MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, August 01, 2013

KCB BANK WAFUTURISHA

Inajulikana kwa jina la KCB Bank Tanzania jana walifanya kitu cha kipekee kabisa , katika mwezi huu mtukufu waliweza kuwakusanya waislamu wengi kupita kiasi pamoja na baadhi ya viongozi kadhaa wa vyama vya siasa, pamoja na aliyewahi kushika madaraka makubwa sana katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania si mwingine bali ni Mzee Ally Hassan Mwinyi


Decoration ilifanywa ipasavyo kabisa na wataalamu walitumia ujuzi wao kuakikisha hakuna linaloharibika.

 Set up ya Buffet la futari nayo ilisetiwa , kikamilifu.
 Mhhhh anaitwa Swahibaaaa alikuwa busy na simu sijui anapiga ikulu au laaa hilo sikulijua kwa haraka haraka.

 Ni kawaida kabisa kwa staff wa Jb Belmont all suite Hotel and Conference Centre kuakikisha kila huduma inakwenda na wakati , Jesca pamoja na Zaida wakiwekana sawa kabla ya kutua Huduma za kipekee kwa wageni waalikwa

 "nakuambia leo nitachelewa maana mpaka sahii awajaingia kuanza mawahidha " Bila shaka ni maneno ya mwanadada huyu akiwataharifu Nyumabani yote hayo yalikuwa ni katika kuakikisha kila kitu kinaenda sawa

 Dada Shose pamoja na wafanyakazi wengine  wa KCB wakiwa katika pozi la picture hao ndio walikuwa wafanikishaji wakubwa wa shughuli nzima kutoka upande wa KCB Tanzania
 Umati wa waislamu wakiwa katika hali ya usikivu kabisa ndani ya Jb International Conference Centre
 Mzee Ibrahimu Lipumba akiwa anabadilishana mawazo pamoja na watukufu waislamu

 Shekh akitoa Hazana mbele ya mgeni Rasmi
 Mh Mwinyi akiwa makini kabisa pamoja na wageni wengine




 Mh Mwinyi pamoja na wageni wengine wakitoka ukumbini kuelekea sehemu maalumu aliyoandaliwa kwaajili ya swala kabla ya kubreak the fast

 Hapa mpaka sasa sijapata jibu , nilikuwa na wasi wasi mkubwa sana watu kuvaliana viatu sijui ilikuwaje ila ndo mamabo ya Iftari na KCB
 Meza za vyakula vya futari vilipendeza sana

 Wakati wa kupata futari ulifika na utaratibu ulikuwa mzuri sana kama unavyoona katika picha


 Shukurani zilitolewa kwa waandahaji kwa kufanikisha kila kitu , asilimia mia 
Katika jambo liliolo shangaza wengi ni pale Mh Mwinyi alipotoa shukurani kwa kutolewa ushamba nina nukuhu '" Sina mengi ya kusema zaidi nashukuru ndugu zangu wa KCB Tanzania kwa kunitoa ushamba sikuwahi kudhani Tanzania kuna ukumbi mzuri kama huu nashukuru sana " hiyo ilikuwa kauli yake mzee wetu



Kiukweli mambo yalikuwa mazuri na kila aliyeudhuria alifurahi .Zawadi kutoka KCB zilitolewa kwa wageni wote waliohudhuria . Shukuranio za pekee ziwaendee KCB kwa kuamini kwamba Jb Belmont Hotel wanaweza na za mwisho kwa wafanyakazi wote wa Jb kwa service nzuriiiiii ..

No comments: