MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, January 23, 2018

KUFUNGA MALANGO YA KUZIMU NA KUHARIBU JESHI LA KUZIMU SEHEMU YA NNE



Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

23TH January 2018

Zaburi 116-3-5 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. 

Zipo shida ambazo zinawapata watu kitoka kuzimu. Kuzimu inaweza kuandaa shida juu ya mtu au changamoto juu ya mtu na ikampata. Siyo kila shida unayoipitia ni kwamba ni mpango wa Mungu au ni jaribu la Mtu. Jana nilisema vyote vinaweza kupotea lakini Imani yako haitapotea, na nilisema vile vile kwamba hivi vyote unavyoviona haviko ndani ya uweza wako lakini Imani yako iko ndani ya uweza wako. Tuliona namna ambavyo Ayubu alijaribiwa na kuteswa lakini aliilinda Imani yake. Na kama Imani yako haitapotea maana yake vyote ulivyopoteza vitarejea kwasababu ya Imani yako.

Imani iko ndani ya uweza wako. Ndiyo maana Stephano anapigwa mawe lakini Imani yake haikuguswa, Petro amewekwa gerezani lakini Imani yale haikuguswa. Danieli amewekwa kwenye tundu la simba lakini Imani yake haikuguswa, hata wewe Imani yako haitaguswa kwa jina la Yesu.

Mungu ni wa pekee na usijaribu kumlinganisha na wewe kukosa fedha au jaribu unalopitia. Ukishafika mahali kumuona Mungu ni wa pekee ndani ya changamoto yako utamuona Mungu. Haijalishi umelala njaa au umetembea kwa miguu au umekataliwa Mungu ni wa pekee. Ndipo Shedraki na wenzake wakasema hakika Mfalme hatutakusujudia hata kama Mungu wetu hatatuokoa kwenye moto huu lakini hatutakusujudia kwasababu Mungu wetu ni wapekee.

Mwambie jirani yako Mungu ni wa pekee.

Ninajua kweli unapitia hali ngumu lakini Mungu wako ni wapekee. Nilazima umuambie shetani yote unaweza kigusa lakini Imani yangu hauwezi kuigusa, haijalishi utaleta changamoto gani kwangu Imani yangu hautaigusa. Ndipo Paulo anasema Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Warumi 8:35. Mungu wako ni wapekee hakuna cha kukutenga naye.


Bishop Dankton Rudovick Rweikila
Power of God Fire Church
Chanika Buyuni
P.o.Box 11920
Simu +255   753 230 680 +255 717 538 499
Youtubu Chanel https://youtu.be/mJSqGrFBd4 inc
Or
Bishop Dankton Rudovick Rwekila


No comments: