MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

KUPOKEA NGUVU YA KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU (KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU) SEHEMU YA PILI

Tunaendelea na sehemu ya pili ya somo letu la kuvishwa au kupokea nguvu ya kutoka mahali ulipokaa muda mrefu. Tuliangalia mambo matatu ya msingi yanayotokea pale Mungu anapokutoa mahali ulipokaa muda mrefu ambayo ni; 

1.    Mtazamo wako kubadilika.
2.    Utakuwa na bidii ndani yako isiyokuwa yakawaida.
3.    Utakuwa na maono (macho ya kuona mbali) 

Mungu anapotaka kukutoa mahali ulipokaa muda mrefu MAMBO HAYO YANATOKEA KWAKO. Ni kweli kwamba wako watu wanaoona umekaa mahali muda mrefu lakini Bwana ameshuka ili kukuhamisha ulipokaa.   

Twende tukaangalie maandiko kwenye kile kitabu cha Yohana ili niweze kukueleza mambo kadhaa kwenye kitabu hiki cha Yohana. Nitanukuu mistari kadhaa lakini wewe soma sura nzima ili uweze kupata picha yote. 

Yohana 9:1-411 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. 10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? 

Yesu alipokuwa anapita alimwona mtu kipofu, ninachotaka ujue hapa ni kitu kimoja Yesu anapopita kwenye maisha yako anajua historia yako. Wengi wanajua tangu kuzaliwa kwako ulikuwa masikini, tangu kuzaliwa kwako umekuwa mtu wa shida nyingi, toka kuzaliwa kwako unaumwa mangonjwa ya kila namna kila leo lakini YESU ANAPITA KWAKO NA KUBADILISHA HISTORIA YA MAISHA YAKO. 

Wanafunzi wa Yesu wanamuuliza juu ya ni nani ambaye ametenda dhambi kati ya kipofu na wazazi wake. Ni kama wewe unavyopitia na kujiuliza ndani yako kama umetenda dhambi au la! Kuna hali unapitia mpaka unajiona wewe ni mkosaji au wazazi wako na ndiyo maana wanafunzi wanahoji ili kuweza kujua chanzo cha tatizo. 

Siyo kila jambo ni kwamba mtu amefanya dhambi, kuna mambo yanatokea kwaajili ya utukufu wa Mungu ndani yako, na ndiyo maana saa yako ya kuinuliwa inakuja. Kama Mungu asipokupitisha utashuhudia kitu gani? Utakuwa na historia gani mbele za Bwana? Mungu ameachilia hayo ili wewe uweze kuwa mwamba, na ndiyo maana Yesu anaitwa mwamba Imara na sisi tumejificha kwake. Hakuna mishale inaweza kukupata ukiwa kwenye mwamba. 

Ukiwa kwenye mwamba ni lazima ujenge jambo ambalo litaonekana, na mimi najua kwamba kuna jambo unakwenda kulijenga na litaonekana juu ya mwamba. 

YESU ALIWAJIBU WANAFUNZI WAKE Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake. Na ndiyo maana kuna mambo yanakutokea nimesema siyo kwamba umetenda dhambi na Bwana anasema yanatokea hayo ili kazi zake zidhihirike ndani yako. Mungu hawezi kukudhihirisha bila kuwepo na jambo la kudhihirishwa. 

Hawawezi kuona utukufu wa Bwana kama hakuna mtu anayelia ili haweze kuwa na kicheko, Mungu anataka kumuona mtu mgonjwa ili uweze kuona uzima wake. 

IMETUPASA KUZIFANYA KAZI ZAKE YEYE ALIYENIPELEKA MAADAMU NI MCHANA, USIKU WAJA ASIPOWEZA MTU KUFANYA KAZI. Kuna anayeonewa lakini vile vile yupo ambaye amekuja kuzifanya kazi za Bwana ili ziweze kutimia. Ngoja nikuonyeshe kitu ambacho majirani zako wanajua na wale walikuzunguka na namna watakavyosema juu yako. 
BASI JIRANI ZAKE, NA WALE WALIOMWONA ZAMANI KUWA NI MWOMBAJI, WAKASEMA, JE! HUYU SIYE YULE ALIYEKUWA AKIKETI NA KUOMBA? Majirani zako wanaokufahamu wataulizana kwamba si yule aliyekuwa mgonjwa si yule aliyekosa kazi, si yule alikuwa mgonjwa. Ndiyo maana nilisema kuna mambo ambayo yatatokea kwenye maisha yako hata wewe mwenye haujaomba. 

Majirani zako watashangaa na wala hawataweza kuamini muujiza wako, hawataamini kwamba wewe una gari, wewe ni mbunge, Diwani au wewe ni tajiri. Nasikia nguvu ndani ya neno hili ninaposoma “WENGINE WAKASEMA, NDIYE. WENGINE WAKASEMA, LA, LAKINI AMEFANANA NAYE. YEYE MWENYEWE ALISEMA, MIMI NDIYE” Sikiliza neno la Bwana ninaposema neno hili ninaona MATAJIRI WAMEKETI MAHALI HAPA ninaposema neno hili ninaona WABUNGE WAMEKETI MAHALI HAPA. Wale majirani zako unaowaona hawataamini kwamba ni wewe, ndugu zako wanakujua hawataamini kwamba ni wewe mwenye utajiri wa namna hiyo. Wengine watasema siyo wengine watasema ndiye ndiyo maana mimi sishangai wanaponiita mimi MNAGERIA WAKATI NIMEKAA GONGO LA MBOTO NA WALINIJUA NALALIA MIHOGO. Ni wale waliokujua tangu utotoni lakini watasema wewe siye kwa namna ambavyo BARAKA ZIKO JUU YAKO. 

Ngoja nikuambie watu watakuuliza ni nani amekutendea hayo au imekuwaje umepata biashara, imekuwaje umepata uzao, wewe waambie haujui yupo mtu mmoja anaitwa YESU ULIPOINUA MACHO YAKO HAKAKUTOKEA. 

Kuna mambo yatatokea kwenye maisha yako wengi watashangaa wala hawatasadiki habari zako. Ndugu huyu huyu alipobadilika Mafarisayo hawakumuamini. Siyo kwamba wewe ulivyookoka kwamba wengi wamesadiki la hasha18 BASI WAYAHUDI HAWAKUSADIKI HABARI ZAKE, YA KUWA ALIKUWA KIPOFU, KISHA AKAPATA KUONA; HATA WALIPOWAITA WAZAZI WAKE YULE ALIYEPATA KUONA. 19 WAKAWAULIZA WAKISEMA, HUYU NDIYE MWANA WENU, AMBAYE MNASEMA KWAMBA ALIZALIWA KIPOFU? AMEPATAJE, BASI, KUONA SASA? 20 WAZAZI WAKE WAKAWAJIBU, WAKASEMA, TUNAJUA YA KUWA HUYU NDIYE MWANA WETU, TENA YA KUWA ALIZALIWA KIPOFU; 21 LAKINI JINSI AONAVYO SASA HATUJUI; WALA HATUJUI NI NANI ALIYEMFUMBUA MACHO. MWULIZENI YEYE MWENYEWE; YEYE NI MTU MZIMA; ATAJISEMEA MWENYEWE. 

Mistari hii inamaana kubwa sana, hata wazazi wako hawatajua namna ambavyo umepona hawatajua ni wapi umetoa utukufu ambao umeubeba. Ni kweli wewe ni mtoto wao ila usijaribu kuwaambia watu kwamba kawaulize wazazi wangu sikiliza hata wao hawajui ni wapi ulipoponea ugonjwa huo uliozaliwa nao, hawajui ni namna gani umekuwa tajiri wakati kwenye familia hakuna mwenye utajiri kama huo. 

Historia yako itabadilishwa na Bwana atakutengenezea historia mpya ambayo haibadiliki kwenye maisha yako. Umempata asiyebadilika YESU KRISTO WA NAZARETHI PEKE YAKE ABADILIKI.  




No comments: