MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Friday, October 15, 2010

DUUUUUUUU

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000
(Laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia. Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi yake.

Kisha akai-post barua ile. Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa
ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.


Barua ilisomeka hivi:

"Mpendwa Mungu,

Jina langu ni JANET, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika
jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania , bara la Africa .


Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.


Naomba sana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya
kazi na
kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
sana .


Natanguliza shukrani.

Wako mtiifu,


JANET."


Wafanyakazi wa posta walifurahishwa sana na barua hiyo na kisha wakaamua
waipeleke kwa Rais . Rais naye alipoipokea ilimfurahisha
sana na
kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani
kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi sana .


Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:

"Mpendwa Mungu wangu,

Nashukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba.
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya Tanzania .
Kama
ilivyo kawaida yao hao wezi, wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya
kodi ,
kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu.



Nashukuru saanai!!!!!!!!!!!

8 comments:

Kibár Mañuel said...

Kibár Mañuel hahahahaaa

Baraka Deo said...

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha iyo nzuri mno!

Revocatus Biro said...

Lema hii ni nima hebu nisukumie na mimi bana maana inafurahisha....! huyu mtoto alikuwa wa machame marangu au kibosho?

Happy Lema said...

Tehe tehe! Hii kali,nimeipenda.

Mutta James said...

Lemaaaaaaaaaaaaaaaa.... aaaaaaaaaaaaaaahh, you did make ma day bruv. lol

Arnold Alley said...

Sazy huyo mama akumfanyia fear coz kwanza atamtengenezea beef kali huyo dogo na sir god kwani atahic mungu awackilizi watoto.

Shileo Victor said...

hayo matusi sasa @ babie joy unajua warombo wote watakutafuta.!!!!!!!!!!!!! halafu Lema hizo siyo ishu wala nini?!!!!!!!!!!!!!

Babie Joy said...

Huyu lazima alikua Mrombo