Msingi
katika kanisa lolote la Mungu wa kweli ni neno la MUNGU, kila kanisa la kweli
lazima lianze na msingi wa neno la Mungu na siyo hisia au mapokeo ya binadamu
(Mafundisho) kila kilichojengwa katika msingi imara kitadumu ndiyo maana neno
la MUNGU linaitwa “mwamba” (1 Wakorintho
10:4) Yesu Kristo alifundisha kwa habari ya wajenzi wawili. Mjenzi mwenye
hekima na Mjenzi Mpumbavu.
Yule
mpumbavu alijenga bila msingi mvua ikaja na upepo hukavuma ukaipiga ile nyumba
na ikaanguka na anguko lake ni kuu, lakini yule mjenzi mwenye hekima alijenga
juu ya mwamba na mvua ikaja na upepo ukavuma, ukaipiga ile nyumba nayo ikaanguka
kwa kuwa ilijengwa juu ya Mwamba. Mathayo
7:24
Hivyo
kanisa ni lazima lijengwe katika msingi wa NENO kwa maana NENO ni MUNGU
mwenyewe Ufunuo 19:11-13, Waebrania 11:3. Kanisa la Yesu Kristo
mwenyewe kabla hajaondoka alishaweka msingi wa kanisa lake hapa duniani, kwa kusema
juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu hata malango ya kuzimu ya kuzimu hayatalishinda.
Mwamba huo ni KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI Mathayo 16:18.
Hakuna
Msingi mwingine zaidi ya uliowekwa na Kristo katika kanisa lake MWANA WA MUNGU
aliye hai. I Wakorintho 3:11-13
IMANI WAEBRANI 11:1
Imani ni kuwa na uhakika na mambo
yatarajiwayo na ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Msingi wa Imani ndani ya kanisa
la Mungu unatokana na Neno la MUNGU ambaye ni KRISTO. Kila mwananfunzi wa Yesu
yaani yeyote aliyeokolewa lazima awe na Imani juu ya wokovu alioupokea. (Yesu
Kristo aliyemwamba wa wokovu) Kwa maana Imani huja kwa kusikia neno la Kristo, Warumi 10:17.
Pasipo
Imani haiwezekani kumpendeza MUNGU, kwa maana kila amwendeaye Mungu lazima
aamini yeye yupo na huwapatia dhawabu wale wote wampendao, Waebrania 11:6.
Hivyo kanisa la Mungu lazima lijenge Imani ya waumini wake katika wokovu
walioupokea sawa sawa na neno la Mungu na siyo kitu kingine. Waebrania 11:32-38, Warumi 10:11, kwa
maana Mungu apendezewi na mtu au na kanisa lenye Imani ya kusita sita. Waebrania
10:38
Hivyo
ushindi juu ya Jambo lolote ni juu ya Imani yako, ndiyo maana Yesu aliwaambia
watu kuwa Imani yako imekuponya
UTAKATIFU 1WAKORINTHO
3:17
Ni
kanuni ambayo inatakiwa ifuatwe na kila ambaye ameokoka (Mwana wa MUNGU) kwa
sababu mara baada ya kuokoka tu, Roho mtakatifu anaingia ndani yetu (Ndani ya
roho zetu) na huu ndiyo unakuwa mwanzo wa nguvu za Mungu na moto wa MUNGU
kushuka juu ya maisha ya mtu, kinachobaki ni kuendelea kuchochea moto huu kwa
maombi na utakatifu kwa kuwa baada ya kumpokea BWANA Yesu Kristo, Roho
Mtakatifu anakaaa ndani yako, na wewe unakuwa umefanyika hekalu la Mungu
1Wakorintho 3:16.
Hivyo
pasipo kuchochea moto (NGUVU) wa
Roho Mtakatifu moto huu utazimika “Mithali 26:20. Moto hufa kwa kukosa kuni” Kanisa
la Mungu lazima likumbushwe kutunza Nguvu (MOTO) ya MUNGU kwa kukemea maovu
(dhambi) na kufundisha watu kutembea katika utakatifu wote ili kulinda uwepo /
Nguvu za MUNGU ndani ya Kanisa kwani nguvu za Mungu ukaa ndani yetu Waefeso 3:20, Waefeso 6:10.
UTII 1SAMWELI 15:22
Yesu
Kristo ni mtii na kondoo wake pia wanapaswa kuwa watii, Yesu Kristo alikubali
kwanza kunyenyekea na kutii na kwenda msalabani na MUNGU akamwadhimisha na
kumkirimia jina lipitalo majina yote. Wafilipi 2:5-10
Hivyo,
Kristo ni kichwa cha kanisa Efeso 5:23-24 na sisi tu viungo vya Kristo 1Wakorintho
6:15 inatupasa kuwa na utii katika Kristo na kufanya mapenzi yake. Inatubidi
tusikie sauti ya Yesu, Sauti ya Yesu ni neno la MUNGU, hivyo kila tunapojifunza
katika neno, inatupasa kuliweka moyoni, ni lazima upende kulisikia neno la
MUNGU, kulisoma neno la MUNGU na pindi neno linaposema badilika, yaani jambo
lile ambalo Yesu anataka ulifanye katika neno lake lifanye mara moja na huko
ndiko kumtii na kumfuata Yesu Kristo Yohana 10:27-28. Kondoo wangu
waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa
uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya
katika mkono wangu.
UPENDO 1YOHANA 4:7-11
Upendo
ndani ya Kanisa la kweli ni nguzo muhimu kwani MUNGU hukaa katika upendo, na upendo
ni amri kuu ya Bwana Yesu, yeye MUNGU ni pendo na watu wote ndani ya Kanisa
lake ni lazima wawe na upendo wa ndani, kuwapenda majirani na watu wote na pia
kumpenda MUNGU. 1Wakorintho 13:1-13
No comments:
Post a Comment