MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, September 01, 2010

THIS TIME IS QATAR AIRWAYS IFTARI IN PARADISE CITY HOTEL

Ilikuwa furaha ya ajabu kwa watu hawa kukutana pamoja na kupata futari ndani ya kiota cha paradise city hotel mambo yalikuwa mazuri kabisa kwani watu walipata milo ambayo kamwe awakudhania inawezekana kupatikana hapa kwetu tanzania
Ndani ya ukumbe pendwa wa serengeti ball room ndipo tulipofuturu kwa pamoja na Qatar airways

watu walikuwa wengi sana na kila mtu alikuwa mwenye furaha ya hali ya juu kufika sehemu nzuri na yakistarabu kama hapa kweli hii ni paradise
Kulikuwana mapochopocho ya kila aina wenyewe wanaita buffet tour hii ni moja kati ya station nyingi za humo ndani
mambo ya Chef ayakuwa madogo kabisa ilikuwa ni high profile tuu kweli mambo yalikuwa mambo yalikuwa mambo
Chef Heriki alikuwa makini kwa upande wa chapati live
Huyu ndiye Shekh Francis(picha ya juu mwenye kanzu ) sasa sijui jina na dini vinaendana haya ni katika hali ya kuweka mambo sawa tu kwa ajili ya ndugu zetu
Machef walikuwa makini kuakikisha mabo yanakuwa kama yalivyo pangwa kiukweli mambo yalikuwa mazuri mno ndani ya kiota hiki cha maraha
Kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu, kufunga mwezi wa Ramadhan ni lazima kwa kila Muislamu mwenye afya njema na aliyekwisha balehe kama kwenye Qur aan surat Baqara aya 183 inavyosema “Enyi ambao mlioamini mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa wale ambao waliopita kabla yenu ili muwe wacha Mungu”.

Hata hivyo watu walioruhusiwa kutofunga ni pamoja na mtoto mdogo asiyefikia balehe, mgonjwa ambaye akifunga anaweza kuzidiwa, mwanamke aliye kwenye siku zake za mwezi (hedhi) au baada ya kujifungua (nifasi) pamoja na mzee asiyeweza ambaye hutakiwa kumpa masikini kibaba cha chakula kwa kila siku asiyofunga.

Kwa Tanzania kibaba cha chakula hufaa kuwa unga wa sembe au mchele kwani ndio huliwa na watu wengi zaidi.Mtume Muhammad (S.A.W) anasema kuwa kwa watakaofunga wataweza kuingia katika mlango wa Alrayaan ambao upo katika pepo na siku hiyo ya Kiyama patasemwa “Wako wapi wenye kufunga? Hataingia katika mlango huu mtu yeyote asiyekuwa wao”.

Kufunga huko ni kujizuia kula , kunywa, kutofanya tendo la ndoa pamoja na kuacha mambo yote mabaya yanayokatazwa ikiwamo kutukana matusi au kutembea uchi na badala yake ni kufanya mambo mema kwa kadiri ya uwezo wako. Kufunga huko huanza alfajiri mpaka Magharibi baada ya jua kuzama.

Mbali na ulazima wa kufunga kwa kila Muislamu, kuna mambo yanayoweza kuharibu funga ya mtu na kulazimika kuilipa swaumu hiyo iliyoharibika. Mambo hayo ni pamoja na kutoka katika Uislamu kuhamia dini nyingine, kujitapisha kwa makusudi, kufuturu kabla ya kuzama jua, kuingiza kitu tumboni, kujitoa manii na kufanya tendo la ndoa mchana.

Mtume Muhammad (S.A.W) anasema, kwa wanaodharau kufunga ikiwa ni kuiacha nguzo ya nne ya Uislamu ni kafiri na wanafaa kuuliwa na mali zao kuchukuliwa na pia mali yake anayotoa kwa ajili ya dini pamoja na shahada yake haikubaliwi.

Na kwa wale wanaoacha kufunga Ramadhan bure bila kuwa na sababu ya msingi inayokubalika kidini, hata akija kuilipa haiwezi kukubalika maishani mwake.Licha ya kila Muislamu kulazimishwa kufunga, pia hupata malipo mazuri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo ni pamoja na kuyeyuka kwa nyama ya haramu iliyoko mwilini mwa mfungaji, kupata rehema za Mungu na kupewa amali zilizo bora.

Mfungaji huyo pia hatashikwa na kiu siku ya Kiyama, kuondolewa adhabu za kaburi pindi atakapofariki dunia, hupewa karama kubwa siku ya Kiyama pamoja na huepushwa na njaa siku ya Kiyama.Wakati wa Ramadhan inaelezwa ni wakati mzuri zaidi wa kuomba dua na kwa anayeomba akiwa kwenye swaumu, dua yake hukubaliwa kwa haraka.

Hadithi iliyopokelewa na Bukhari na Muslim inasema kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) anasema utakapokuja mwezi wa Ramadhan hufunguliwa mlango wa peponi na hufungwa mlango wa motoni na yanafungwa mashetani hivyo ni kipindi kizuri kwa Waislamu na hasa kufanya toba.

Mwezi wa Ramadhan ndipo kulipoteremshwa Quraan na usiku wa mwezi huo unaelezwa ni bora kuliko miezi 1,000 ambapo malaika huteremka katika usiku kwa amri ya Mola wao kwa kila jambo hivyo wakati huo huwa mzuri kwa ajili ya maombi.

Wakati wa Ramadhan kuna mambo ambayo Muislamu akiyafanya huweza kumfanya apate thawabu kama kuwahi kufuturu, kuchelewa kula daku, kuwafuturisha Waislamu wenzake, kusoma Qur-an na kuzungumza maneno mazuri.

Wanaotoa sadaka za Ibada wakati wa Ramadhan wanapata thawabu gani?
Kwa anayefunga siku moja katika Ramadhan kwa ajili ya Mwenyezi Mungu atamuepusha uso wake na moto umbali wa baina ya mbingu na ardhi na humpa thawabu za mashahidi 300.

Kwa mwenye kuswali rakaa moja katika Mfungo huo, malipo yake ni sawa na mtu aliyesali rakaa 70,000 isiyokuwa Ramadhan na kwa atakayemsalia Mtume rakaa moja ni sawa na kumsalia rakaa 100,000 katika miezi mingine ya kawaida.

Mtu atakayemfuturisha mtu akashiba au wakala pamoja ni kama mtu aliyetoa sadaka ya dhahabu iliyojaa katika ardhi huku kwa atakayempa sadaka mcha Mungu ni kama katoa sadaka vituo vyote vinavyopata mwangaza wa jua.

Mafundisho ya dini yanaeleza kuwa kwa mtu atakayempa nguo moja mtu asiyekuwa na nguo katika mwezi wa Ramadhan basi Mungu atampa mtoaji nguo 70 peponi katika nguo watakazovaa mashahidi. Pia atakayemtembelea Muislamu katika mwezi huu hulipwa thawabu mfano wa mtu aliyemtembelea Nabii Muhammad(S.A.W).

Wafungaji wa mwezi huu wa Ramadhan, wanaelezwa kuwa siku ya Kiyama watakapotoka kwenye makaburi yao watajulikana kwa harufu nzuri kuliko manukato kutoka kwenye vinywa vyao.

Watapelekewa sinia nyingi za vyakula vya aina mbalimbali na wataambiwa na malaika “Kuleni kwani mlikaa na njaa wakati watu walipokuwa na shibe, tena kunyweni kwani mlikuwa na kiu wenzenu walipokuwa roho zao zimeburudika, pumzikeni kwani mlikuwa katika taabu na hali watu walikuwa ndani ya starehe”.




Ni hayo tu kwa leo ndugu wadau kama unayasikia na huyatilie maananii 

No comments: