MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Monday, November 11, 2013

Waebrania 12:14-29 (Neno: Bibilia Takatifu)

Waebrania 12:14-29

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na utaka tifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana. 15 Angalieni sana mtu ye yote asishindwe kupata neema ya Mungu, na muwe waangalifu pasizuke chuki ambayo, kama mmea wenye sumu, inaweza kukua ikaleta matatizo na kuwachafua wengi. 16 Hakik isheni kwamba miongoni mwenu hamna mwasherati au mtu asiyemcha Mungu. Kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja, aliuza haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza. 17 Maana mnafahamu ya kwamba baadaye, alipotaka kurithi ile baraka aliyokuwa apewe, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.
18 Hamkuja kukaribia mlima ambao unaweza kuguswa, na ambao unawaka moto; wala hamkuja kwenye giza, huzuni na dhoruba, 19 na mlio wa tarumbeta na sauti ikisema maneno kwa kiasi ambacho wale walioisikia waliomba wasiambiwe neno lingine zaidi. 20 Kwa maana hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: “Kama hata mnyama atag usa mlima huu, atapigwa mawe.” 21 Kwa hakika waliyoona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.” 22 Lakini ninyi mmekuja kwenye Mlima wa Sioni, na kwenye mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni, ambapo wamekusanyika kwa shangwe maelfu na maelfu ya malaika. 23 Mmefika kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu ambao majina yao yameandikwa mbin guni. Mmekuja mbele ya Mungu, hakimu wa watu wote, na mbele ya roho za watu wenye haki, waliofanywa wakamilifu. 24 Mmefika kwa Yesu, msuluhishi wa agano jipya, na kwa damu ile iliyonyunyizwa, inenayo maneno mema kuliko damu ya Abeli.
25 Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa hawa kuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi tutaepukaje tukimkataa yeye anayetuonya kutoka mbinguni? 26 Wakati ule sauti yake ilitetemesha dunia, lakini sasa ameahidi, “Kwa mara moja tena nitatetemesha si nchi tu bali na mbingu pia.”
27 Maneno haya, “Kwa mara moja tena,” yanaonyesha kwamba vile vinavyotetemeshwa vitaondolewa, yaani vyote vilivyoumbwa, kusudi vibaki vile tu visivyoweza kutetemeshwa.
28 Kwa hiyo, tuwe na shukrani kwa kuwa tumepokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna itakay ompendeza, kwa unyenyekevu na kicho; 29 maana Mungu wetu ni moto unaoteketeza.

No comments: