MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, November 13, 2016

OMBENI BILA KUKOMA


Na Bisho Dankton Rudovick Rwekila ✍🏼

🙏Kuomba ni kudai au ni uhitajo wa jambo ambalo unastahili kulipokea .

👉Wakati unaomba katika ombi hilo linageuka kiwa haki yako, hovyo basi wakati unaomba unatakiwa uombe mpaka ulipokee jambo ambalo unaliomba ( Push until something happend)( PRAY)

Na kazi ya shetani 👶🏿ni kuhakikisha anakuzui hata kama unastahili kulipokea .

📖*Luka 18:1-6* Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima. Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.

📖Biblia inatueleza kwa habari ya Yesu na wanafunzi wake akiwapa wanafunzi wake mfano wa Kadhi Dhalimu na Mwanamke Mjane . Biblia inasema yule kadhi hakutoa haki kwasababu alikuwa mwenye haki la hasha ! Lakini ni kwasababu ya kusumbuliwa mara kwa mara na yule mwanamke mjane.

 🙏Unapoomba aumpangii Mungu wakati wa kukupa unachohitaji wewe ni kuomba . 📖Biblia inasema dhahiri Afya ni haki yako, utajiri na heshima ni haki yako, na mambo mengine mengi ambayo ni haki yako , ambazo ni ahadi juu ya maisha yako kama Mwana wa Mungu.

Biblia inasema "Maombi ya mwenye haki yanafaa sana tena akiomba kwa bidii"

Tatizo la wengi 👩‍👩‍👦‍👦👨‍👩‍👧‍👦wanapoomba 🙏wakati wanasubiria majibu shetani anaingia na kutupangia muda wa kupokea majibu, na anakuonyesha ni kama majibu yako yamechelewa na unastahili kulalamika sasa . Na tunasahau kabisa kwamba kuomba ni kwetu lakini kujibu ni kwa Bwana, na siku zote yeye hawai wala achelewi ( Godly time is the perfect time) . Inafika wakati mtu aliyekuwa anaomba anaishia njiani wakati ulikuwa unaomba haki yako🚶🏻.

Unapoomba bila kukoma hata kama wakati wako wa kupokea kile ambacho umekiomba na ni haki yako kutokana na maombi yako Mungu anakiachilia juu yako. 🙆🏻

Shetani anapokuleta uchovu ni kwaajili ya wewe kupoteza muujiza wako ambao hakika Bwana ni lazima alikuwa autimize juu yako. Unachohitajika kujua ni kitu kimoja , 👉muota ndoto hatakufa mpaka ndoto yake imetimia.

Kama huyu mwanamke mjane angelikata tamaa japo alikuwa na haki asingelipata haki yake. Alimsumbua kadhi mara kwa mara na mwishowe akapewa haki yake. Usikate tamaa kwa habari ya ndoto yako hata kama umechelewa kwa muda mrefu sasa .

Kuna watu wamekimbia ndoa zao🏃🏽🏃🏽, Biashara zao, masomo yao n.k kwa kuona Mungu amechelewa.

Kuna mambo mawili ya kuzingatia katika kuomba bila kukoma.

1⃣Lazima uwe na Imani ya Uvumilivu .
Imani ni kile unachokiona kwenye ulimwengu wa Roho na unakitarajia kitakuwa cha kwako. Unahitaji kujua ni nini Mungu amekusudia juu yako . Kwa maana nyingine kile unachokiona mbele yako kwa macho ya kiroho .

2⃣Lazima uwe na macho👁👁 ya kuona haki yako .
⏩Lazima umuombe Roho Mtakatifu hakupe macho ya kuona hatma yako. Unaweza kuwa na njaa sawa lakini je mbele yako unaona chakula🍟🍔una tabu sawa lakini unaona nini mbele yako. Kama macho 👀 yako ya rohoni yakekufa autaweza kusonga mbele .  Wengine wakiona tanuru la moto🔥 wewe unaona nini ? .

Cha kuomba 🙏 ni wewe kuwa na macho 👀ya rohoni . Kama macho hayaoni msaada unaweza kuwa umefika lakini wewe ukakata tamaa kwasababu auoni mbele . Wengi wasio ona Rohoni wanafungua kesi kabla hata awajashinda wanakata tamaa anaona kama sio haki yake na unafungua kesi nyingine miaka kumi na zaidi, kila mara unafungua kesi tu. Ndivyo yalivyo katika maombi 🙏🏼unaomba na unapeleka madai yako na haki yako kabisa na Yesu kama wakili wako anakutetea katika jambo hilo kabla haujashinda kesi⚖ unaiacha. Biblia inasema dhahiri katika habari ya kadhi. Kadhi alisema ijapokuwa simchi Mungu lakini nitampa haki yake. Unaona dhahiri huyu kadhi alikuwa ni mtu mzalimu lakini kwa sababu alisumbuliwa mara kwa mara alitoa
haki.

Yesu akasema " Na Mungu Je ! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku , nae ni mvumilivu kwao?.⚖

 Ndiyo maana Biblia inasema tafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na hayo yote mtazidishiwa . Maana yake kama umeokoka kwa habari ya kwenda mbinguni hautakata tamaa wala kurudi nyuma . Haijalishi vikwazo unavyokutana navyo unachokiangalia ni mwisho wa safari yako.

👉Wengine wanapopata Baraka katikati ya safari wanajua kwamba wamefika safari yao. Kumbuka jambo moja katika safari yako ya kwenda Mbinguni unapostawi ndiyo maadui wanaongezeka kwako .  Baraka katika safari yako ya kwenda mbinguni inawavuta maadui wengi.

Hutakubaliana na mimi katika mfano huu unaomba Baraka ya ndoa💑na unapata, sasa angalia vita unayokutana nayo baada ya ndoa, utamkuta mtu Amelia masaa kumi, na kujikumbatia mwenyewe hata usione wa kukufariji, na Baraka nyingine nyingi tazama matukio baada ya kufanikiwa au kupata aina ya Baraka ambayo uliiomba kwa Mungu.

Ndiyo maana nasema elewa unachokiomba unapoomba Baraka kubwa ujue ni namna gani unajipanga kulinda hiyo Baraka au huo muujiza.

Zaburi 51:17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

Lazima uhakikishe Roho yako inapondeka, maana yake unafinyangwa . Mungu anataka moyo ❤🔨uliopondeka na hapa sasa ndipo penye shida . Wengi wamejaa manung'uniko na kujiinua hapo ndipo Mungu uwadharau watu kama hao. Kama, Mungu akikudharau hutaweza kupokea kwake, Unapotembea na hofu ya Mungu lazima iwe juu yako.

Matokeo ya watu ambao Roho zao zimepondeka

Isaya 49:15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

Kuna watu walikuwa na hofu kwa habari ya dhambi , ukikaribia dhambi tu mwili unakufa ganzi . Lakini hofu aipo ndani yako tena. Maana yake ni nini ? Kiburi kimeinuka , ulipoona unaomba jambo na linafunguka na kiburi kinainuka

Mungu anataka unyenyekevu ndani yako . Mtu anayeomba unyenyekevu hauondoki ndani yake. Unahitaji moyo wa unyenyekevu unapoenda mbele za Bwana ili, Yesu aweze kusimama kama wakili ⚖

Usijaribu kumsusia Mungu kile ambacho ajafanya kwako . Omba Roho ya unyenyekevu , kabla ya kuingia kuomba bila kukoma.

Nami ninakuombea Nguvu ya Roho Mtakatifu izidi kukuatamia ili utambue siyo kwa matendo ya sheria bali ni kwa Neema ya Damu ya Yesu Kristo ndiyo tunaweza kuhesabiwa haki.

Mungu akubariki sana na nakukaribisha katika Ibada za mikesha kila Jumanne na Alhamisi saa 09:00 usiku mpaka saa 12:00 usiku na Jumamosi Ibada ya Ukombozi saa 09:00asubuhi mapaka 12:00mchana . Ibada ya Jumapili inaanza saa 09:00 mpaka saa 01:00 za mchana.

Mungu akubariki sana na siku njema

Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Chanika Buyuni
Dar es Salaam, Tanzania
+255 753 230 680 +255 717 538 499

No comments: