibu ya maswali yote uwezi kuyapata ukienenda kwa pupa .

Wasanii wetu kama kioo cha jamii wamekuwa si mfano wa kuingwa kama wengi tunavyozani wakati fulani nilijiona mwenye kipaji na nikataka kujitumbukiza kwenye tasnia ya maigizo lakini sikuweza na sababu sikupata lakini wakati Roho mtakatifu aliweka mzigo wa mimi kuwaza nilianza kutaka kujua chanzo cha kusita sita . Watoto wengi wanaharibika kwasababu ya vioo vyetu vya jamii wasanii wamekuwa wakiiga mitindo mipovu ya mavazi pamoja na stahili za maisha yao amabayo aimpendezi Mungu hata kidogo simulizi zao ni za starehe na mapenzi , sidhani kama maisha ni mapenzi tu , taifa lina changamoto nyingi na wao wamekuwa busy katika kubomoa maadili ya kitanzania na pengine ya hata nchi jirani jambo hilo ni hatari sana

Embu tuige mfano hata kwa wenzetu wanaigeria filamu Nyingi pamoja na kuigiza utajiri wamekuwa wakiliinua jina la Mungu wetu , aina maana ukiact vizuri kwa maadili autauza nina imani utauza na tena kuliko kawaida sidhani kama kuna filamu imewahi kutolewa copy nyingi kama filamu ya JESUS  sijui kama unalitambua hilo hala naamini ndiyo filamu bora na yenye kuuza na kuongoza kwa mauzo dunia nzima

Tumrudie Mungu wetu tutumike kwa kusudi lake na utaona matunda ya maisha , tumia kipawa ulichopewa kufundisha na kuelelimisha na si kujinufahisha na kuharibu vijana wengi wa kitanzania na Mungu atakubariki na utaishi miaka ya ahadi , utakufa maana utakuwa unatumikia kusudi la Mungu , mmejisahau sana mpaka na Hereni mnaingia nazo maeneo ya ibada , milegezo mapaka makanisani na majina yenu ni wapendwa kabisa jamani jamani , tumrudieye Mungu nasema tena na kutumikia kusudi lake .

Mwisho sina cha kuongeza wala kupunguza na Mungu atupe busara na tutafanikiwa tu , Amen .

No comments: