MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, October 25, 2009

Mganga wa Kienyeji ajisalimisha kwa Yesu (Dk. Manyaunyau)

Aliyekuwa mganga wa kienyeji, Jongo Salum, maarufu kwa jina la Dokta Manyaunyau amesababisha watu kupigwa na butwaa, baada ya kujitokeza hadharani na kutangaza azma yake ya kumpa Bwana Yesu maisha yake Jumapili iliyopita.





Azma yake hiyo aliitangaza kwenye mkutano mkubwa wa Injili ulioandaliwa na Soul Winners Ministry International (SWMI), uliofanyika kwenye viwanja vya Yombo Matankini jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya mganga huyo kukwama katika jaribu lake la kuharibu mkutano huo kwa njia za kishirikina



…..akishuhudia umati wa watu, uliowachukua muda mrefu kuamini kama kweli aliyekuwa anazungumza na kukabidhi maisha yake kwa Yesu alikuwa Manyaunyau, mwenyewe alisema amekuwa akifanya uharibifu mkubwa katika kuzalisha migogoro katika ndoa za wakristo, ikiwa ni pamoja na kuvunja uchumba kabla ya ndoa.




Alisema kwa siku hiyo alikuwa anakusudia kuharibu nguvu ya mkutano huo, lakini alijikuta akikwama na hivyo kujikuta akishawishika kuacha kazi hiyo na kuamini kwamba Yesu ni kiboko.



…….Baada ya shuhuda zake na kuutangazia umma kuwa sasa ameamua kuokoka, aliruhusu watumishi wa Mungu wafike nyumbani kwake kwa ajili ya kuchoma moto zana (tunguli) zote ambazo alikuwa akijivunia katika biashara yake ya kuzimu.



Kwa jijini Dar es salaam, dokta Manyaunyau amekuwa akifanya kazi ya uganga wa kienyeji kwa uaminifu mkubwa kutoka kwa wateja wake, kwani hadi alipokuwa anatangaza kuokoka, tayari amefika kiwango cha utajiri wa kumiliki mali mbalimbali, yakiwemo magari ya daladala, ambapo haijafahamika mara moja kama atayafanya nini baada ya kuanzisha maisha hayo mapya ndani ya Kristo.



Miongoni mwa mambo aliyokuwa akiyafanya kwa wateja wake ni kuchangisha fedha katika mitaa mbalimbali, ili kutoa wachawi mitaani, jambo lililompatia umaarufu mkubwa kutoka kwa wateja wake, maana wanadai aliimudu vilivyo kazi hiyo. Mojawapo ya mambo ya kipekee aliyokuwa akifanya mganga huyo wa kienyeji ni kuwakata shingo paka kwa meno na kunywa damu zao hadharani

No comments: