Na
Bishop Dankton Rudovick Rweikila
15th
January 2018
Jana tuliangalia sababu ya mtu
kuapa na leo tunaendelea na sababu ya pili ambayo ni KUMRIDHISHA MTU KWAAJILI YA UAMINIFU (KIAPO CHA KUKOMESHA UBISHI)
Hii ni moja ya sababu ambayo watu
wengi wanaapa kwaajili ya kumridhisha mtu. Wengi sana wamewaapia watu kwa
mtindo huu. Kwa mfano unaweza kuwa umekopa pesa kwa mtu au kumuazima kwa
minajili ya kumrudishia fedha na unamuapia yule mtu kwamba ikifika siku Fulani
mimi nitakuwa nimekurejeshea. Wengine wanaapa kabisa kama nakudanganya nife au
mali zangu zipotee, watoto wangu wafe, ardhi inimeze. Sasa mtu anaapa kwasababu
ya kumridhisha yule anayemnenea na anaapa kumbe sivyo alivyo sawa sawa na kiapo
chake.
Mwanzo 25:29-33 29 Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja
kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. 30 Esau akamwambia Yakobo,
Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo
walimwita jina lake Edomu. 31 Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo
haki yako ya mzaliwa wa kwanza. 32 Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu
kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? 33 Yakobo akamwambia, Uniapie
kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
Wakati Esau anaapa alijua ndani
ya moyo wake kwamba Yakobo hawezi kuwa mkubwa kwake hivyo kwasababu ya chakula
aliamua kudharahu haki yake ya uzaliwa wa kwanza kupitia kiapo. Kuna wengi sana
wamedharau haki za watoto wao utasikia mtu akisema BORA NISINGEZAA. Wengine
wameapa kabisa juu ya fedha zinazopita kwenye mikono yao. Mtu anasema kazi hii
aina msaada kwangu wala ainisaidii chochote ghafla unashangaa fedha yako
inaanza kukosa kazi kwasababu ya laana uliyojiapia. Haya yanapotokea inakuwa
mateso kwetu.
Esau alipouza haki yake ya
uzaliwa wa kwanza wakati wa kubarikiwa ulipofika alibarikiwa Yakobo, na Esau
akatamani kumuua ndugu yake. Kuna mambo yamenatokea leo kwasababu ya viapo
ulivyokula kwa kinywa chako mwenyewe. Ujawahi kusikia tu akisema mimi naweza
kuishi maisha yeyote mtu anadharau kile alichonacho na kutaka kuishi maisha
yoyote, SIYO MAISHA YA USHINDI YEYOTE.
Shika moyo wako tuombe….
Sema Bwana Yesu ninaomba
unisamehe yale yote niliyotamka kwa kinywa changu na yaliyotoka ndani ya kinywa
changu, niliyoapa leo naomba unisamehe kwa kiapo hicho kwa jina la Yesu kwa
damu ya Yesu. Bwana Yesu ninaomba Damu yako ifute kile kiapo nilichoapa kwa
nafsi yangu kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu Amen.
Sikiliza nikuambie alichokifanya
Esau badala ya kukumbuka alipokosea alipandwa na hasira. Wengi tunapokosea
uchungu unajaa ndani ya miyoyo yetu na kutaka kuongeza uovu Zaidi. Esau
alilaani maisha yake mwenyewe na badala ya kukimbilia toba aliingiwa na uchungu
ndani yake na kutaka kuongeza kosa Zaidi ndani yake kwa kutaka kumuua ndugu yake.
Unalaani maisha yako mwenyewe na unapowaona waliofanikiwa wivu unaingia ndani
yako na kutaka kuchukia wengine.
Na tunapoendelea na somo hili
ninatamani kila mtu aandike kile ambacho unaapa mara kwa mara kwasababu hiyo ni
roho ya kulaani maish yako. Kuna wengi sana bila kuapa hauoni Raha hiyo ni
roho. Unajikuta kila unapo ambiwa ukweli unakataa hata kama hauna madhara kwako
unajikuta unakataa ukweli tu, na unaapa kabisa. Biblia inasema NDIYO yako iwe
NDIYO na HAPANA iwe HAPANA. Roho hii uwa inazalisha ubishi na mashindano na mtu
anafikia hatua anaona apendwi kwasababu ya mashindano hayo na kwasababu ya
kutokupenda ukweli Mungu akikuweka kwa watu wenye kusema kweli utakataliwa
kwasababu ya ukweli wao. Kutembea kwenye ukweli ni Neema. Na mimi naomba Mungu akupe
Neema hiyo kwa jina la Yesu. KWELI ITAKUWEKA HURU KWA JINA LA YESU.
Muulize jirani yako unatembea
kwenye kweli? Anakubali udhahifu wako?
Madhara ya kutokukubali ukweli
hauwezi kutambua kosa lako. Mungu akupe Neema ya toba kwa jina la Yesu. Kuna
wakati mwingine ndani ya moyo wako unasikia kabisa ninachosema ni uongo kwa
hiyo unajikuta unatubu moyoni lakini kinywa akikiri, ukiulizwa unakataa kabisa.
Maandiko yanasema Mithali 6:2 Basi
umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, ` Umekamatwa
kwa maneno ya kinywa chako, Na uzima wa mtu humo ndani ya kinywa
chake.
Dhambi hii hiko sana ndani ya
walokole wengi na kutengeneza si rahisi sana, Shetani awezi kukuacha upone.
Miyoyo mengi imejaa manunguniko
na malalamiko na hayo yametokana na kutokuwa na moyo wa toba. Ndiyo maana
unakuta mtu anacheka na wewe lakini ndani anasaga meno nah ii inatokana na
kutokukiri makossa. Maandiko yanaongelea kwa habari ya Kaini na Habili na
walitoa sadaka wote wawili lakini Mungu akaitakabali sadaka ya Habili na ndugu
yake akajaa uchungu ndani ya moyo wake na mwisho akamuua nduguye.
Moyo huu unazuia mafanikio yako,
mafanikio yanatokana na watu hivyo ndani mwako ukishaaza kuzalisha ubaya
unafikia kufukuza watu. Biblia inasema ataleta mataifa kwako wakupe utajiri,
sasa ukishakuwa na moyo wa kufukuza watu utafukuza utajiri wako. Hauwezi kuwa
na moyo wa kupokea watu kwasababu ya mabaya uliyoyajaza ndani ya moyo wako,
ndiyo maana maandiko yanasema LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO
(Mithali 4:23). Ndiyo maana Biblia
inaongelea kwa habari ya mtu kusamehee saba mara sabini ili uweze kuishi na
watu.
Maandiko yanasema katika amri
kumi iliyokuu Zaidi ni upendo, kwasababu upendo ndiyo unajenga mahusiano na
watu wengine. Ndiyo maana Paulo aliandika haya hata kama unene kwa lugha uwe na
Imani ya kuamisha milima kama auna upendo si kitu (1Wakorintho 13:1..). Kama
ukiwa hauna upendo ni sawa na mtu anayeishi kwenye chumba kilichofungwa. Mungu
ana haja ya kufungua malango yako kama hakuna wakupita kwenye malango hayo.
Maandiko yanasema hivi “name nitalegeza viuno vya wafalme; ili
kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa” (Isaya 45:1-3).
Mungu ana haja ya kufungua malango ambayo hakuna atakayeingia.
Mwangalie jirani yako mwambie
NAKUPENDA KWA JINA LA YESU….
Wakati Adamu ameumbwa alikuwa
tajiri na kila kitu lakini alikuwa mpweke, mpaka alipopewa msaidizi. Ukifunga
mlango wa upendo, Malango ya utajiri yasahau, Malango ya Amani yasahau.
Kwasababu (source) chanzo cha yote ni upendo na bila upendo hakuna kitu ambacho
kitafanyika kati ya mtu na mtu.
Kataa neno la kunena kwamba watu
wa nini kwenye maisha yako. Na Mungu akuletee watu waaminifu kwa jina la Yesu.
KIPIMO CHA UTAJIRI KWENYE MAISHA YAKO NI PALE UNAPOANZA KUDHAMINI KILA
MTU MAISHA YAKE, KAZI YAKE. NA DALILI YA KUSHUKA NA KUPOTEA NI PALE UNAPOANZA
KUDHARAU KILA MTU KWENYE MAISHA YAKO. Na mimi nakuambia fanya uchunguzi
wako (Homework) utaona wengi waliodharau watu na kuwapenza wanakuwaje.
Kuna wengine wanadhani kumpenda
mtu hauwezi kumkema, sikiliza nikuambie ukali ambao tulipitia kwa wazazi wetu
si kwamba walikuwa hawatupendi bali walitupenda sana na ukali wao umetufanya
tuwe watu bora kwenye maisha yetu. Kuna wengine bila kukemewa sana na kusema
wanaweza wakapotea na ukipata nafasi ya kukemea jua kwamba kuna kusudi zuri juu
yako ili ufike mahali. Ukiona unakemewa sana maana yake jicho la Bwana liko juu
yako.
Kingezo kingine cha mafanikio ni
kuonekana, inawezekana huko kwenye familia lakini hauonekani, na ukionekana
ujue yote utaambiwa yawe ni mabaya au mazuri utaambiwa. Kuna watu ambao
wakifika mahali lazima wataonekana. Kuna watu ambao ndani ya familia kila
likitokea jambo lazima wakushirikishe hiyo ni ishara mojawapo ya kuonekana.
Kuna watu wamejilaani pasipokujau
kwamna wamejilaani anapokuwa anaonekana na kuitwa kila mahali anaanza kusema
kwanini mimi? Na unazuia milango yako ya kuonekana.
Mungu anapotaka kumuokoa mtu lazima
ainue mtu kwaajili ya maisha yako. Wakati wa Agano la kale Mungu alimuinua Esta
akaenda mbele ya mfalme kwaajili ya Wayahudi. Na leo Mungu ameinua Power of God
Fire Church kwaajili yako. Haijalishi wakina Hamani wako lakini Bwana ametuinua
kwaajili ya kazi yako, ndoa yako, shamba lako, n.k.
Tuombe.
Eee Bwana Yesu naomba nipe Neema
ya kujitambua kuwa mimi ni nani na niko kwaajili gani kwa jina la Yesu, wewe
shetani uliyenifunga na kunichelewesha ninakataa kwa jina la Yesu haya si
maisha yangu ninakataa kwa jina la Yesu kuanzia leo nakataa kila roho ya kiburi
unayoshindana na uzima wangu kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu. Ninakataa Roho
ya kiburi toka ndani yangu, roho ya kiburi inayojiunua ndani yangu kwa jina la
Yesu. Roho ya kiburi cha uzima ninakataa kwa jina la Yesu.
Kausha kila shina la kiburi ndani
yako kwa damu ya mwana kondoo. Endelea kuomba kukataa Roho ya kiburi kwenye
maisha yako…..
Kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu
ninafuta kila laana ya kukataa haki yangu, siku ya leo ninatengua kila kiapo
cha kinywa changu kwa jina la Yesu. Enyi Majini mlionishati maisha yangu
kwaajili ya kiapo hicho nilichoapa nikakataa ukweli wakati nilitenda uovu leo
ninakiri Bwana Yesu nisamehe leo ninakiri yote Yesu, niliogopa wanadamu Yesu
lakini leo ninakiri kwa kinywa changu Baba yangu, ni kweli Bwana nilitenda
dhambi ya uongo, nilichonganisha Baba nisamehe, nilisema watumishi wako Baba
nisamehe. ………
Anza sasa kutengua kila viapo
ulivyoapa kwa uongo kwa Damu ya Yesu Kristo tumia damu ya Yesu Kristo (Ufunuo
12:11). Piga kila kiapo ulichokinena kwa uoga mbele za watu piga kila kiapo
unchokikumbuka na usichokimbuka. Hayo maneno uliyoyanena kama ni ya haki kumbe
ni uongo piga viapo hivyo kwa Damu ya Yesu, hivyo viapo vilivyongangania uchumi
wako, ndoa yako na maisha yako kwa ujumla.
Ninakamata kila Roho ya chuki na
mashindano katika jina la Yesu, kila Roho ya mashindano leo ninashindana na
wewe kwa jina la Yesu Kristo. Kila Roho ya mashindano iliyoshikilia nafsi yangu
leo ninaipiga kwa jina la Yesu. Umeshikilia amani yangu na kuleta uchungu ewe
roho ya chuki toka achia nafsi yangu. Ninapiga kila mapepo ya uchungu ndani
yangu kwa jina la Yesu. Ninapokea Roho
ya Amani, Furaha, Upendo kwa jina la Yesu Kristo.
Ninafuta kila hati ya mashitaka
iliyoandikwa niliponena kwa maneno ya kinywa changu kwa Damu ya Yesu, hayo
maneno niliyojitamkia juu ya uchumi wangu kuwa vyuma vimekaza ninayakataa kwa
jina la Yesu Kristo. Leo ninafuta kila hati ya mashitaka kwa jina la Yesu
Kristo. Ninafuta kila maneno machafu
ambayo shetani anayatumia kuninasa hili nirudi nyuma kwa damu ya Yesu,
Imeandikwa kwenye Wakolosai 2:14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena,
akaigongomea msalabani; Ninafuta hiyo hati ya mashitaka kwa damu ya Yesu.
Endelea kuomba kwa mzigo mpaka uone jambo kwenye ulimwengu wa Roho na
ukimaliza ita nguvu ya Roho Mtakatifu kisha mwaga Damu ya Yesu Kristo utaona
namna ambavyo unapokea nguvu isiyo yakawaida.
Mungu akubariki tukutane siku ya
kesho kwenye mkesho wa Jumanne.
Bishop Dankton
Rudovick Rweikila
Power of God Fire
Church
Chanika Buyuni
Simu +255 753 230 680 +255 717 538 499
Youtubu Chanel
https://youtu.be/mJSqGrFBd4 inc
Facebook link. Power
of God Fire Church https://www.facebook.com/Power-of-God-Fire-Church-965783380111414/
Or
Bishop Dankton Rudovick Rwekila
No comments:
Post a Comment