Na Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Mungu anataka kukufungua ili uweze kuwa na uhuru wako wa kuchagua jambo jema au baya . Uzima na mauti . Kuna watu awapendi Sigara,🚬 Pombe🍺 na vitu vya aina hiyo au vile vitu visivyompendeza Mungu🚫.
Isaya 14:24-25 Bwana wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea; kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao.
Isaya 43:1-2 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
Shetani👹 amekufunga🔗🔗 ili ukae kwenye maamuzi ambayo siyo ya kwako.📖Biblia inasema nimeweka uzima na mauti mbele yako , chagua uzima ili uwe ili uwe hai, wewe na uzao wako (Kum 30:19)
Wakati Roho Mtakatifu ananifundisha juu ya somo hili alinichukua mpaka kwenye mfano wa gari🚘 ambalo limejaa mafuta⛽ na Dereva👷 ambaye amepanga safari na kuhakiki kwamba mafuta yatamfikisha katika safari yake anayokwenda, yawezekana mafuta aliyoweka yanamfikisha Morogoro lakini kufika ubungo, mafuta⛽ yameisha kwa maana nyingine tank limetoboka 🚘.
👩👩👧👧Ndivyo inavyotokea kwa Mkristo ambaye ametoka kanisani🏰 na amempokea Roho Mtakatifu na kujazwa Nguvu za Roho Mtakatifu, lakini unapofika njiani unarudi katika hali yako ya kawaida ya dhambi kabla aujafika kule ambako Roho Mtakatifu alitaka ufike, kwenye kazi yako , Biashara yako , Kampuni yako , Ndoa yako n.k
Kupokea Roho Mtakatifu ni jambo moja, kuishi naye ni jambo jingine, na kukubali akuongoze ni jambo lingine.
Unapokea Nguvu💪 kwasababu ya kazi yako na wakati unaelekea kwenye kazi yako ghafla mambo ya Dunia 🌏yanaanza kukusonga na unajikuta ukitenda dhambi ambayo ni machukizo mbele za Mungu maana yake safari inaishia hapo na unakwama kabisa japo ulipokea nguvu ya kutosha kabisa.
Ndiyo maana kwenye maombi unasikia nguvu💪 ya Mungu kububujika lakini tukiangalia maisha yako halisi hakuna hatua 🚶ambayo umepiga kwenye maisha yako ya wokovu.
JE MUNGU ANAONGOZA MAISHA YAKO ?
Matendo 4:29 Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,
Walipokea Nguvu💪 na walikuwa na nia moja, ni muhimu kuangalia maisha yako je wewe una nia moja katika Kristo Yesu, kwasababu ukiangalia kanisa🏰 la sasa kila mtu anajiangalia mwenyewe na kujiongoza kwa namna inavyompasa yeye mwenyewe, Chuki zimejaa ndani ya kanisa🏰 na manunguniko kila siku yanazidi kutafuna kanisa la Bwana.
Wengi katika kanisa leo wamebaki wakihesabu ni miaka mingapi sasa wameokoka, bila kuangalia maendeleo yao katika wokovu.
Unafanya dhambi leo kisha kesho unatubu siku mbili mbele kabla hata ya muujiza wako unaanguka tena kwenye dhambi, miaka nenda rudi.
Ni sawa na mtoto wa Rais wa Nchi fulani au mtoto wa tajiri mwenye fedha 💰💸💸💵💴nyingi na madaraka makubwa, lakini mtoto wake analia njaa na kulala nje kila siku huku akijisifu Baba yake ni Rais au tajiri. . Mungu wetu ndiyo mwenye vyote na sisi kama watoto wake ni warithi sawa sawa na ahadi zake lakini maisha tunayoishi ni ya watoto wasio na BABA.
MTU MWENYE ROHO MTAKATIFU ANAKUWA NA MAMBO SABA AMBAYO YANAASHIRIA KUWA ANAONGOZWA NA ROHO
1⃣ Nguvu ya Upendo
2⃣Nguvu ya kushirikiana katika moyo mmoja
3⃣Nguvu ya kuambatana bila Kukata tamaa kwa moyo mmoja
4⃣Nguvu ya kuhurumiana inayotoka katika moyo wa kweli (Huruma ya KIUNGU) Katika huruma ni muhimu kupima huruma ya shetani na MUNGU. Huruma ya shetani inaambatana na sifa za kujitukuza mwenyewe, Huruma ya KIUNGU inamtukuza Mungu peke yake.
5⃣Nguvu ya kusamehe . Aijalishi aina ya kosa Biblia inasema Jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka. Waefeso 4:26
6⃣Nguvu ya kuomba msamaha. Aliye na Roho Mtakatifu ni mwepesi wa kuomba msamaha
7⃣Nguvu ya kumuheshimu MUNGU na watumishi wake.
Unapokuwa na mambo hayo tanki lako linakuwa salama na alijatoboka, Ili hatua saba hizi zitokee kwako ni lazima upitie hatua tatu muhimu
1⃣Kumpokea Roho mtakatifu.
2⃣Kuishi naye.
3⃣Kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Mungu akubariki sana,
Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Chanika Buyuni
Dar es salaam, Tanzania
Tel: +255 753 230 680 +255 717 538 499
No comments:
Post a Comment