MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, August 31, 2014

I WANT MORE ENEMY

Ni maisha yanayofanya binadamu kutafuta jinsi ya kuishi na ni maisha yanayomfanya binadamu kumkosea binadamu mwenie ni maisha haya haya utamtambua rafiki na adui but ni maisha haya Mungu humbariki binadamu kwa namna zote za rohoni na mwilini lakini maisha haya yanaweza kukufanya kujua rafiki na adui na maisha haya haya yanaweza kukufanya kujua kushoto na kulia sasa mimi nimejua marafiki na wanafiki .

Wandugu kwa utangulizi wa hapo juu kidogo unaweza kushtuka na kujiuliza maswali mengi kimemkuta nini kaka lema , ki ukweli sikujua kama ningeweza kujua ukitaka kufanikiw katika maisha lazima uwe na maadui , na mimi napenda maadui kwasababu Mungu uandaa meza mbele ya adui zangu kila adui ajapo kwa njia moja sharti aondoke kwa njia saba na mimi naamini neno hilo , it is very important to have enemy because they make you to grow.

Watumishi wa Mungu kama auna adui then you have nothing lakini ukiwa na adui inamaanisha lazma unakitu ndani yako the enemy will never look for nothing they will always be there for something 

Ukisoma biblia kidogo Mwanzo mlango ule wa 26 na kutafakari maadui hutoka wapi utaona mtumishi wa Mungu Isaka katika kipindi cha njaa kubwa alitaka kukimbia na Bwana alimtokea akamwambia akae katika nchi atakayomwambia na akasema atakuwa pamoja nae na atambariki na akamuhahidi kumpa nchi hiyo yeye na uzao wake na Isaka alikaa maali pale kwenye nchi hile na alibarikiwa sana mpaka wafilisti walimuhusudu kwa kuwa alikuwa mkuu sana , ilifika kipindi mfalme wa nchi hile akamwambia Isaka atoke kwao maana yeye ananguvu sana

Lakini ukisoma biblia tena kuhusu habari za Daudi katika kitabu cha Samweli 2 mlango wa 5 Daud ivyowekwa mafuta ili awe mfalmejuu ya Israel wafilisti walipanga kumuangamiza .

Ukiangalia kwa upanda juu ya story zote mbili utagundua kuwa kila mtumishi wa Mungu anapo barikiwa basi shetani lazima alete taflani fulani katikati , na shetani amfuati mtu ambaye ana kitu lazima amfuate somebody mwenye something na ukiangalia kwa makini hata shetani aliweza kumgusa Ayubu na kumwambia Mungu kwasababu tu amembariki Ayubu ndo sababu ya yeye kumtumikia lakini bila kusahau Moyo wa Ayubu ulikuwa kwa bwana na alikuwa mtii sana.

Ni maombi yangu kwako Mungu wangu kila adui anayekuja kwa  njia moja atatoka kwa njia saba baba aliemtakatifu sana atatujalia haya ya miyoyo yetu kwa ajili yetu na taifa letu . Mungu wangu na baba yangu naomba kwako , kila adui aliyeinuka kinyume nami aishi na kushuhudia hukuu wako kwenye maisha yangu nasimama baba kama mtumishi wako na kutangaza hukuu wako na nahitaji msaada wko bwana wa majeshi katika kila aibu ambayo shetania ameniweka nami narudisha kwao mara saba katika jina lako takatifu Baba najua kwa kila Daudi na Goliathi baba najua kwa kila Musa kuna Farao baba najua kwa kila pito kuna msaada toka juu mbinguni Baba najua kwa kila pigo kua kupona Baba nami najua kwa kila jaribu kuna ushindi further i know in every test there is a testimonies . BABA tupe nguvu ya kumshinda Goliath baba tupe nguvu maana watajaribu kucopy lakini awataweza baba watajaribu kufanya kama sisi lakini awatakuwa na nguvu mfalme wa amani watajaribu kushindana lakini awatashinda JEHOVA , kwania ata Farao naye alikuwa na nyoka lakini yoka wa Musa aliwameza nyoka wote wa Farao baba . Nguvu zako ndiyo nguzo imara   


Kila mara Mungu huwa upande wetu na ukiamini kuwa yeye ni yule jana leo na hata milele basi katika shida yako ukiliitia jina la Bwana atakuokoa na utakuwa imara kwa kila yanja , Mungu wangu wa Mbnguni akubariki sana na kukupigania katika kila jambo

No comments: