MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

KUPOKEA NGUVU YA KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU (KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU)




Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 

Kuna watu wamekaa kwenye hali fulani kwa muda, inawezekana ni kwenye umasikini umekaa kwa muda mrefu au kwenye changamoto yeyote ambayo umekaa muda mrefu. Leo unakwenda kutoka mahali ulipokaa kwa muda mrefu. 

Kuna mambo matatu yanatokea Mungu anapotaka kumuamisha mtu ambayo ni
1.    Mtazamo wako kubadilika.
2.    Utakuwa na bidii ndani yako isiyokuwa yakawaida.
3.    Utakuwa na maono (macho ya kuona mbali). 

Mambo haya hayawezi kutokea pasipokuwa na nguvu ya Mungu. Tuangalie maandiko haya namna ambavyo Yesu alibadilisha maisha ya mtu aliyekaa kwenye shida kwa muda mrefu. 

Yohana 5:3-12Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.] Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo. 10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro. 11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende. 12 Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani? 


Mungu anapomuamisha mtu ni kinyume cha utaratibu wa binadamu ambao wanautumia. Na leo Mungu anatafuta mtu miongoni mwetu ili aweze kumuamisha. Yesu anaelewa kwamba yapo magonjwa umekaanayo kwa muda mrefu. 

Yesu anajua ni muda gani umekaa na changamoto yako na ndiyo maana anakuuliza kama unataka kuwa mzima. Yesu anahitaji kuona namna ambavyo huko tayari, ndiyo maana Yesu akumuuliza kama anataka mtu wa kumtupa kwenye birika bali alimuuliza kama anataka kuwa mzima. Ndivyo ambavyo Yesu anakuuliza leo unataka kuwa tajiri, unataka kuwa na ndoa, unataka kuwa yule au vile. 

Yesu alipomuuliza huyu kiwete kama yupo tayari kupona alitoa hoja ambazo kwake alizijua niza msingi kulingana na mazingira ambayo alikuwa nayo, alimuambia Yesu hivi “Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu”Unaona namna ambavyo mtu huyu alijibu ndivyo ambavyo wewe unajibu mara kwa mara kwamba Bwana tatizo si utajiri sina watu wa kunipa mtaji au mkopo. Yesu alimpa majibu ya kushangaza sana alisema hivi “Simama, jitwike godoro lako, uende”Yesu anataka leo habadilishe historia yako na utoke ulipo na kwenda kwenye historia nyingine. Kiwete huyu alikaa kwenye hali yake kwa miaka thelathini na minane. Sijajua umekaa kwenye changamoto yako kwa miaka mingapi ninachojua mimi Yesu yule yule aliyemponya kiwete ndiye atakayekutoa kwenye hali yako. Sikiliza YULE KIWETE ALIPOPONA UGONJWA WAKE WAPO WATU WALIINUKA NA KUAZA KUSEMA JUU YA UPONYAJI WAKE LAKINI YEYE HAKUJIBU ALIWAAMBIA JAMBO MOJA “Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende”Kwa hiyo wapo watakaosema wakiona historia yako imebadilika. Kuwa tayari kuvuka kwenye historia yako ya miaka uliyopitia na changamoto ulizozipitia. 

MUNGU AKUBARIKI SANA NA AKUVUSHE MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU. 




No comments: