MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, March 24, 2021

MAOMBI YA KULIVUA VAZI LA KIPEPO ULILOVIKWA NA SHETANI.

 MAOMBI YA KULIVUA VAZI LA KIPEPO ULILOVIKWA NA SHETANI.


Na Pastor Daniel Lema


Neno vazi lina maana ya kitu chenye kuvaliwa. Wakati mwingine vazi ni utambulisho wa mwilini na Rohoni. Yesu atakapo kaa kwenye kiti cha Rehema ni tofauti na atakapokaa kwenye kiti cha hukumu. Kila cheo katika ulimwengu wa Roho kina vazi(utambulisho) Lipo vazi la Mwanajeshi pia hutambulishwa kwa njia ya vazi na vazi Hilo linakuwa na cheo Bwana Yesu asifiwe! Katika ulimwengu yapo mavazi yanayokutambulisha na yapo

kukuruusu kuingia sehemu flani. Kwa hivyo sababu ya vazi lake tayari kila mtu anajua wajibu wake. Ukienda hotel wale wahudumu huwa wana vazi maalumu. Linawatambulisha. Na vazi Hilo linamfanya atumwe Na mteja! Au amuhudumie mteja bila kuulizwa maswali. Kanisani vazi la mhudumu linamfanya aweze kukusanya sadaka na watu wasiwe na wasiwasi maana wanajua kazi ya lile vazi.

KWA IYO VAZI LINAWAKILISHA KAZI.

VAZI LA HAKIMU LINAWAKILISHA HUKUMU. 

VAZI LA DR. LINAWAKILISHA HUDUMA YA AFYA, 

VAZI YA WAKILI LINAWAKILISHA UTETEZI, 

VAZI LA MWANAFUNZI LINAWAKILISHA KUJIFUNZA, 

VAZI LA SPIKA WA TANZANIA LINAWAKILISHA UONGOZI WA KITI BUNGENI, 

VAZI LA JESHI LINAWAKILISHA ULINZI NA MPIGANAJI WA VITA. 

LIPO VAZI LA NESI LINAWAKILISHA HUDUMA YA AFYA, kama jinsi ilivyo Katika ulimwengu wa Mwili ndivyo ilivyo Katika ulimwengu wa Roho. Vazi Ni symbol ya kazi. Au ni Alama ya kazi. Watu wanaokuona watakutreat kutokana vazi lako. Kibiblia kuna aina mbili za Neno vazi


1. Vazi linaloonekana mfano Mwanzo 3:21 '' BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika."


2. Vazi la kiroho ambalo halionekani kwa macho ya kawaida ila matokeo ya vazi hilo huonekana, mfano Warumi 13:14 '' Bali mvaeni Bwana YESU KRISTO, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake."


Ukiangalia tafasiri ya BHN juu ya andiko hilo Biblia inasema kwamba ‘’Bwana YESU awe vazi lenu’’


Kwa jinsi gani tumvae KRISTO?


Wagalatia 3:27 inajibu kwa kusema ‘’Maana ninyi nyote mliobatizwa katika KRISTO mmemvaa KRISTO.‘’


Tena 1 Petro 1 :15 inajibu kwa kusema ‘’ bali kama yeye(YESU) aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;‘’


Vazi la KRISTO ni vazi jema sana.


Lakini pia kuna vazi baya kiroho ambalo mtu anaweza akavikwa kutoka ulimwengu wa roho wa giza, na ndilo linahitajika kutoka kwako kwa jina la Yesu ili uvikwe vazi jipya. 


Ni damu YESU KRISTO pekee inayoweza kuliondoa vazi hilo la giza kwa maombi kupitia jina la YESU KRISTO.


Tutashinda leo kwa jina la YESU KRISTO kama ambavyo ROHO MTAKATIFU ametupa ufunuo huu muhimu wa maombi ya siku 21 ndani ya POWER OF GOD FIRE CHURCH CHINI YA BABA YETU BISHOP DANKTON RUDOVICK RWEIKILA. 


Kwa hiyo kipepo wachawi au majini wanaweza kumvika mtu vazi la kipepo ili limtese, unaweza kuvikwa vazi la kukataliwa, kuumwa umwa kila mara, kudharauliwa, kuwa mtu wa hofu tu , kufuatiliwa na majini kila siku, umasikini, mateso n.k


Nataka tuangalie vipengele vifuatavyo, 


1. Wenye dhambi wasiotubu kwa Bwana YESU watakwenda jehanamu kwa sababu kiroho watu hao wamevaa vazi la kigeni yaani vazi wasilotakiwa kulivaa wanadamu walioumbwa na MUNGU.


Vazi hilo la kigeni ni dhambi. 


Sefania 1:8 '' Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya Bwana, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni.''


Vazi hilo hakuna anayemvalisha mtu yeyote ila ni mtu mwenyewe kwa matendo yake ya dhambi anajivalisha, kumpokea YESU na kutubu tu ndio njia pekee ya kulivua vazi hilo la kigeni liitwalo dhambi ambalo halitakiwi kuwako katika wanadamu wanaoutaka uzima wa milele. Ndugu livue vazi liitwalo dhambi ili lisiwe kamwe kwenye maisha yako maana hilo ni vazi la kigeni yaani ni vazi baya kwako.


2. Wokovu wa YESU KRISTO ni vazi wanalotakiwa kulivaa watu wote duniani. 


Isaya 61:10 '' Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika MUNGU wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.''.


Ndugu hakikisha unalivaa vazi hili muhimu sana. Usiuzoelee wokovu kabisa maana ni hatari mno walokole tumezoea hili vazi na kulifanya si kitu. 


Zaburi 132:16 '' Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia.''



3. Maisha ya haki katika KRISTO YESU ni vazi analotakiwa kulivaa kila mtu.


Ayubu 29:14 '' Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.''




4. Utakatifu katika KRISTO ni vazi la wateule wa MUNGU. 


Ufunuo 3:5-6 '' Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. ''. Ndugu hakikisha unalivaa vazi hilo bila kulivua hata siku moja. Wakolosai 3:10 ''mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. ''




5. Wito/Huduma ni vazi kwenye ulimwengu wa kiroho.


2 Wafalme 2:9-15 ''...... Kisha akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani.14 Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka. .......'''


Kama MUNGU amekupa wito au huduma kwa ajili ya kazi yake katika Kanisa la MUNGU hakikisha unatimiza wito wako na huduma yako. 


Usikatae kufanya kazi ya MUNGU. Usilivue vazi hilo wanalovaliswa na MUNGU wateule wake waliookoka.


6. Nguvu za ROHO MTAKATIFU ni vazi la wateule wa KRISTO. 


Luka 24:49 ''Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.''


7. Vazi safi la utakaso wa damu ya YESU KRISTO.


Zakaria 3:4 '' Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi''.


Ndugu hakikisha unamkimbilia Bwana YESU kwa ajili ya kutubu na baada ya kutubu atakuvika vazi jipya la utakaso, hivyo utaanza kuwa mtoto wa MUNGU na vazi la kwanza la dhambi malaika wataliondoa kwako maana sasa utakuwa safi mbele za MUNGU.


Katika kitabu cha Ayubu tunafahamu kwamba kwa kibali cha MUNGU na kwa sababu Maalumu MUNGU alimpa kibali shetani amshambulie Ayubu(Hiyo ilikuwa kwa Ayubu tu hivyo usijenge Imani yako kwamba unateseka kwa sababu MUNGU ametaka uteseke) Katika Maandiko anayemshambulia Ayubu ni shetani na shetani alimshambulia Ayubu kwa magonjwa mabaya . Nataka ujifunze kitu kwamba Ugonjwa unaopigana nao kipepo ni vazi.


Ayubu 7:5-6 ''Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini. '' Ayubu anakiri kwamba amevikwa vazi la ugonjwa.


Kuna watu wamevikwa mavazi machafu. 


Zakaria 3:3 ''Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.''


Kuna watu watu wamevikwa vazi la aibu,kudharauliwa, kuonewa, magonjwa, madeni, umasikini,ajali, matatizo na kila uonevu.


Kuna watu kila akijaribu kuomba kazi hapati lakini wengine wanajaribu tu na kupata kazi, ndugu livue vazi la kipepo ulilovalishwa kwa kutamkiwa kichawi na mawakala wa shetani.


Kuna waliovikwa kichawi vazi la laana, kukataliwa, kuabishwa na kufeli katika maisha.


Kuna watu wamevikwa vazi la kipepo la kuwafanya wawe chini tu.


Zaburi 109:18-29 ''Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake. Na iwe kwake kama vazi ajivikalo, Na kama mshipi ajifungao daima.''


Vua mavazi ya kipepo, yavue kwa damu ya YESU KRISTO.


Pia katika maisha yako yote usikubali tena usikubali haswaa vazi lako la Wokovu likachakaa, 


Ufunuo 7:14 ''Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.''


Hakikisha unalifua kila siku vazi lako la Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana. Fua vazi lako la Wokovu kwa wewe kuishi maisha matakatifu kila siku, Kufanya maombi kila mara, kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU na kulisoma na kulitafarakri Neno la MUNGU.


Omba MUNGU akuvike vazi la furaha 


Zaburi 30:11 '' Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.''


Omba MUNGU kwamba majira yako ya baraka yavikwe wema.


Zaburi 65:11 '' Umeuvika mwaka taji ya wema wako; Mapito yako yadondoza unono.''


Omba MUNGU awavike fedheha wote waliokuonea kipepo.


Zaburi 109:29 '' Washitaki wangu watavikwa fedheha, Watajivika aibu yao kama joho.''.


Endelea kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU ili siku ya mwisho uvikwe mwili mpya usioharibika wala kuzeeka.


1 Kor 15:53-54 '' Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. ''


Maombi ya leo.


1. Vua mavazi yote ya kipepo uliyovalishwa na mawakala wa shetani kwenye ulimwengu wa roho. Yataje mavazi hayo kupitia vifungo unavyoona umefungwa mfano magonjwa, kuteswa n.k


2. Choma moto kwa damu ya YESU KRISTO kila vazi la kipepo ulilovalishwa na mawakala wa shetani.


3. Omba MUNGU awavike fedheha maadui zako.


4. Omba MUNGU ili majira yako ya baraka yavikwe wema


5. Omba MUNGU kwamba vazi la haki alilokuvika likupe baraka


6. Omba MUNGU akuvike vazi la furaha.



Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa. Bwana akuviahw vazi jipya leo kwa jina la Yesu.

KUVULIWA VAZI NA KUVIKWA VAZI

 KUVULIWA VAZI NA KUVIKWA VAZI


Na Bishop Lambart Ileta


15th March 2021. 


Kuna vitu kadhaa tunataka tuangalia katika mfungo huu wa siku 21. Tunakwenda kuvaa vazi lakini sasa kabla ya kuvaa vazi ambalo linapatikana kwenye ufalme. Haya mavazi yanapatikana kwenye ufalme na upo kwenye ulimwengu wa Roho. Sasa lazima tujue haya mambo kwa kina kidogo. 


Warumi 10:9-10


Tunataka kuangalia ulimwengu wa Roho ni kitu gani na unaingia vipi. Biblia inasema ukiamini kwa moyo na kukiri ndipo unaokoka. Unapoamini na kukiri kwamba Yesu ni Bwana unaingia kwenye ulimwengu wa Roho. Ulimwengu wa Roho upo karibu sana na sisi kuliko vile tunavyofikiri. 


Kwa hivyo hatua ya kwanza ni kukiri kwa kinywa na unapokiri unapata wokovu na haki yako na unafunguliwa geti na mlango wa kuingia kwenye ufalme na kisha utaanza kupata haki za mfalme. Sasa utapataje hizo haki ni kwa kumuamini mfalme na neno lake. Unajua unapoamini kwamba wewe ni wa ufalme wa mbinguni itakuwa hivyo usipoamini hauwezi kuwa na haki ya ufalme huo. Ukiamini tu unapata ufalme. Kile kilichotoke kwa wale wezi wawili pale msalabani ilikuwa ni kuamini kwamba Yesu ni Bwana kiuhalisia hatukuona mahali ambapo huyu ndugu aliongozwa sala ya toba lakini aliamini moyoni mwake (Luka 23:39-43). Hizo ni siri za ufalme nakupa ukiamini tu. Jinsi ya kutengeneza na kupokea ni imani uliyonayo. Tengeneza imani yako ili kuweza kutengeneza mambo makubwa najua unaamini ndiyo maana huko hapa lakini unahitaji kuzidisha imani yako (Warumi 1:17). Unahitaji kuikuza imani yako kwasababu shetani anasimama kwenye imani yako ili wewe usiweze kusimama kwenye ile haki. 


Sasa utauliza nakuzaje imani? Imani inakuzwa kwa kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17). Na kama imani inaweza kuja inaweza kuondoka vile vile kwasababu inaondoka kwa kusikia vile ambavyo siyo neno la Mungu. Yuda 1:3


Kukiri maneno ni jambo lingine na kuyaamini ni jambo lingine. Kuomba ni jambo lingine na kuamini kile unachoomba ni jambo lingine ndiyo maana Biblia inasema ukiomba uamini kwamba yamekuwa yako na hayo yatatokea. Marko 11:24


Efeso 3:17-20


Kristo anakaa ndani ya moyo wako kwa imani. Imani ndiyo inakufanya ujue kwamba una Mungu au hauna Mungu ndani yako. Ukiamini kwamba yupo ndani yako yupo kweli kwa imani. Ukijua upana urefu na kina na kuamini ndivyo unavyopewa. Kwa kadri ya kuamini kwako na kujua upana wake na kina chake. 


Jambo la pili ni kujua upendo wake kwamba unajua anakupenda kiasi gani? Baba yako anaweza kuwa na vingi lakini unajua upendo wake kwamba anaweza kukupa. Kama haujui upendo wake hauwezi kupata haki yako. 


Sasa sikiliza usichanganye imani na uaminifu kwamba mimi nafunga ni kweli, mimi nafagia kanisa ni kweli lakini hayo yote kama hauna imani ni bure. Uaminifu haukusaidia kutengeneza jambo kwenye ulimwengu wa Roho bali inakusaidia pale ambapo Shetani anapeleka hoja zako akakosa kile ambacho atakushtaki nacho. Tofautisha haya mambo mawili faith and Trust.

NGUVU YA KUGEUZWA NA KURUDISHWA KWENYE ASILI YAKO

 NGUVU YA KUGEUZWA NA KURUDISHWA KWENYE ASILI YAKO


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila


14th March 2021


NENO HILO LIMEBEBA MAMBO MANNE 


YEREMIA 2:21


Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu?


》Unachosikia


》Kadri unavyoona ndivyo unatamani kusikia ( Unavyoona)


》Imani


》Mazingira


Mwanadamu aliumbwa mzabibu mwema na Mungu anauliza alipanda mzabibu mwema imekuwaje kugeuka na kuwa mzabibu mwitu. Sasa ili kujua kwamba mwanadamu anabadilikaje na aligeukaje lazima turudi kwa Adamu. 


Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu lakini aliporuhusu kusikia kutoka kwa ibilisi ndipo akaona tunda lifaa kuliwa na ghafla mazigira yakabadilika na wakajificha kujiona wako uchi. Mungu alipomtembelea Adamu alimkimbia Baba yake hivyo akategemea mabaya wakati alikuwa anamkimbilia Baba yake hapo awali. Imani yake ikageuzwa na mazingira yakageuka tena. 


Ndiyo maana mtu anapookoka anakuwa kwenye hali nzuri sana kiroho lakini ghafla anapoaanza kusikia maneno ya walokole ndipo uharibifu unatokea kwake na kuanza kushuka kiroho. Utasikia mtu akisema mimi nilifunga mara nyingi sikufanikiwa anakukatisha tamaa kwa kusudi kabisa. Hii si kwa habari ya kuokoka tu unapokwenda madhabahuni kwa mara ya kwanza utashangaa bidii utakayokuwanayo. Lakini ukianza kusikiliza maneno ya watu ndipo utakapopata shida. 


Kwa kadri moyo wako unavyobadilika ndivyo mahusiano yako na Mungu yanabadilika. Yule mwana mpotevu alipopoteza mahusiano na Baba yake ndipo Huduma nyingine ziliisha (Luka 15:11-32)


Shahuku ya ndani ikishageuzwa unaanza kwenda mahali kimazoea. Kwamba ni kwasababu jumapili kuna ibada lakini siyo kwasababu unashahuku na Baba yako. Nehemia aliposikia kuta zimebomolewa akasikia huzuni ndani yake. 


Baba yako ni wa vyote na ukutakiwa kuwa hivyo, kile ambacho kimekufanya uone ibada ya kawaida, maombi ya kawaida, mifungo ya kawaida kuna jambo alimekugeuza. Mahusiano yakifa hata kwenye ulimwengu wa kiroho yanakufa, ndiyo maana angalia yule mtu ambaye unamchukia hauwezi kuona akikubariki bali utaona anakukaba na kukufanyia mabaya. Hivyo ndivyo ulivyo ukimpenda Mungu wako utaona namna ambavyo utaona kwenye ulimwengu wa roho, utaanza kuona muda wa ibada ni mfupi, muda wa maombi kama hautoshi. Ukiona hayo jua moyoni mwako ibada hiyo haikuhusu. 


Mungu wako hawezi kukusahau wewe rudisha tu mahusiano na Mungu wako. Yeye amechora jina lako kwenye viganja vya mikono yake wala si kwenye viganja vya Malaika. 


Mabaya si sehemu yako unapokuwa na Bwana yatakuwa ya muda tu . Ayubu alipita kwenye jaribu hata wale rafiki zake wakina Bildadi, Sofari na Elifazi wakasema ni nani atakayevumilia kwa haya yaliyokupata na walijua ni mtu mwenye haki. Sikiliza dhiki hiyo ilikuwa ya kitambo tu ( 2 Wakorintho 4:17) na baada ya muda utangaa. 


Luka 5:1-11


Petro alisema kwa neno lako tutashusha nyavu. Petro alisikiliza neno la Bwana na hata alipoiangia kwenye chomba hawakumdai kutumia chombo chake. KWA NENO LAKE UNAWEZA KUFANYA MAKUU SANA. 


Kesho tunaanza maombi ya siku 21 masaa kumi na mawili kufunga na kuomba na tunakutana saa kumi kumi kamili jioni ibada itakuwa imeanza. Walete wagonjwa na wenye shida mbali mbali Bwana atawahudumia katika siku hizi ishirini na moja. 


Bishop Dankton Rudovick Rweikila

Power of God Fire Church

Chanika Buyuni

Simu +255  753 230 680 +255 717 538 499

Youtubu Chanel https://youtu.be/mJSqGrFBd4 inc

Facebook link.POwer of God Fire Church https://www.facebook.com/Power-of-God-Fire-Church-965783380111414/

Or 

Bishop Dankton Rudovick Rweki 

https://www.facebook.com/profile.php?id=100010423302719

www.powerofgodfirechurch.blogspot.com

Thursday, June 25, 2020

IDARA ZA MASHETANI ZINAZOSABABISHA KUZUIA HATIMA YA MTU 2

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila.

 

25th June 2020.


 

IDARA YA PILI

Idara ya udhahifu

 

Tunapoongelea idara ya udhahifu maana yake ni Roho za mashetani. Zile Roho ambazo zinafanya kazi ndani ya mwili wa mwanadamu. Mara zote tunafundisha mwanadamu ni muunganiko wa vitu vitatu: -

ü  Mwili

ü  Nafsi

ü  Roho

 

Na mwili umetoka mavumbini na Roho yako imetoka mbinguni na nafsi ni kiunganishi kati ya mwili na Roho. Mwili unapenda mambo yake ya Dunia na ndiyo maana ushindana na Roho. Kwa hivyo udhahifu tunao ongelea unawekwa kwenye mwili wako.  Mwili ukifunguliwa kwenye udhahifu ndiyo unasikia mtu amepata kitu Fulani na amefanikiwa mahala Fulani. Kuna maamuzi ambayo unatakiwa kuyafanya lakini mwii wako umegoma kwasababu umetiwa udhaifu. Udhahifu ule unakuwa sehemu ya maisha yako kwa maana mwili wako umetiwa udhaifu.

 

Sasa unapokuja kwenye nafsi yako ndipo unakutana na mambo kama matatu: -

ü  Nia- Ile nia ya kufanya mambo Fulani ile nia ya kutaka kufanikiwa katika jambo Fulani.Nafsi ikifungwa nia ya mtu inapotea na kujaa hofu, unaogopa sasa kwenda mahali.

ü  Utashi- Ni ile hali ya kuwa na maamuzi Fulani. Una utashi wa kumpenda Mungu na unao utashi wa kutokumpenda MUNGU wako. Una utashi wa kuamini watu na unautashi wa kutokuamini. Kwenye utashi wako ndipo shetani anapozuia mafanikio yako. Una utashi wa kubeba maagizo ya Mungu au kuyaacha na hapa ndipo tunapishana kwenye Baraka kwenye utashi. Ukishakuwa na nia pamoja na utashi ndipo unapa jambo la Tatu.

ü  Hisia

Kwanini shetani sasa anaiba nafsi ya mtu ni kwasababu hakuna mtu ambaye anaweza kufanikiwa pasipokuwa na Nia Utashi pamoja na hisia. Ndiyo maana mtu anafikia hatua nasema mimi sitaki rafiki kwenye maisha yangu. shetani akifunga nafsi yako ni sawa sawa na gari bila ya kuwa na magurudumu haliwezi kwenda. Sasa kwanini hili pepo la udhahifu? Pepo la udhahifu linateka nafsi yako na linapoteka linafunga nia yako, utashi pamoja na hisia zako.

Shetani akishafunga nafsi ya mtu anakuja kufunga milango mitano ya fahamu za mwanadamu: -

ü  kuonja

ü  Kuona

ü  kunusa

ü  kusikia

ü  kugusa/ Kuhisi

 

kama watu ambao hawajaokoka tu wanatambua nguvu ya nia utasikia wakisema kama una nia ya kufanikiwa utafanikiwa, vipi sisi ambao tumeoka. Lazima tuvae nguvu ya Nia kwa jina la Yesu.

 

Utashi wa mtu unaweza kugeuzwa na ulianza tangu kipindi cha Edeni. Adamu na Eva walikuwa kwenye Bustani na shetani akageuza ustashi wao kutoka kwa ule wa Mungu na kuona tunda linafaa kuliwa. Shetani alitumia milango mitano ya fahamu na akawateka Adamu na Hawa na kuwaangusha kabisa.

 

Kuna maisha ambayo unapitia kwasababu walgeuza utashi wako. Na ili ujue kwamba haukupatia ni namna ambavyo Roho yako inapiga kelele. Roho inaona mwisho wa njia yako na ndiyo maana unaendelea na kuishi lakini Roho yako inapiga kelele. Ukiona kwenye maisha yako unaishi na unajutia ni kwasababu ulitumia vibaya utashi wako.

 

Mathayo 8:17

ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.

 

Kuna magonjwa na udhahifu hapa na usije kuunganisha magonjwa na udhahifu ni vitu viwili tofauti. Ukishinda udhifu unaweza kushinda magojwa. Kinachotangulia kabla ya magonjwa ni udhaifu. Udhahifu unatangulia ndipo umasikini unakaa, roho ya kushindwa, n.k. Hauwezi kuondoa magonjwa kama haujaondoa udhahifu, ndiyo maana Yesu aliwaponya magonjwa ya namna yote lakini akawaondolea na udhahifu wao.

 

Warumi 8:26

Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

 

Udhahifu huu ni upi? ni katika nafsi yako ambayo imeshindwa kutumia utashi wako vizuri ndiyo maana Roho anasema hautajiuliza cha kufanya wala kusema kwasababu yeye atasema kwa niamba yako. Una utashi wa kuwa na rafiki Fulani lakini Roho anakuambai hapana. Amekuja kukusaidia kwenye udhahifu wako na ndiyo maana anakuamsha uombe lakini unakataa na anainua mtu mwingine anakupigia simu au anaweza kutumia mtu mwingine kwasababu anajua umeamua hauwezi kuomba. Roho yupo kwaajili ya kukusaidia udhahifu wako. Yusufu alikuwa hamtaki Mariamu ana amemuona ana mimba na kwasababu ya udhahiofu wa maamuzi ya ghafla anataka kumuacha Mariamu na Roho akamwambia Yusufu HAPANA!  Cha Mungu hauwezi kukiacha hivyo Yusufu hakufanikiwa na alisaidiwa na Roho ingawa tayari alikuwa na maamuzi ya kumuacha Mariamu.

 

Roho akishakusaidia unarudi kwenye mapenzi ya Mungu, kwasababu unahitajika kuyatenda yaliyo mapenzi ya Mungu. Zaburi 143:10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa,