MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

MAANDALIZI KABLA YA NEEMA



Mungu uwaandaa watu wake kabla ya Neema. Baraka ndani ya mtu ni neno ambalo ametamkiwa na wala si mali ambazo mtu anapewa. 

UNYENYEKEVU MBELE ZA BWANA 

Mithali 22:4Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima. 

Kabla ya kupokea heshima yako na utajiri wako Mungu anataka kuona moyo wa unyenyekevu ndani yako ambao huko tayari kupokea. Si wote wanaweza kuandaliwa pamoja na kwamba matukio ya shida yanaweza kuwapata wote. Mungu anaweza kutuma neno la Baraka na ukasikia nguvu ya kupokea hiyo Baraka na baada ya hapo ndipo unaingia kwenye maandalizi ya kuipokea hiyo Baraka. 

1 Petro 5:5-6 Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; 


Petro anaongelea kwa habri ya vijana kunyenyekea wazee. Mungu anapokuwa anakuandaa anaondoa Roho ya kiburi ndani yako na kuweaka roho ya unyenyekevu ndani yako. Unapojikweza Mungu atakushusha ili upate kujifunza pale unapokuwa umeshushwa. Sasa ni kiburi kipi kipo ndani ya mtu

·     Mungu amekuambia uje kwenye ibada wewe unasema siendi 
·     Unaama kanisa kwaajili ya makwazo kwamba siendi tena mahali pale kwaajili ya makwazo ukikimbia makwazo huko hata hapa yapo makwazo. 
·     Kususa kwaajili ya Uzima ndani yako, afya uliyonayo na mengine yanayokuzunguka 
·     Kukataa kutumika ingawa Mungu anataka kukutumia. 

Unapokuwa na moyo wa unyenyekevu utamuheshimu kila mtu na kumthamini kwasababu hauwezi kujua mtu huyo kesho ni nani.  

Ushuhuda 

Kuna Dada mmoja ambaye alitaka kuolewa na waziri na akaomba maombi yake ili haweze kuolewa na waziri. Akampata kijana ambaye alitaka kumuoa na akamkataa na akaoolewa na kijana mwingine ambaye hakuwa waziri lakini baada ya muda mfupi akawa waziri, hivyo na yeye akawa mke wa waziri. Kipindi fulani wakati wakaenda kwenye mgahawa na wakiwa wamekaa wanakula Dada huyo akamuona yule mwanaume aliyetaka kumuoa akamwendea na wakasalimiana na kufurahiana sana.  Wakati wanaondoa akamuelezea mume wake yule ndiye alitaka kunioa kipindi fulani. Mume wake akamuambia angekuoa ungekuwa kwenye mgahawa huu kwa sasa. Mke wake akamjibu akasema hapana bado ningekuwa mke wa Waziri kwasababu maombi yangu mimi nilitaka kuolewa na waziri hivyo basi kijana huyu angekuwa waziri kama ningeolewa naye. 

Tafakari kwa kina jambo hili. 

Unyenyekevu ndiyo utajiri na heshima na Mungu anawainua ambao wananyenyekea. Ukiwa myenyekevu ni rahisi sana kwako kusikia kile unachoambiwa na Mungu wako. 

Mithali 18:12 Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu. 

Hauwezi kupokea heshima kama hauna Roho ya kushuka ndani yako. Kabla ya kupaa heshima moyo wa kunyenyekea lazima huwe ndani yako. Heshima hautaipokea kwenye ndoa, huduma, biashara, kazi mpaka moyo wa unyenyekevu utokee. Neema ya mtu imeambatana na heshima. Na hili uweze kupokea heshima lazima upitie kwenye mchakato fulani wakati unaelekea kwenye Neema yako. Ndipo UTASIKIA MTU AKISEMA “WE NIACHE TU NAPITIA SANA” Haya yote yanakupata ili usiweze kujiinua. 

Mithali 29:23 

Na hautaweza kutoka katika mchakato huo bila ya Mungu kuupima moyo wako. Ni lazima Mungu akupime kwanza upite kwenye darasa na kufanya mtihani. Kila anayeomba Mungu anamjibu tatizo ambalo lipo ni unyenyekevu wa mtu kupokea.


