KIAPO CHA UJINGA
Na
Bishop Dankton Rudovick Rweikila
16th
January 2018
Hichi ni kiapo ambacho mtu anaapa
kwa ujinga na inatokana na kumzoea mtu Fulani au mazoea ya kupitila kwenye
familia hivyo inatokea mtu kuapa. Leo tunakwenda kushugulika na aina hiyo ya
kiapo kwa jina la Yesu.
Muhubiri 5:2-3 1 Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa
Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu;
Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya. 2 Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa
chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu
yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache. 3 Kwa
maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia
ya wingi wa maneno.
Maandiko yanatambua kwamba kuna
maneno ya ujinga na maandiko yanasema usiseme maneno ya ujinga. Unaweza kuona
ni neno la aibu kusema maneno ya ujinga lakini yana madhara makubwa kwenye
maisha yako. Na maneno ya ujinga unanena kwa kinywa chako.
Kuna mambo mawili yanafanyika
kwenye maisha yetu kuna maneno ya ujinga lakini kuna kutembea kwenye ujinga au
kuishi na watu wenye ujinga. Kuna mwingine ana ujinga lakini anaishi na watu
wanaonena ujinga.
Maombi
Ninakataa maneno yote niliyonena
kwa ujinga kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu na kwa Damu ya Yesu.
Maneno ya ujinga mara nyingine
mtu anaweza kuyasema wakati amekasirika yanaweza kusemwa na mume kwa mke au mke
kwa mume. Kwa mfano utakuta mtu akimuita mke wake paka, mbwa na majina kama
hayo. Hayo ni maneno ya ujinga kwasababu hauwezi kulala na mbwa hivyo hayo ni
maneno ya ujinga.
Moyo wako usiwe na haraka kunena
maneno mbele za Bwana, unakuta mtu anatamka wiki hii nitaomba wiki nzima na
unakuta hautekelezi lile ambalo unalisema mbele za Bwana. Wengi wanakuwa wepesi
kunena maneno haya ya ujinga kwasababu ya kutaka kuonekana. Ni muhimu kuelewa
kila neno unalosema mbele za Bwana Mungu analihesabu na kulidai kwako na kama
Mungu atalihesabu kumbuka jambo moja yupo mshitaki wetu ibilisi na utashangaa
wakati unadai haki yako anaibua hoja kwasababu ya maneno ya ujinga uliyoyatamka. (Ufunuo 12:10, 1Petro 5:8)
Ninakuomba mwaka huu usiwe mtu wa
kusema maneno uwe mtu wa maneno machache na mwingi wa kutenda, mwaka huu ni
mzuri shetani apende hasipendi huu ni mwaka mzuri. Na uwe ni mwaka wako wa
mafanikio na kibali mbele za Bwana kwa jina la Yesu na Mungu akufanikishe kwa
jina la YESU. Muombe Mungu usikae na watu ambao wanaujinga au wana mawazo ya
ujinga. USIKUBALI UJINGA KWAJINA LA YESU.
Mungu anataka uwe na maneno machache
ili unapopata ndoto iwe ni ndoto ya Mungu yenye kukufanikisha siyo ndoto ya
uchovu ambao unatokana na maneno ya ujinga uliyoyaongea kutwa zima.
Maombi
Ninakataa kila ndoto ya uchovu
niliyoota kwa jina la Yesu. Kila ndoto ya uharibifu iliyotokana na uchovu
ninaikataa kwa jina la Yesu. Ewe ndoto ya uchovu iliyoleta mafarakano kwenye
ndoa, kanisa nakataa kwa jina la Yesu. Leo ninakataa pepo la ujinga ninajitenga
na uchawi wa ujinga ndani yangu unaopita kwenye ndoto kwa Damu ya Mwana Kondoo.
Ninafuta kila ndoto ya uchovu niliyoota kwaajili ya ujinga kwa jina la Yesu.
Ndoto zinazotokana na uchovu wa
namna hii zinaleta sana mafarakano baina ya mtu na mtu. Mungu akupe neema ya
kukataa ujinga ndani ya maisha yako kwa jina la Yesu.
Sauti ya mpumbavu inatokana na
wengi wa maneno. Maandiko ndiyo yanasema hivyo sasa nataka ujue jambo moja kila
neno linalotoka kwenye kinywa chako alipotei Bure. Unaweza usione madhara leo
lakini baadae utashangaa kuona madhara ya maneno hayo katika safari ya maisha
yako. Unaweza kusema neno leo na shetani anahifadhi linaweza kutokea mwaka
ujao, kwa watoto wako au kwa wajukuu wako. Kumbuka neno unalolitoa kwenye
kinywa chako ni mbegu ambayo umeipanda na leo ninataka kuifuta hiyo hati kwa
jina la Yesu.
Kutoka 20:7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako,
maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
Unaweza kutamka maneno kumbe
Mungu anakuhesabia una hatia kwasabababu ya kutaja jina la Mungu wako bure.
Kwenye maneno ya ujinga wengi wanalitaja jina Bwana bure. Kwani ujawahi kuona
mtu anaapa uongo au kwa ujinga wake anatumia jina la Mungu.
Tuangalie wanaotembea kwenye ujinga
2 Samweli 15:11 11 Na watu mia mbili walioalikwa
wakatoka Yerusalemu pamoja na Absalomu, wakaenda katika ujinga wao wasijue neno
lo lote.
Absalomu anatalka kufanya uasi
kwa Daudi na amekusanya watu mia mbili wanaokwenda kwa ujinga wao bila kujua
neno lolote ambalo amelitenda Daudi. Usikubali mtu hauteke moyo wako na aujaze
ujinga kuna watu ambao miyoyo yao imeibiwa na kujazwa ujinga. Wengi wanajazwa
ujinga huu na wakati mwingine wanapoteza uaminifu wao, upendo wao na hata utu
wao kwasababu ya kujazwa ujinga.
Maombi
Kwa jina la Yesu kwa Damu ya Yesu
ninakataa kila ujinga walioujaza moyo wangu kwa jina la Yesu na Kwa Damu ya
Yesu.
Ujinga huu ukiingia kwenye kanisa
ni hatari sana kwa kanisa hata kwa upendo bayana ya ndugu na ndugu kwasababu ya
ujinga huu. Ni hatari kuambiwa mtu huyu hakupendi wakati anakupenda na
kwasababu ya kusikia maneno ya ujinga unajikuta ukimchukia mtu bila sababu.
Unaweza kumpiga rafiki yako
kwenye maombi kwasababu ya wewe kusikiliza maneno mabaya ya ujinga wa mtu. Kwa
hiyo unajikuta unajipiga wewe mwenyewe katika maombi ya namna hiyo, unapotuma
neno kama halina pakutua linakurudia wewe na ni hatari kwako. Haya yametokea
kwenye familia, kwenye ndoa, kwenye makampuni n.k. Jana nilisema jambo moja
kubwa sana ukisha jaza ubaya juu ya watu ndani ya moyo wako umefukuza utajiri
wako.
Wengi wetu hatujui namna ambavyo
shetani anatuteka, shetani akiruhusu moyo wako kuwaza mazuri umefanikiwa na
akiujaza moyo wako mabaya hautafanikiwa. Mungu anahitaji kupita kwa mtu ili
mafanikio yako yatokee. Kwa hiyo Mungu anakujengea mahusiano na watu ili uweze
kufanikiwa, hivyo basi mahusiano yakiondoka hauna namna ya wewe kuweza
kufanikiwa. Wengi ambao wako kwenye umasiki wametekwa na kufungiwa kwenye
chumba ambacho kinawanyima mahusiano na watu. Wengi Roho hii wanaita Roho ya
kukataliwa. Sikia nikuambie Roho hii inaanza kwako wewe binafsi kwa kukataa
watu, ukikataa watu na watu nao wanakukataa wewe pia. NI MAOMBO YANGU LEO MUNGU
AKUPE MILANGO YA MAHUSIANO.
Mpigie Bwana Yesu mnakofi mengi
mengi…..
Wengi tunaomba utajiri bila kujua
milango inayoleta utajiri ni ipi. Sikiliza jiulize una marafiki wangapi
unaowapenda na unaowaamini, hiyo ndiyo milango yako ya utajiri. Yesu anasema
mpende jirani yako kama nafsi yako kwa hiyo kipimo cha upendo ni namna
unavyoipenda nafsi yako. Unapompenda mtu hautamtamkia maneno ya ujinga bali
maneno ya hekina na Busara. (Yakobo 2:8,
Warumi 13:9, Luka 10:27)
Kwa wale wanandoa naomba mshike
hili, Unaweza kuishi na mtu ambaye haumpendi kweli? Ilo najua kabisa haliwezekani
kama unamchukia mwenzako utamtamkia mabaya na kamwe hamuwezi kufanikiwa.
Maandiko yanasema apataye mke anapata kitu chema na anajipatia kibali kwa
Bwana. Maana ya kibali ni ili uweze kufanikiwa katika hatua za maisha yenu. (Mithali 18:22). Kama unamchukia mke
wako je unatafuta fedha kwaajili ya nani, ni kwaajili yako na Familia yako na
kama ukipanda wote mnapanda. Ukifanikiwa na yeye anafanikiwa hivyo una sababu
ya kuomba mabaya kwa ujinga wako kwa jina la Yesu
Kile ambacho unatakiwa kuombea
usiku na mchana ni mahusiano, hata mbinguni hautaenda bila kuwa na mahusiano
mazuri. Na sisi ni jeshi moja hivyo hatuna sababu ya kupigana na kudhuriana kwa
jina la Yesu. Ndiyo maana jeshi linawatu wachache kuliko raia lakini jeshi
linawamudu raia na sisi ni jeshi la Bwana na tunashinda wapepo kwa jina la
Yesu. Ndiyo maana Yakobo anayasema haya kwamba mashindano/mapigano yanatoka
wapi? (Yakobo 4:1)
Wewe ni jeshi la Bwana hivyo
hakikisha una mahusiano mazuri sana na wengine.
Mungu akubariki sana na
tunakukaribisha katika maombi haya ya siku Ishirini na Moja na utamuona Mungu
katika viwango vingine. Tuonane kesho saa kumi kwaajili ya maombi. Na kwa
mafundisho mengine Zaidi unaweza kuangalia kwenye chanel yetu ya Youtubu,
Facebook na Blog yetu.
Bishop Dankton
Rudovick Rweikila
Power of God Fire Church
Chanika Buyuni
Simu +255 753 230 680 +255 717 538 499
Youtubu Chanel
https://youtu.be/mJSqGrFBd4 inc
Facebook link. Power
of God Fire Church https://www.facebook.com/Power-of-God-Fire-Church-965783380111414/
Or
Bishop Dankton Rudovick Rwekila
No comments:
Post a Comment