Na
Bishop Dankton Rudovick Rweikila
14th
January 2018
Ukifuta kiapo bila ya kufuta
sababu zinazosababisha mtu kuapa utakuwa umefanya kazi bure na sisi hatutaki
kufanya kazi bure kwa jina la Yesu.
Mithali 6: 2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa
kwa maneno ya kinywa chako,
Leo tunakwenda kijitenga na
maneno ya vinywa vyetu kwa jina la Yesu
Sasa sababu zipo nyingi sana
ambazo zinaweza kumsababisha mtu kula kiapo na leo tutakwenda kutembelea jambo
moja ambalo ni WIVU.
1. WIVU
Wako watu wengi wamejaa wivu na
wamepanga kupangua mawazo yako hata kama yanamanufaa kwako lakini kwasababu ya
wivu wanataka kufanya mabaya juu yako.
Matendo ya Mitume 13:45-47 45 Bali
Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa
na Paulo, wakibisha na kutukana. 46 Paulo na Barnaba wakanena kwa
ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa
kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa
milele, angalieni, twawageukia Mataifa. 47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa
na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa
dunia.
Wayahudi walijaa wivu na wakawa
wanapingana na maneno waliokuwa wanayatoa. Kuna watu ni lazima wawe matajiri pinga
unavyoweza lazima wawe na mafanikio. Hata kama watazuia miaka mingapi lakini
nilazima uwe na mafanikio. Waliokutegea mitengo ila hauwezi kuangamia ni lazima
utapita katikati yao. Kwenye mabaya waliokuandalia yupo Mungu ambaye
atakuinulia watetezi wako na utapita katikati yao. Wana wa Israeli ilikuwa
nilazima watoke kwenye utumwa. Farao aliwazuia lakini kwasababu ilikuwa ni
lazima watoke Mungu aliachilia mapigo na wakaachiliwa. Wapende wasipende lazima
waachie mwaka wako huu ni mwaka wako wa UREJESHO.
Usikosee njia yako ni lazima
upite na kutokea upande wa pili wa mafanikio ya maisha yako. Kuna watu
wanajiona nafsi zao kama vile hawastahili. Kama watu hawa ambao Paulo alikuwa
anawahubiria waliona kama hawastahili vile walikuwa wanapewa. Kuna watu wanaona
hawakustahili hata kuolewa, kuna wengi wameolewa na wanaona kama hawakustahili
kuolewa na wale ambao hawako kwenye ndoa wao ndiyo wanaona walistahili kuolewa.
Na ndiyo maana kinywa chako kwenye ndoa yako kiko kinyume na ndoa yako. Huko kwenye
ndoa na unaona kabisa hakustahili kuolewa. Kuna watu wanabiashara lakini
wanajiona kama hawakustahili kuwa na biashara hiyo.
Kuna wengine wanaona kwamba
hawakustahili kuzaliwa Tanzania na ndiyo maana wananungunika kuwepo. Wewe
ambaye unaona ulistahili kuwepo unatafuta njia ya kupita kwasbabu unajua
unastahili.
Muulize jirani yako ulistahili
kuwepo kwenye Ibada leo?
Biblia inasema siyo wewe
uliyenichagua bali mimi ndiye niliyekuchagua. Kwa hiyo siyo wewe uliyejialika
kwenye Ibada bali Bwana ndiye amekuchagua uwepo kwa neema yake. (Yohana 15:16). Na ndiyo maana
unapokuja kwenye ibada kila mtu analo fungu lake. Uliwahi kuona mtu anaalikwa
kama mgeni rasmi kwenye sherehe na akakosa chakula si raisi kabisa. Kwa hiyo
ukiona mwingine anakula hauogopi kwasababu wewe siyo mzamiaji, jua zamu yako
imekaribia. Hivyo basi unapoona mwingine kafikiwa jua zamu yako imefika una
haja ya kupindua pindua bufee andaa tumbo lako. Uzima wako ulistahili kuwepo,
watoto, kazi na vingine vingi ulivyonavyo na vinavyokuja vilistahili kuwepo
kwako.
Biblia inasema utakula kwa jasho na
wala si kwa mateso, na tena Biblia inasema utazaa kwa uchungu si kwa mateso.
Kwa hiyo unaweza kuwa kwenye kinakilishi (Computer) na jasho likatoka tu
kumbuka hilo, SIYO KILA ANAYETUMIA NGUVU ANATAJIRIKA. Si unakumbuka kila mahali
Yusufu alikpokuwa anapita alikuwa na nafasi ya utawala. Alipokuwa gerezani
alikuwa na nafasi ya kutawala kama msimamizi, na alipokwenda kwa Potifa alikuwa
msimamizi juu ya nyumba yake.
Kuna watu ambao walipeleka mawazo
yao kwenye maofisi na makampuni walipokataliwa na wao wakajikataa. Sikia neno
la Bwana wakikukataa kampuni hii geukia nyingine, Paulo walipomkataa aliwaambia
“Ilikuwa
lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali,
na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia
Mataifa.” Kwa hiyo mwaka huu ulichonacho lazima kitokee kwa jina la
Yesu. Una mawazo mazuri ya umoja lakini wengine hawataki wewe songa mbele na
wale waliokubali na Mungu atakuacha kwa jina la Yesu.
Usigeukie upande wa pili
kwasababu ya wivu au ubaya, bali geuka kwasababu ya Bwana
Tunenda kuomba maombi ya kufuta
roho za wivu na Roho ya kujikataa. Sasa ubaya au wivu unaweza kuwa ndani yako
au ndani ya jirani yako hivyo leo unajipiga kwanza wewe unakaa sawa ndipo
unapokwenda kwa jirani yako.
Yohana 11:1-4, 40- 1 Basi
mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na
Martha, dada yake.2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta
miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. 3 Basi
wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. 4 Naye
Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu
wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.
Yesu aliapisha magonjwa na kusema
ugonjwa alionao lazaro si wa mauti bali kwaajili ya utukufu wa Mungu. Ni sawa
na wewe kuitamkia biashara yako “wewe biashara umeleta hasara lakini hasara
hii si ya mauti”. Kwa hiyo wakati Yesu anamfufua Lazaro alikuwa
anatenda kwaajili ya utukufu wa Mungu.
Ukisoma Mstari wa nne na Tano
utaona namna ambavyo Yesu anaongelea kwa habari ya ugonjwa wa Lazaro. Kwenye
Mstari wa 40 utaona namna ambavyo Yesu alisema “Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini
utauona utukufu wa Mungu?” Kwa hiyo Yesu alijua kuwa atafufuka kwaajili
ya utukufu wa Mungu. Usiangalie ugumu ulionao kwenye maisha yako bali angalia
utukufu wa Mungu. Usiangalie migogoro kwenye ndoa yako angalai utukufu wa
Mungu.
Yesu alilia kwa sauti kuu
kwaajili ya kudai haki yake kwasababu alijua Baba anamsikia.
Ingia kwenye maombi kwaajili ya
kupiga kila wenye wivu….. Omba mpaka usikie kitu kwenye ulimwengu wa Roho.
Mungu akubariki tuonane Jumatatu
saa kumi kwenye maombi ya siku 21 ili tuendelee KUREJESHA KWA JINA LA YESU.
Bishop Dankton Rudovick Rweikila
Power of God Fire Church.
Simu: + 255 753 230 680 + 255 717
538 499
No comments:
Post a Comment