MIFANO YA WATU WALIOFANIKIWA KUPITA CHUO CHA MAFUNZO 

Mwanzo 25:30, 27:11-19 

Esau alikuwa mzaliwa wa kwanza na akaudharau uzaliwa wa kwanza kwaajili ya njaa ambayo alikuwa nayo. Ni kama vile leo kwaajili ya njaa unadharau kanisa, maombi kwamba yatanifaa nini mimi nimeomba sana. Lakini hakujua kwamba ndiyo anauza haki yake na Baraka zake. 

Kwenye mlango wa27:11-19 Tunaona namna ambavyo Isaka alitaka kumbariki mzaliwa wa kwanza na akamuita na kumtuma chakula kitamu. Mama yake Yakobo Rebeka anasikia habari hizi na kwa kuwa yeye alikuwa anajua tangu tumboni kipi kilitokea hivyo akamuita Yakobo na kumuambia afanye kama ambavyo Esau ameagizwa. Yakobo kwa unyenyekevu anamuambia mamaye “Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini.  Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka”Angalia namna ambavyo Yakobo alinyenyekea mpaka mamaye akamuambia laana yake na iwe juu yake. 

Yakobo amebarikiwa na Babaye bado hata Mungu ajamtokea na kusema naye bali mamaye ndiye alisema na anakimbilia kwa mjombaake Labani kwa kusingizo cha kwenda kuoa lakini mamaye alisimia ndugu yake akitaka kumaliza. Yakobo alifika mahali akalala na tazama akaota ndoto ikisema “Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua”

Yakobo akatoka mahali pale na kuelekea kwa Labani na akaanza kutumika kwa kusudi la kumpata Raheli. Yakobo anatumika miaka saba kwa Raheli lakini anapewa Lea na Yakobo anapewa sharti lingine kwamba lazima amtwae mkubwa kwanza kabla ya mdogo. Akatumika tena miaka saba tena ndipo akampata Raheli wala hakulalamika bali alinyenyekea. Wakati wa kutoka kwake Yakobo kwa mjombaake Labani Mungu alimpa utajiri kwa njia ya ajabu sana na hayo yote yalitokea kwasababu ya Yakobo kusikia sauti ya Bwana. Yakobo alipewa mitihani ya ajabu lakini yote alifaulu. Mungu aliachilia wazo ndani ya Yakobo ambalo hakushindana na mtu. 

ANGALIA MTIHANI WA IBRAHIMU KUMTOA ISAKA

Huu ulikuwa ni mtihani wa ajabu kumtoa Isaka kama sadaka, Mungu alimuambia Ibrahimu akamtoe mwanae wa pekee ambaye alimpata akiwa katika uzee. Kwa hiyo Ibrahimu akaondoa na kwenda kumtoa mwanae sadaka huko horebu 

DAUDI
Daudi alikuwa akichunga kondoo na akapakwa mafuta ya kifalme, Daudi anapitia mitihani ingawa alikuwa ni kijana mdogo asiyejua vita. Daudi anakwenda kuwapelekea nduguze chakula vitani anamkuta Goliathi akitukana majeshi ya Israeli. Daudi anakwenda vitani na kumuua Goliathi na baada ya hayo mfalme anamuinukia na kutaka kumuua Daudi ambaye ameiondolea Israeli aibu. Sauli Roho mbaya kutoka wa Bwana ikamshukia na akaanza kumkimbiza Daudi ili kumuua na Mara kadhaa Mungu alimtia Sauli mikononi mwaka lakini Daudi alinyenyekea wala hakumgusa Sauli. Soma 1 Samweli 17:1-58, 1 Samweli 18:10-11, 29.  


Nakushauri kama ulipewa mtihani na ukashindwa ni muhimu sana kwenda mbele za Bwana kwa toba, usikubali ujasiri ndani yako nenda mbele za Bwana kwa toba yeye ndiye anayeweza kusahisha mtihani wako. 

No comments: