MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

KUPOKEA NGUVU YA KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU (KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU)

Tulianza somo hili la kupokea nguvu ya kutoka mahali ulipokaa muda mrefu (kutoka mahali ulipokaa muda mrefu) na leo tunaendelea na sehemu nyingine ya somo. Ngoja nikukumbushe tulipotoka. Tuliangalia kwamba Kuna sababu za kukaa mahali muda mrefu ambazo ni;

1)   Kukosa nguvu ndani yako 
2)   Malango ya mtu kufungwa au mtu kukosa njia ya kutokea 
3)   Macho ya mtu kufungwa na kuridhika kukaa ulipo 
4)   Kuzuiliwa na adui zako usite mahali ulipo 
5)   Kufungiwa milango au malango yako na adui zako 

Hizo nisababu za mtu kukaa mahali muda mrefu na tuliangalia pia mambo matatu yanatokea Mungu anapotaka kumuamisha mtu ambayo ni
1.    Mtazamo wako kubadilika.
2.    Utakuwa na bidii ndani yako isiyokuwa yakawaida.
3.    Utakuwa na maono (macho ya kuona mbali) 


Na jana tuliangalia namna ya kupokea nguvu ya Roho Mtakatifu. 

No comments: