MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

HATMA YAKO

Na Pastor Lambati Ileta 


Watu wengi hatima zao zimepotea lakini bado hawajajua ni wakati gani wa kurejesha hatima zao. Maandiko yanasema watakujia kwa njia moja watatawanywa kwa njia saba. Kama hatima yako ulipoteza kwa njia moja leo urejeshe kwa njia saba. Lakini ili uweze kurejesha kwa njia saba lazima ujue ni kwa njia gani au mlango gani ulipotezea hatima yako. 

Juzi wakati Baba anafundisha Somo la Roho Mtakatifu kutoka kwenye kile kitabu cha Mwanzo, Roho Mtakatifu alikuwa ananisemesha vItu kadha wa kadha na baada ya muda yakatoweka lakini leo tena yakarudi nikajua kuna jambo kwenye neno hilo. Ngoja nisome tena mahali pale ili nisimamie hapo. 

Mwanzo 1:1-51Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. 

Kuna nguvu katika giza na yapo mambo ya siri katika giza, hatima za watu kupotea katika giza. ROHO MATAKATIFU ALIKATAA. Roho Mtakatifu aliketi juu ya vilindi vya maji ili giza lisimeze. Na leo Roho Mtakatifu atulie juu ya uzao wako kwa jina la Yesu, juu ya kazi yako kwa jina la Yesu. 

Giza si jema na leo utaona namna ambavyo giza siyo zuri kwani kuna hatima nyingi zimefichwa kwenye giza. KWA JIONI IKAWA ASUBUHI, hapo ndipo penye siri kwasababu kwenye kufunga na kufua papo hapo. Kwenye kufunga na kufungua biashara pamefichwa katika siri hii, ya giza na nuru. Siku imebeba hatima ya mtu na mafanikio yake yapo ndani ya siku. Watu wengi hawachoki mchana wanachoka usiku jiulize ni kwanini? Mchana unafanya kazi lakini hauchoki WALA KULALA LAKINI. Usiku ndiyo majira ambayo vita vinapiganwa kwenye ulimwengu wa Roho. 

Mwanzo wa siku unafananishwa na mzaliwa wakwanza kama lango. Ukiweza kutawala usiku mchana hautakusumbua kinyume chake ukishindwa kutawala usiku mchana umeshindwa kabisa. Kama ukishindwa kutawala usiku mchana wako niwamaangaiko kwasababu hatima ya mchana inatengenezwa usiku. Usiku wa manane kwa maana wakati wa kubadili majira ndipo adui anapanda vya kwake. 

Luka 22:44-5344 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.] 45 Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni. 46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni. 47 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu. 48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? 49 Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga? 50 Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. 51 Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya. 52 Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang'anyi? 53 Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza. 


Huyu ni Yesu ambaye aliona maisha yake yanataka kuingia giza akaomba ili haweze kulitawala giza. Walilala usingizi wanafunzi wake hawakuomba na kuingia rohoni kwa hiyo hata wakati Yuda amekuja kumsaliti yeye alikuwa bado Rohoni na hakuwagusa lakini wanafunzi ambao walilala na wakiwa mwilini wakakamata mapanga kujua ni vita ya mwilini. 

Angalia ule mstari wa 53 Yesu alivyowaambia “Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza” 

Saa ya mamlaka ya Giza ni usiku na ndiyo maana viko vitu vingi sana vinatendeka wakati wa usiku na adui ndiyo wakati wa kutafuta hatima yako. 

Kwenye kile kitabu cha wafalme utaona namna ambavyo wale wanawake wawili ambao mmoja mtoto wake alikufa kwa kumlalia usiku. Sasa sijajua ni mara ngapi umelalia Biashara yako usiku wa manane. Hii siyo issue sana ya yule mama angalia kwa upande wako ni mara ngapi umelalia hatima yako usiku wa manane. 

1 Wafalme 3:19Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. 

Hatima ya mtoto huyu iliishia hapo kwasababu mama yake alilala na kumlalia mtoto. Ndivyo ilivyo kwako unapomlalia mtoto wako, iwe ni biashara, huduma, karama unapolala bila kuhakikisha kwamba mtoto wako yuko sawa hatakufa. 

Angalia jambo lingine huyu mama anaamka usiku na kuangalia anakuta ana mtoto, hatima za watu wengi zinamezwa kwasababu ya usingizi mzito. Unaingia chumbani hata kuomba hauombi kwasababu ya usingizi mzito. Unalalia kazi yako na unaamka asubuhi hauna kazi tena, hauna biashara tena. Sasa angalia yule mwanamke wa pili ambaye aliibiwa mtoto wake hapa nataka ujifunze mambo mawili makubwa.

1.    Mtoto kuibiwa usingizini. 
2.    Mtoto kufa kwaajili ya usingizi.

Hayo ndiyo mambo makuu niliyoyasema kwenye kufunga na kufungua siku hivyo basi uhalisia wa mambo unavyaona mchana mara nyingi yamefanyika usiku. Mchana ni muda wa kudhihirishwa tu.  Huyu mwanamke mwingine japo alipata ushindi mi nataka uangalie kitu kimoja kama mfalme hakuwa na hekima kitu gani kingetokea kwenye hatima ya yule mtoto. 

Hauwezi kutawala mchana wako kama usiku ulilala vya kutosha. Ni muhimu sana uka amka usiku na kulaani na kubatilisha mipango yao wakati wa majira kufunga na kuingia majira ya siku nyingine usiku. 
 
Pastor Lamart Ileta na Mke wake Happiness Lambart 
Angalia Isaya 29:15Ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye? 

Unaona namna ambavyo wanasema usiku kwenye giza kwamba hakuna ambaye anawaona. Kuna watu ambao hawatendi kazi mchana kabisa na ikitokea wanatenda kazi basi wamekamatwa. Mchawi hawezi kuloga nyumbani kwa mtu mchana hawezi. Kuna idara ambazo ni idara korofi zinazotenda kazi usiku ili kuharibu vitu vya watu;

1.    Idara ya wachawi
2.    Idara ya ugavi wa vyakula vya kipepo kwa ajili ya kupanda magonjwa. 
3.    Vinyozi wakipepo.
4.    Majini mahaba (Wanawake au wanaume wakipepo) 
5.    Idara ya watoto wakipepo
6.    Sherehe (washereheshaji wa kipepo na sherehe zao wanaosherekea kushindwa kwako) 

Tunakwenda kutembelea hizi idara na kuharibu kabisa utendaji kazi wa idara hizi na kuzilaani ili zisiweze kutenda kazi tena kwenye ulimwengu wa Roho katika jina la Yesu. 

Idara hizo nilizozitaja hapo juu ni idara yeti saana na ukianza kuichambua kila moja namna inavyotenda kazi usiku ni somo la siku kadhaa kwa kila moja. 



No comments: