MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

SALAMU KUTOKA MLIMANI SEHEMU YA PILI

1.     NGUVU YA KUVUKA BILA KUKATA TAMAA


Kuna nguvu ya kuvuka bila kukata tamaa, yaani bila kuchoka na kupoteza matumaini

Yakobo 5:7-8Kwahiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. 

Kila anayevumilia huwa na mategemeo yabaadae kwamba kuna kitu nitapata cha dhamani. Maandiko yanafananisha tumaini lako kama kupanda mazao, hautaweza kupanda mazao na ukavuna leo lazima uvumilie na utaona matokeo mazuri ya dhamani. Wala usibabaishwe na wanaovuna haraka, mbegu yako si ya kawaida ina vitu vya dhamani. Kwa hiyo kama unaomba maana yake kuna vitu vya dhamani unavipanda ndani yako, inawezekana kabisa kuna watu wanakubeza na kukucheka lakini hawajui kitu ulichobeba niche dhamani sana. 

Tuangaie kile kitabu cha Mika kuna jambo zuri sana la kutia moyo na Bwana analiachilia kwaajili yako 

Mika 7:7-8Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia. Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, Bwana atakuwa nuru kwangu. 

Kuna watu ambao wameanguka KIUCHUMI, KIMTAZAMO, KIELIMU lakini Bwana anasema kuna saa yakusimama tena. Kama adui zako walifurahi kwamba umeishiwa huu ni wakati wako wa kusimama tena. Bwana amekushusha ili uweze kujua maadui zako, Bwana anataka ujue wale walio karibu yako. Ukiwa umebarikiwa hauwezi kujua miyoyo ya watu. Ukiwa na kitu hata kama umekosea wanakutetea ndiyo maana Bwana leo amekupitisha ili uweze kuwajua walio upande wako. 

Kuna wakati Mungu anafunga Baraka zako ili uweze kujua wale ulionao kama wamekufuata kwaajili ya kukupenda au walikufuata kwaajili ya mkate (Fedha), kama ambavyo walimfuata Yesu kwaajili ya mkate. 

9. KUBADILISHWA JINA LAKO

Napoishi kwenye maisha yako kuna majina umepewa lakini si majina yako. Kwa kuwa kila jambo linatambulikana kwa jina. Inawezekana kutokana na tukio ulilopitia unaitwa kwa jina hilo, inawezekana ulipitia hali ya ugonjwa na ukaitwa mgonjwa. Kwa hiyo kuna majina yanatokana na hali yako au tukio lilotokea kwako kipindi fulani. Kama ambavyo kuna majina mabaya kuna majina mazuri, ndivyo hivyo hivyo kama ambavyo kuna matokeo mabaya na mazuri pia yapo. Hakuna mtu alitaka kuitwa mgonjwa lakini kutokana na tukio la wewe kuugua ukaitwa mgonjwa. Hakuna aliyetaka kuwa masikini lakini kwasababu ya umasikini wako umeitwa masikini ambalo ni jina uliloitwa.

Isaya 62:2-4

Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; NAWE UTAITWA JINA JIPYA, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 

Mungu ataandaa tukio na watu watakuita jina lingine kwa jina la Yesu. Mungu hataruhusu utukufu uwe juu yako hakuna mabaye anaweza kubadiliha jina pasipokuwa na utukufu wa Mungu. Yusufu aliitwa Bwana ndoto, jina lake lilibadilishwa na akaitwa mwenye akili. Mungu ataleta tukio kwako na kila mtu atashangaa na wengine watakuita fremasoni kwa maana Bwana amekubariki. Yesu anavyo vya kutosha na atawashangaza wengi kwenye maisha yako. 

Kwa kuwa utukufu wa Mungu huko juu yako hautaitwa jina la zamani tena bali utapewa jina jipya tena litakalotajwa na kinywa cha Bwana.
Ezekieli 34:16 Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.

Bwana anataka urudi kwenye kusudi lako la Baraka, kusudi lake la ndoa, kusudi lake la wewe kuwepo. Ndiyo maana Bwana anawatafuta waliopotea ili wapete kurejea kwa jina la Yesu. 

Yesu alipofika kwa lazaro ilikuwa takribani siku ya nne tangu Lazaro afariki, na alipokwenda Yesu alikuta Lazaro ananuka. Alikuwa ameshabadilishwa jina na kuitwa maiti.  

10. POKEA VIWANGO VYA ROHO MTAKATIFU 

Hii ni hatua ya mwisho na kifurushi cha mwisho, na katika kupokea Roho Mtakatifu kuna mambo mbali mbali ambayo unaweza kupokea. Roho Mtakatifu anapo kupandisha kiwango kuna mambo yanatokea katika viwango vyake 

Utapokea nguvu 

Matendo 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. 

Kuna nguvu ya ajabu utapokea ambayo si ya kutenda mambo madogo ambayo wewe unayaweza ni mambo makubwa ambayo yatawashangaza wengi. 

Kufanya makubwa yanayopita akili za mwanadamu 

Kuna mambo utafanya na wanadamu watashangaa, Petro na Yohana wakati wanakwenda kusali hekaluni walikutana na kiwete ambaye alikuwa akiomba omba pale na wao wakamuambia.

Yohana 14:16Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 

Utapokea elimu Roho Mtakatifua si elimu ya wanadamu 
Kuna mahali utaingia na utanena jambo mpaka wenye hekima watashangaa

Luka 12:12kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema. Kuna migogoro utaitatua na wengi watashangazwa na hekima yako. 

Kujazwa na kunena kwa lugha mpya yakuwasiliana na Mungu wako pasipo wengine kujua 
Hii ni lugha ambayo ni yakimbingu ya mtu na Mungu wake. Kwa hiyo nikisema naomba gari, nyumba na mengine utajua lakini nikinena kwa lugha hakuna ambaye ataelewa, hata wachawi hawajui kwasababu hii ni lugha ya kwako pekee na Mungu wako. Na unaponena kwa lugha hata mwili wako, nafsi yako haielewi ni Mungu pekee anayejua, unapoomba kwa Roho Mungu anafanya makubwa zaidi kuliko unayofikiri. 

Matendo ya Mitume 2:8Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 
Kesho tutaangalia maandalizi kabla ya neema yako, namna ambavyo Mungu anakuandalia maisha yako kabla ya wewe kuwa Mbunge, Mafanyabiashara n.k. Yule anayeandaliwa anakuwa mzuri kuliko ambaye ajaandaliwa. Daudi aliandaliwa na ndiyo maana akatawala vizuri hivyo hivyo kwa Yusufu. Tutaangalia kesho juu ya jambo hili funua Yakobo 4:6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. 

Mara nyingi mtu yeyote akiinuliwa pasipokupitia mahali kuna kiburi ndani yake, tofauti na yule aliyepitia mapito fulani. Ni lazima Mungu akupitishe hili uweze kuwa na Roho ya unyenyekevu. Mungu ataachilia neema juu yako bila kukuandaa na kushughulika na kiburi. 

Wakati wa kuandaliwa utaona ni mateso aibu na udhia lakini Mungu anakuangalia moyo wako ili apate kujua namna ulivyo. Mungu anapokujaribu na kukupa alafu akaona umechanganyikiwa anakunyima na kukuandaa tena. 






No comments: