MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, January 27, 2010

JINSI YA KUPIKA KUKU WA KUPAKA

MAHITAJI
1.Vipande vya kuku bila mifupa
2. Tui zito la nazi
3. Nyanya zilizo iva safi bila ubichi
4. Pili Pili Hoho
5. Vitunguu swaumu vilivyopondwa
6. Vitunguu maji vilivyo katwa katwa
7. Mafuita safi ya kupikia
8. Hiriki 'mbegu zake'
9. Amdalasini ya unga
10.Giligilani ya majani

JINSI YA KUPIKA:
Weka sufulia jikoni, weka mafuta ya kula, weka vitunguu maji, kaanga, weka vitunguu swaumu kaanga, weka nyanya ambazo umezikata vipabde vipande, kaanga, weka pili pili hoho iliyokatwa katwa vipande vipande, weka hiriki iliyotolewa maganda 'mbegu', wacha mchanganyiko wako uchemke kwa muda kido(wakati moto upo mwingi)- baada ya dakika kumi kisha punguza moto, wacha imchemke teana kwa muda wa dakika ishirini zaidi, 'wakati unaendelea kugologa ili isiungue'-, weka amdalasini ya unga ndani yake, ipua mchanganyiko wako pembeni wacha upoe kwa kwa muda kisha blendi vizuri na blender machine mpka iwe laini zaidi hiyo sosi yako:

Weka sufulia yako jikoni, weka mafuta ya kupikia, weka vitunguu maji, kaanga, weka vitunguu swaumu, kaanga mpaka viwe laini kabisa, kisha weka vipande vyako vya nyama ya kuku ambavyo havina mifupa, kaanga, kisha weka sosi yako ambayo ulikuwa umeisaga hapo awali, acha imchemke kwa dk-5, kisha weka tui lako la nazi ndani yake, kisha wacha ichemke kwa muda wa dk-5 tena, remba chakula chako na majani ya giligilani.

ZINGATIA YAFUATAYO: Wakati unaweka tui katika chakula chako jikoni hakikisha tui halichemki kwa muda mrefu hadi chakula kupoteza muonekano- Kama sosi yako umeona haina rangi ya kutosha wakati unaipika mara ya kwanza waweza weka nyanya ya kopo kuleta rangi  nzuri zaidi.

Imetayarishwa na mjasiria mali toka ktk kiota cha paradise city.

No comments: