MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

KUFUTA HUKUMU YA SHETANI




Kuna hukumu ya shetani na kuna hukumu ya Mungu, hukumu ya shetani ni kinyume na hukumu ya Mungu. Hukumu ya Mungu inatokana na mtu kutenda mabaya juu ya Mungu wake au kwa lugha nyepesi dhambi. 

Kama kuna hukumu kuna mtu anahukumiwa, na kama iko hukumu kuna mtu anaye hukumu vile vile kuna gereza la kuweka mfungwa baada ya hukumu. Shetani anaweza kuhukumu;
·     Ndoa yako 
·     Kazi 
·     Elimu
·     Huduma
·     Karama 

Isaya 42:22Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.

Hautawekwa kwenye gereza pasipo kuhukumiwa na kama umewekwa kwenye gereza hauja hukumiwa maana yake unasubiri hukumu yako.

Isaya 61:1Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 

Mfungwa hawezi kujifungua mwenyewe mpaka awe na mtu wa kumfungua na kuifuta hiyo hukumu ambayo mtu amehukumiwa kwayo. Wako watu waliofungwa lakini Mungu anatangaza kufunguliwa kwao. Magereza ya mateso yatawekwa mbali na wewe mbali na kuonewa. 

Matendo 26:4- 9, 10-18 
Kwa maana Wayahudi wote wanajua maisha yangu tangu ujana, yaliyokuwa tangu mwanzo katika taifa langu huko Yerusalemu, wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa. Na sasa ninasimama hapa nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi baba zetu waliyopewa na Mungu, ambayo kabila zetu kumi na mbili wanataraji kuifikia, wakimwabudu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, Ee Mfalme. Kwa nini limedhaniwa kwenu kuwa ni neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu? Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti; 

Haya ni maneno ya Paulo ambaye alikuwa akitumikia ufalme wa shetani kabla Yesu hajamuokoa lakini alipogeuka na kuokoka, vita ikainuka juu yake na wakamshitaki ili kumuhumu. Ndivyo ILIVYO KWAKO, KUNA HUKUMU UNAHUKUMIWA KWASABABU YA WEWE KUOKOKA. Kuna watu wanashitakiwa kwasababu wanaenda kanisani sana, kwasababu wanaomba sana hayo ni mashitaka yashetani. 

Paulo anasema kwenye ule mstari wa kumi kwamba aliwafunga wengi kwenye magereza. Maana yake kuna watu walihukumiwa na kufungwa kwenye magereza kama ambavyo wewe unaweza kufungiwa kwenye magereza ya mateso. 

Paulo anaendelea kusema kwamba “nikiisha kupewa amri na wakuu wa makuhani; na walipouawa nalitoa idhini yangu” Kwa hiyo wapo waliopewa amri kwaajili ya kufuatilia maisha yako na wao wanatekeleza lile ambalo wanaambiwa na Kuzimu. 

Hukumu ambazo unatakiwa kufuta 

1.     Hukumu ya kifo 
·     Kwenye kazi 
·     Ndoa 
·     Biashara 
2.     Hukumu ya mateso 

3.    Hukumu ya kutofanikiwa
4.    Magereza tunayovunja 
5.    Magereza ya kichawi
6.    Ndoto za kila aina za kichawi. Kuota kula usiku, nyoka n.k

Greza la umasikini kila unachofanya haufanikiwi

Greza la mizimu unaota watu waliokufa. Wale ambao wamekufa lakini unawaota ilo ni gereza la mizimu, chcochote unachoota kuhusu hao wafu ni mizimu. 

Gereza la watu wabaya. Kila unayekutana naye anakuwa mbaya kwako hilo ni gereza. 

MASHIMO 
Mashimo ya kuonewa. Kila mahali unapokwenda unaonewa, Roho ya kuonewa ni shimo 

Shimo la Nguvu za giza. Unaishi na mtu kumbe ana nguvu za giza, maandiko yanasema adui wa mtu ni wanyumbani mwake ndiyo maana kila unachokifanya hakifanikiwi kwaajili ya shimo hilo. 

Shimo la utasa au kuzaa mapooza 

Hili ni shimo utasa kwenye mahusiano, biashara, kutokuzaa. Kuna watu amabo wanaomba lakini maombi yao yanaishia kwenye mashimo ya utasa. 

MATEKA 
Madhabahu ya wachawi, miungu, waganga wa kienyeji, madhabahu za uovu

Hayo ni madhabahu ambayo yameteka watu kwaajili ya mabaya. Kuna madhabahu ambayo inakaa ndani ya moyo wa mtu na ndiyo maana Bwana amesema hatavunja moyo wa jiwe na kuweka moyo wa nyama. 
























No comments: