MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

KUPOKEA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU

Kuna mambo matatu yanayotokea wakati unajiandaa kupokea nguvu ya Roho Mtakatifu. Mambo hayo ndiyo yanakuandaa kwaajili ya shahuku ya kupokea nguvu ndani yako. Tuangalie mambo hayo angalau kwa sehemu. 

1.     KUWA NA UWAKIKA KWAMBA ROHO MTAKATIFU YUPO. 

Kabla ya kumpokea Roho Mtakatifu ni lazima uwe na uwakika kwamba Roho Mtakatifu yupo. (Waebrania 11:6)   Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. 


2.     ROHO MTAKATIFU NI WAWOTE NA KILA AMTAKAYE ATAMPATA. 

Roho Mtakatifu ana uwaba siyo kwamba ameingia kwa yule hawezi kuingia na kwako. Roho yupo kwa kila mwenye mwili. Usiwe na woga kwamba fulani amembeba na amejazwa sana hivyo na mimi siwezi kumpata Roho Mtakatifu. (Matendo ya Mitume 1:8, Matendo ya Mitume 2:1-18)

3.     ROHO AKIINGIA NDANI YAKO KUNABADILIKO LITATOKEA. 

Hautaweza kufanikiwa pasipo Roho Mtakatifu kwa hiyo ukiona haujampokea Roho Mtakatifu unajichelewesha. Ni muhimu sana Roho kuwa ndani yako ndipo utaona mafanikio yako. Usijicheleweshe kuomba Amani pasipokuwa na Roho ambaye ndiye mwenye vyote. Kuna namna ya kuandaa shahuku ya Roho Mtakatifu na unapokuwa nayo isibadilishwe na mtu yeyote yule. 

4.     TAMBUA ROHO MTAKATIFU YUPO KILA MAHALI AMBAPO UNAWEZA UKAWEPO WEWE. 

Mfano rahisi unaweza usiwepo kwenye biashara wakati huu lakini Roho yeye yupo kwenye biashara. Unataka kwenda chuo, ulaya au mahali popote Roho Mtakatifu alishafika kabla ya wewe kufika. Unataka kuoa au kuolewa Roho Mtakatifu anamjua mume wako kabla ya wewe kuwa na yeye. Kama ambavyo unatamani mtu akusimulie ulaya ilivyo kama ametoka huko tamani na Roho Mtakatifu akusimulie yale ambayo haujayafikia kwasababu yeye amekwishafikia. 

Yale ambayo unatamani ndani yako kama mapenzi ya Baba yako Roho Mtakatifu anayajua hayo hata tarehe ya kutwaliwa kwako yeye anayajua yote. Ndiyo Maana Bwana Yesu akasema siwahiti tena watemwa bali rafiki zangu KWANINI kwasababu ametujulisha yote ya Baba yake. Yohana 15:14-16


5.     TAMBUA ROHO MTAKATIFU KAMA MUUMBAJI AMBAYE ANAWEZA KUUMBA CHOCHOTE KWA SAA YEYOTE. 

Roho alipotulia kwenye vilindi vya maji, Mungu aliposema na iwe nuru na Nuru ikatokea na aliposema na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu alipokuwa anasema jambo lilikuwa linatokea kwasababu Roho alikuwepo kutekeleza.Mwanzo 1:2-31Ezekieli 36:26

Naona jambo linatokea kwa mtu Roho Mtakatifu anakaa kwenye vilindi vya moyo wa mtu. Roho akikaa ndani yako vipo vijito vya uzima vitatiririka ndani yako. Roho akikaa ndani yako kuna jambo linatokea unaposema kwasababu Roho yupo kwenye vilindi vya moyo wako. 

Mungu hakujaze shahuku leo ndani ya moyo wako na narudia tena hakuna jambo ambalo linaweza kutokea pasipo Roho KUKUATAMIA. Ndiyo maana ukisikia wazo fulani nenda ndani ya moyo wako na utizame. Nuru iko ulimwenguni lakini watu wengi wamependa giza na kuacha Nuru. (Yohana 3:19) Mungu anataka kuondoa giza ndani yako na kuweka Nuru. 

Mungu akubariki sana tuonane kwenye ibada ya kesho kwaajili ya mashangilio ya wema wa Bwana na kwa stahili hile hile tunateka na kutawala. KWA STAHILI HIIIIIIII



No comments: