MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

SALAMU KUTOKA MLIMANI



Na Bishop Dankton Rweikila 


Nakusalimia kwa jina la Yesu Kristo wa Nazarethi, nasalimia tumbo lisilozaa kwa jina la Yesu nasalimia maisha yako yaliyokwama kwa jina la Yesu. Nasalimia mikono yako kwa jina la Yesu. 

Nilikuwa kwenye maombi kwa siku kadhaa mlimani nikimuomba Bwana kwaajili yako. Unajua Baba anapotoka safari kuna zawadi anakuwa amebeba kwaajili ya watoto wake wanao msubiri kwenye malango ili kupokea. Na mimi leo nimekuja na zawadi kadha wa kadha. Baba amenipa mafurushi kumi kwa ajili yako na kila furushi lina watu wake ambao wanatakiwa kupokea. 


1. UTAJIRI NA MAFANIKIO NI SEHEMU YA MAISHA YAKO

Wafilipi 4:19 
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. 

Mashamba ni utajiri wake, nyumba ni utajiri wake, dhahabu na fedha ni utajiri wake, Bwana akujaze leo. Kwa hiyo kadiri ya utajiri wa Mungu hivyo vyote ni mali yako. Anza kuangalia kwenye kiroba hicho na ubebe chako, nataka uelewe neno hili NA MUNGU WANGU ATAWAJAZENI KILA MNACHOKIHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE. Kwa hiyo ndivyo itatokea kwako kwa jina la Yesu. 

3. KUPONYWA MAGONJWA YAKO NA KUPEWA AFYA NJEMA 

Wakati napokea ujumbe huu Mungu alinionyesha maono makubwa mno, Ngoja nikueleze kitu kimoja kuna watu wanaotegeneza vitu (Waunzi) na wanatengeneza vyombo mbali mbali kulingana na mahitaji ya watu, lakini vile vile wanatengeneza spea kwaajili ya kurekebisha gari linapopata shida huko linapokwenda. Kwa hiyo wakati wa gari kuharibika wako watu ambao wanatengeneza amboyo siyo waunzi ni watu ambao wanatumika katika kutengeneza. Kama ikifika wakati gari hilo likafika hatua ya kushindikana itapelekea gari lile kuachwa lakini ikatokea mtu akapata mawasiliano na kiwanda cha gari ilo basi litaundwa upya kwasababu wao ndiyo wanajua namna walivyoliunda. Hivyo ndivyo ilivyo kwa mwanadamu kwamba unaweza kuuumwa na kuangaika kwa mafundi na ikafika wakati mafundi wameshindwa, lakini yupo ambaye ametengeneza na ndiye ameniagiza kukuambia huo ugonjwa ulioshindikana umeweka spea za kila aina lakini hautoki kwake kuna tiba ya kweli.


Mathayo 8:1717 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. 

Unapooanza kusoma neno linasema ILI LITIMIE LILE NENO LILILONENWA NA NABII ISAYAelewa jambo moja Mungu anamtumia nabii Isaya kunena hayo kwa hiyo kuna neno ambalo linatakiwa kutimia kwenye maisha yakol eo kwa jina la Yesu. 

TAHARIFA 
Nataka kutoa taharifa baada ya salamu za jana na leo vile vile 


JICHO LA UOVU 
Unapotaka kufanikiwa kuna jicho la uovu ambalo linataka kuangalia mafanikio yako ili liweze kuachilia uovu juu ya Baraka ambazo umepokea. Jicho la uovu linafuatilia ili kuhakikisha kwamba unarudi nyuma. Wanaweza kukuacha ufunge na ukimaliza mfungo unashangaa huko pale pale. Unakwenda kwenye semina na ukirudi kutoka huko unabaki pale pale. 

Ngoja nikuonyeshe kwanza jicho la uovu kabla sijaanza kufungua vifurushi. 

1 Wafalme 13:1-3, 7 & 11

1 Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako. Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika. Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu. 11 Basi nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao. 

Huyu ni nabii ambaye ametumwa kwa mfalme na ambaye alikuwa na madhabahu yake na akatamka neno juu ya madhabahu na ikapasuka vipande vipande. Najua ziko madhabahu ambazo zinakwenda kupasuka vipande vipande. Huyu ni nabii wa Bwana ambaye ndani yake kuna nguvu ya Bwana kwa hiyo alitamka na likatendeka pale pale. Lakini jicho la uovu ni la ajabu aliogopi mtu linapenyeza taratibu ndiyo maana unashangaa mbona nimepiga wanganga wa kienyeji mbona maisha yangu hayaendi kumbe lipo jicho la uovu ndiyo maana tunakwenda kulishughulikia jicho la uovu. 

4. MAMLAKA JUU YA SHETANI NA NGUVU ZAKE ZOTE NA FALME ZA KUZIMU 

Ninaposema Mungu atakupa kuna kiwango cha Rohoni ambacho utazidishiwa. Mathayo 28:18 
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 

Uwezi kuwa na mamlaka na asiye na mamlaka, Bwana anasema 2018 utakuwa na mamlaka juu ya shetani na falme zake. Bwana anayo mamlaka mbinguni na Duniani.

2 Wafalme 2:19-22 19 Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. 20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. 21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. 22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.

Watu wa mji walisema na Elisha kwamba mji huu unafaa lakini maji hayafai. Kuna vitu kwenye maisha yako vinawezakuwa vinafaa lakini shetani akaachilia mgomo visifae. Na mwaka huu kazi zetu zinakwenda kufaa kwa jina la Yesu. Ninajua shetani kuna kitu ameweka ndani mwaka ambacho hakifai. 

Baada ya maombi haya natamani kila mtu akimbilia mtaani. Hata kama unamtaji wa elfu kumi hakikisha unaingia mtaani kwasababu Bwana anakwenda kuongeza huo mtaji. Ndiyo maana nilikuambia omba Mungu akupe wazo lake na wakati unaomba maombi haya ya siku saba Mungu akupe wazo la utajiri kwa jina la Yesu. Kwa hiyo wakati unaomba usiombe tu, usiombe bila kutega sikio kwa Bwana ili haweze kuachilia wazo kwako. Unapoomba namna hiyo kuna wazo litakuja ndani yako kwamba umekuwa masikini kwaajili ya kitu fulani kuna wazo ambalo Mungu ataliachilia kwako. Ukikemea mapepo, washirikina, wachawi bila kusukuma mzigo huo jua jambo hilo litakurudia. Unaweza kuomba sana na usione matokeo kwasababu mwaomba vibaya ili mvitumie kwa tamaa zenu. Ingawa maandiko yanasema ombeni nanyi mtapewa na maombi ya mwenye haki yafaa sana akiomba kwa bidii. Sasa kuna vitu ambavyo hata kabla haujaomba utapata, yapo ambayo yanatokea hata bila ya kuomba lakini jua kwamba yapo ambayo ni maalumu kwaajili ya watoto wa Mungu wanapoomba maalumu yanatokea. Haya ambayo ni maombi ya wenye haki kuna namna ambayo wakiomba kwa bidi wanapokea package yao, kwasababu maombi ya mwenye dhambi ni chukizo mbele za Bwana. 

Mungu anapotoa anatoa kwa viwango vile vile, kama ni mtu aliyekomaa Rohoni usidhanie utapa kirahisi tu, kuna ambaye ameomba miezi mitatu unashangaa amefanikiwa lakini wewe umeomba miaka mitatu bado haujafanikiwa. Sikiliza wewe ni kiwango kingine ambacho ukitokea ng’ambo ya pili si wa kawaida. Ukiona mtu anaomba na wala hauoni chochote kinachotokea muogope sana mtu huyo kwasababu mji wake anao andaliwa ni mkubwa sana. 

Unapokutana na mambo magumu ambayo unaona kabisa kwenye ulimwengu wa Roho wewe ni tajiri lakini hauoni kutokeza upande wa pili. Unaposhindana kwenye ulimwengu wa Roho utaona namna ambavyo unakuwa na vita kubwa kwenye nafsi yako. Kwa hiyo inapotokea unaona ametokezea upande wa pili na nafsi yako haina ushindani ndani yako tena kwa maana nafsi imekubali wazo la Mungu. Ni lazima ukubali kupigana mpaka nafsi yako ikawe sawa.

Nataka uelewe kitu kimoja cha msingi MAOMBI HAYATAJIRISHI MTU kinachotajirisha mtu ni kile kinachotokana na maombi. Kwa hiyo maombi yanakuzogeza karibu na Mungu na kile ambacho unaondoka nacho kwenye maombi. Nataka uombe na uwe na matokeo ndani yako kwa jina la Yesu. 


5. KUWA NA AKILI NJEMA NA MAHARIFA NA BUSARA.
Zaburi 111:10 10 Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.

Akili ya MUNGU haiwezi kushindana na mwanadamu yeyote. Akili njema inatokana na wewe kumuabudu Mungu kwa hiyo unapoendelea kumuabudu Mungu unaruhusu Mungu kuachilia akili njema kwako. 

Mungu akikupa wazo ni lile la kukufanikisha na unapopokea wengine wanaweza kuona ni jambo la kawaida lakini kwako wewe hilo ni wazo ambalo litakupeleka kwenye hatua nyingine ya maisha yako. Yule mwanamke mjane alipokea wazo kutoka kwa Nabii wa Bwana na alimuambia akaombe vyote kwa majirani tena atake vingi na akajifungia ndani na kumimina mafuta kwenye vyombo na vyote vikajaa. Elisha akamwambia nenda kauze ukalipe madeni yako yote na nyingine ukatumie. Wakoma wakasema tukikaa hapa tutakufa njaa bora tuliendee jeshi la washami maana tukikaa hapa tutakufa na tukiwaendea kama watatuifadhi hai ni sawa. Wazo hilo ndani yao likaanza kufanya kazi ndani yao na wakaenda kwenye jeshi hilo na Mungu akaachilia kitu cha ajabu kwao. 

Nisikilize nikuambie hiyo elfu kumi uliyonayo leo itaisha kama hautaiongeza, kwa hiyo ikihiifadhi itaisha kwa hiyo usiogope kufanya biashara kwasababu ya hasara. Usiogope kwasababu Bwana ataachilia kishindo chaajabu huko kwenye biashara yako. 

Maandiko kwenye Ufunuo 21:8Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Kwa hiyo wewe ambaye ni muoga hauna tofauti na mtu ambaye ni mzizi wote mahali penu ni kwenye ziwa la MOTO. Mwaka huu ni mwaka wa kupiga hatua wacha uoga. 

6. ULINZI NA USALAMA JUU YA MAISHA YAKO NA FAMILIA YAKO 

Kumbukumbu la Torati 9:1-13 1 Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni, watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki? Basi jua siku hii ya leo kuwa Bwana, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia Bwana. Usiseme moyoni mwako, Bwana, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia Bwana niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya Bwana awafukuza nje mbele yako. Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya Bwana, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno Bwana alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo. Basi jua ya kuwa Bwana, Mungu wako, hakupi nchi hii nzuri uimiliki kwa ajili ya haki yako, kwa maana u taifa lenye shingo ngumu. Kumbuka, usisahau ulivyomtia Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana Tena mlimkasirisha Bwana katika Horebu, Bwana akakasirika nanyi hata akataka kuwaangamiza. Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano Bwana alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arobaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji. 10 Bwana akanipa zile mbao mbili za mawe zimeandikwa kwa kidole cha Mungu; na juu yake yameandikwa maneno mfano wa yote aliyosema nanyi Bwana mle mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano. 11 Ikawa mwisho wa siku arobaini usiku na mchana, Bwana alinipa zile mbao mbili za mawe, nazo ni mbao za agano. 12 Bwana akaniambia, Ondoka huko, shuka upesi; kwa kuwa watu wako uliowatoa Misri wamejiharibu; wamekengeuka mara katika njia niliyowaamuru; wamejifanyia sanamu ya kusubu. 13 Tena Bwana akasema nami zaidi, akaniambia, Nimeliona taifa hili; na tazama, ni taifa lenye shingo ngumu; 

Mungu anasema na wana wa Israeli juu ya kumiliki Nchi anayowapa, lakini anawaambia wapo wana wa Waanaki ambao walikuwa na Nguvu kuliko Israeli. Bwana anajua unakwenda kumiliki mtaa na akiangalia kwenye mtaa anaona kuna wachawi wanaotawala kwenye mitaa hiyo hivyo anatanguliza utiisho wake mbele yako kwa yeyote aliyeleta vikwanzo ndani ya maisha yako.

Mungu akitaka kumuinua mtu au kumpeleka mahali lazima amuhakikishie usalama wake kwanza, alifanya hivyo kwa Gidion, Yoshua na wengine wengi. Anasema Bwana wa majeshi usiogope wala usifadhahiki kwasababu yupo Mungu atakayekutangulia kwa moto mbele zako. Unaanzisha biashara kwenye mitaa wanakuambia uonane na wazee wa mtaa usiogope yupo mzee wa siku simba wa kabila la Yuda. 

Mungu amechoka kuwaona waovu na ndiyo maana hatawatoa ili wewe uweze kukaa, unakumbuka nimesema kuna mambo ambayo yatatokea si kwamba kwasababu unaomba sana lakini nikwasababu ya Neema yake juu yako. 

Mambo ya Walawi 26:6 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu. 

Zaburi 121:5-8 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Mungu wetu anajua yapo mabaya yanayotegwa kwenye nyumba zetu, inawezekana wewe umelala na umejifunika kwa Damu ya Yesu lakini wapo wabaya wanakesha kwaajili yako. Lakini Mungu amesema atakuokoa na mabaya yote kwa jina la Yesu. Kuna watu wamelala ni wazima lakini wameamka ni wagonjwa, ulikula vizuri na kulala.

1.    MUNGU ATAKUPA WATOTO WAZURI NA FAMILIA NZURI 

Kumbukumbu La Torati 28:4Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 

Matendo 19:31 

Isaya 54:13
 Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi. 

Zaburi 23:1-6

1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

Uzao wa tumbo lako unaweza kuandaliwa bonde la mauti, lakini Daudi anasema umeandaa meza machoni pa watesi wangu. Kwa hiyo wanaweza kumtafuta mtoto wako lakini Bwana anaweza kumfanikisha. Hata kama wametega madawa kwasababu Bwana yupo upande wako usiogope mabaya kwasababu Bwana yuko pamoja na wewe. Najua unapita kwenye mateso kwenye kukataliwa lakini usiogope mabaya. Maandiko yanasema ukishapita kwenye mabaya kwasababu Bwana amekuandaa meza machoni pa watesi wako, meza ya Baraka yako, nyumba na watoto wako. Ndiyo maana Mungu hawaondoi watesi wako bali anawaacha ili waweze kuona namna ambavyo Bwana anakuandalia meza tena machoni pao. 


























No comments: