MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, March 13, 2014

KURASA INAFUNGWA KURASA INAFUNGULIWA

Nawasalimu katika jina la Yesu Kristo wapenzi wa Lema one blog ok nimekuwa busy kidogo na mambo ya hapa na pale katika kulipeleka taifa letu mbele pia nilikuwa najaribu kufanya marekebisho ya blog ili kuendana na wakati wa sasa na i hope kadri siku zinavyokwenda tutabadilisha mengi

Ok ni majuzi tu nilitamani kupost kitu ambacho kilikuwa ndani yangu ila kazi zikabana na nikagusia kidogo juu ya ni nini roho yangu ilitamani kusema najua roho wa Bwana alitaka kunena na baadhi ya watu , kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania , Mwalimu mmoja mwenye upako na roho ya Kiungu ndani yake alipata fursa ya kufundisha kidogo juu ya ujio wa katiba mpya na nakumbuka tulipata mzigo wa kuombea taifa na wale walioko Dodoma kwaajili ya mchakato mzima wa kupata katiba ndani ya Nchi yetu , unajua mpendwa mambo haya ni ya muhimu sana na ni vyema kujua nafasi yako ya kuiombea nchi yako, katika hali ya kawaida kwasababu tuna amani wewe unaona hauko na mzigo wa maombi ndani ya nchi yako , yakupasa kutambua kwamba katiba mpya ni lango na katika ulimwengu wa kiroho shetani huwa asinzii kutaka vyake vipite katika lango hilo sasa kinacho fanyika hapo ni maombi  tu .

 Kutokujua si sababu ya sheria kutokufuata mkondo wake hama kufanya kazi juu yako wakati ulimwengu wa giza ukitawala yamkini ndo wakristo wengi huamka na kumlilia Mungu lakini wakati wa Kutegeneza katiba kama ilivyo sasa haa tunasema tunaangalia mchezo wa mjengoni usemi wa vijana wengi . Tambua kuwa kila ukurasa unapofungwa ni kama kumaliza Darasa la saba na kuingia form one kama ukujiandaa vyema basi kuna mambo mengi sana yatatokea juu yako maana mengi ni mageni . 

Nchi yetu iko katika misingi mizuri ya Imani maana kila mtu yuko na uhuru wa kuabudu sasa hapo mara nyingi Mungu anayetawala ni yule mwenye nguvu sasa utauliza mambo mengi wateule wakiwa wengi basi bwana ulinda ardhi hiyo isipatwe na madhara , ok embu tafakari safari ya wana wa Israel kutoka Misri ukisoma kwa makini Kutoka 31 kuanzia ule mlango wa 18 utaelewa Musa alikuwa akinena na Bwana Mlimani na alipokawia kushuka ndipo watu wale wakajifanyia Miungu ya sanamu , maana Musa alikwenda kupewa mbao na maangizo ili waendelee na ukurasa mwingine lakini taifa lili badala ya kuomba na kuwa na subira ingawa walishaona miujiza mingu Mungu aliwatendea walirudi nyuma na kulaumu na kisha wakafanya makosa na Mungu alitaka kuliaribu taifa lile na kisha amfanye Musa kuwa taifa kubwa . 
Nchi yetu inahitaji waombaji na si watazamaji hama walalamikaji katika kufunga na kufungua ukurasa mpya huu tulio nao tukimpa shetani nafasi yeye atafanya kazi maana yuko kazini usiku na mchana . Ni maombi yangu kwako wewe mtumishi wa Bwana kuinuka sasa na kuitetea nchii hii kwa maombi na kuomba Nguvu za Jehova zishuke juu ya taifa hili uwepo wake huwe na sisi katika safari yetu tusisonge bila uso wa bwana 

Ukurasa huu huwe wa viwango vya juu tunahitaji kusimama kwaajili ya hilo , wakati unaomba embu kumbuka kuombea toba nchi yetu kisha swala la katiba liweke mbele mtumishi wa  Bwana ili ukurasa ujao nchi yetu iwe ya amani kama ilivyo sasa .

God Bless you kwa haya machache najua umepata kitu ndani yako 

No comments: