MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, December 25, 2013

SALAMU ZA CHRISTMASS LEMA

Ni fursa ya kipekee Mungu ametupa leo kuona siku ya leo ambayo mwana wake wa pekee alizaliwa katika hii dunia , tangia majuzi nimekaa nikiwa nawaza sana ni sms gani naweza kutuma kwa watu nimereceive sms nyingi mno kutoka kwa watu mbali mbali wakubwa kwa wadogo wafanyakazi wenzangu na makampuni mbali mbali , lakini katika hayo yote nimekuwa na mwaswali mengi vile vile , je ni kweli watu wanajua maana ya christmass hama tunasafiri na kula vyakula vya aina mbali mbali , kutanda kwenye maukumbi ya starehe mmh , maana ndiyo wakati dhambi zinaongezeka zaidi na vitu kupanda bei mavazi nk mmh lazma tuweze kujua maana halisi ya christmass ndani ya miyoyo yetu na miili yetu . Yesu huyu aliyezaliwa katika hali ya mwili na mimba yake iliyokuwa katika hali ya roho ,





sijui kama unanielewa sawa sawa hapo , aliletwa kwetu kwaajili ya baraka za kila mtu , katika hali isiyo kuwa ya kawaida Mariam alichukua mimba kwa njia ya roho mtakatifu , kumaanisha kwamba Mungu mwenyewe alishuka kutubariki na kutukomboa natamani ningekuw na Lunga nyepesi ya kukueleza tambua kwamba wazee wetu wa baraka walizaliwa na wanadamu na hapo zamani kabla ya Yesu baraka zilikuwa nizakuachiana kama urithi vile , Mhh Ibrahimu kwa Isaka , Isaka kwa Yakobo na kuendelea vizazi na vizazi hila Yesu sasa aliyezaliwa katika hali ya utakatifu , yaani Emmanuel Mungu pamoja nasi alikuja kukaa na sisi sote na baraka zake ni za vizazi na vizazi Sina mengi ya kusema ila najua utakuwa umepata salamu za Kristmass ni wakati wa kufungua miyoyo yetu na kumkaribisha Yesu maishani mwetu



Nawapenda sana na Mungu awabariki sana

No comments: