MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, June 03, 2014

NO NO NO NO NO NO NO MARA 100

Ukiona heading ya post hii unaweza ukajiuliza nini maana ya no no mara mia , wapendwa embu tutafakari sana mambo hayo hivi karibuni nimeandika post moja juu ya wasanii wetu na nimekumbuka sana mambo kadhaa juu ya wasanii hawa hawa na wakati naangalia social net work kwenye ukurasa wa msanii mmoja na nilishangazwa sana na posting moja ambayo yeye alicopy tu kutoka kwa mama mmoja na katika hali ya kushangaza wapendwa kulikuwa na comment kadhaa na zenye kuonyesha kukubaliana na wengine wakisifu kitenda hicho

Ukisoma Mithali 22 :6 Mlee mtoto katika njia impasayo , naye hataiacha , hata atakapo kuwa mzee ....... Ili swala linatisha sana kwa maisha ya sasa sitaki kuchambua sana swala hili kwa kina maana siku hizi watoto wanaachiwa wafanyakazi well and good mimi nataka kusema swala la mtu anamsifia mtoto wake kuwa anampenda msanii fulani heti mtoto awezi kula hata jina amebadili na mzazi anafurahi sana

Ukisoma katika Mithali 23 :7a Maana aonavyo nafsini mwake , ndivyo alivyo maana nyingine matokeo ya vile ulivyo ni jinsi ambavyo unawaza , sijui kama tunajua kuwa watokeo ya watoto wetu ni vile tunavyo wawazia na kuwaombea wawe maana mzazi unamruhusu mtoto kufikiri kuonekana na maziwa nje na vitu kadhalika wanavyofanya wasanii ni swala la ajabu kidogo na mama mwingine anasema na kutaja jina la msanii yaani mwanagu ukimwambia fulani anakuja anakula chakula kweli jamani hiyo ni sawa mmh something is not right somewhere wapendwa . Siwachukii wasanii wetu kabisa na nawaheshimu sana lakini sioni mchango wao katika hali ya kukuza watoto na jamii kwa ujumla hapo ndo ninapo nyanyasika kiakili na kuuzunika kimawazo , ila siku wakibadilika na hata Bwana wa majeshi aliyewaumba hatafurahi sana .

Unapo mpa mtoto wako jina na sifa za ajabu usisahau hata tabia ataiga mpendwa mlee mtoto vyema na akuwe kwenye kusudi la Mungu na kisha atumike vyema ndani ya kusudi hilo Amen ..

No comments: