MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Monday, July 26, 2010

dawa ya HIV imepatikana




Ndugu Watanzania,

Tumepata habari za kuaminika kutoka vyombo vya habari kutoka Marekani na WHO kwamba wanasayansi nchini Marekani wamegundua chembechembe za kinga ambazo zinauwezo mkubwa wa kupambana na kuua virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba ya uhakika.

Ugunduzi huo tayari umethibitishwa na wataalamu mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.

Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa vimeripoti kuhusu ugunduzi huo ambao unaelekea kutoa mapambazuko mapya kwa ugonjwa huo hatari ambao umekuwa ukiathiri nguvu kazi sehemu mbalimbali duniani, hususan nchi zinazoendelea.

Wanasayansi hao wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) walieleza katika taarifa yao ya wiki iliyopita kuwa kwenye utafiti huo wamebaini aina mbili za chembechembe zinazoweza kumsaidia binadamu kupambana na virusi vya ukimwi.

Mkurugenzi wa Niaida, Dk Anthony Fauci alizitaja chembechembe hizo za kinga kuwa ni VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuua virusi vya ukimwi kwa asilimia 90.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) dawa huthibitishwa pale uwezo wake wa kupambana na ugonjwa unapozidi asilimia 60.

Dk Fauci alisema hayo ni mafanikio makubwa ya kisayansi tangu wataalamu mbalimbali duniani waanze kufanya utafiti wa namna ya kutibu ugonjwa huo.

Alisema chembechembe hizo za kinga hizo VRCO1 na VRCO2 zinaweza kutumika katika kubaini aina mpya ya chanjo ambayo itamuwezesha binadamu kuwa na kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Kwa namna chembechembe hizo zinavyofanya kazi, alisema, zikitumika kama chanjo, mwili wa anayechanjwa unajenga kinga ambayo inavishambulia virusi vya Ukimwi na kuviua.

“Kwa sasa soko lina dawa za kupunguza nguvu na kasi ya virusi vya Ukimwi kuathiri chembechembe nyeupe za kujikinga na maradhi na hakuna tiba,” alisema Dk Fauci.

“Lakini utafiti huu ni njia mpya ya kuelekea kupata ufumbuzi wa kudumu katika utaalamu wa tiba.”

Hata hivyo, alisema utafiti huo unaweka matumaini zaidi katika kutoa chanjo ingawa baadaye utawezesha kusaidia kupatikana kwa tiba kamili.

Jinsi walivyoendesha utafiti huo, Dk Faci alisema walichukua sampuli mbalimbali za damu zenye virusi vya ukimwi kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Katika sampuli hizo, alisema waliweza kupata aina karibu 200 za virusi vya ukimwi na walipozipambanisha na chembechembe za kinga za VRCO1 na VRCO2, virusi vilikufa bila kuathiri chembechembe nyingine za damu.

Hali hiyo aliilezea kuwa inathibitisha kuwa VRCO1 na VRCO2 zina uwezo wa kupambana na aina zote za virusi vya ukimwi.

Haya jamani habari njema ndo hizo, Lakini isiwe sababu ya kuanza kufanya mapenzi ovyo ovyo.

Matokeo yake yatakua kukua kwa kasi kwa yale magonjwa ya zinaa ya zamani kama kswende na gonorea na mengine, mimba kibao zisizotarajiwa, na matokeo yake watotot zaidi wa mtaani, vibaka, mateja n.k Tumia Kinga.

Maisha Mema,
Katibu T.A Reading.
--
Jumuiya Ya Watanzania Reading-UK
Blog :http://www.tanzaniaassociation-reading.blogspot.com/
Email:tzra2009@gmail.com
Tel No: +447865673756

No comments: