MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, January 11, 2018

SILAHA YA KUSIFU





Na Pastor Lambati Ilete

Siku zote mtu akitenda mema anapenda kusifiwa na anaposifiwa anaendelea kutenda yale aliyoyatenda. Kama mwanadamu anapenda kusifiwa na kukumbukwa kwa mazuri aliyoyatenda ni zaidi sana kwa Mungu. Na mwanadamu asiposifiwa anakata tamaa na kushindwa kuendelea kutenda mema. Mungu wetu yeye anatenda mema hata kama usipomsifia anaendelea kutenda mema tofauti na wanadamu.
Sasa siku ya leo tutamsifu Mungu maana maandiko yanasema kusifu kunawapasa wanyoofu wa moyo. Katika sifa kuna vitu vingi sana, sifa tu ni silaha, unaweza kuomba na maombi yako yakashindwa kufika lakini kama ukibadilika na kuanza kusifu Mungu atashuka.
Cheki wakati watu wako kwenye sherehe na wamemualika mgeni rasmi wanachofanya, wanaanza na sifa kwanza kwa kumchezea na kumsifu yule mgeni rasmi maana yake wanaandaa moyo wake kabla hawajamsomea risala. Sifa inaondoa maradhi, ndiyo maana wakati wa Sauli Roho mbaya ilipokuwa inakuja juu ya Sauli Daudi alikuwa anapiga kinubi na inakuwa matibabu kwa Sauli. Ukitumia sifa kwa ufahamu inamambo mengi ambayo unaweza kutumia kama chombo kwaajili ya kukuvusha. Na mimi nataka humsifu Mungu kweli kweli hili kama ulikuwa na uzuni na iondoke kwa jina la Yesu.
 Wakati wa wana Musa walipovuka bahari ya shamu kitu kikubwa walichokifanya asubuhi ya siku hiyo baada ya jeshi la Farao kuangamizwa walisema ni lazima kwanza wamsifu Mungu. Na wewe najua umeshinda mengi sana ambayo maadui zako walikuandalia na ndiyo maana nataka umsifu Mungu wako na kuruka ruka mbele zake.

Kutoka 15:1-21 _1 Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. 2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3 Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake. 4 Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu. 5 Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe. 6 Bwana, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, Bwana, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui. 7 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu. 8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. 9 Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza. 10 Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu. 11 Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu? 12 Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza. 13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu. 14 Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika.
15 Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka. 16 Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee Bwana, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua. 17 Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana, kwa mikono yako. 18 Bwana atatawala milele na milele. 19 Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari. 20 Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza. 21 Miriamu akawaitikia, Mwimbieni Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini_

Leo unapomsifu Bwana kila miungu ya ukoo, wachawi na majini utungu utawashika kwasababu hawatakukaribia. Unapokwenda kuvuka mwaka waliopanga uaibike wataaibika wao kwa jina la Yesu. Waliopanga upate misiba itawapata wao kwa jina la Yesu. Njia waliopita wana wa Israeli ndiyo kaburi la maadui zao. Na leo unapomsifu Mungu njia uliyopita inakuwa kaburi la maadui zako na kuwafunika kwa jina laYesu Kristo.

Bwana Yesu asifiwe…..

Leo madhabahu ya majini, wachawi, miungu inakwenda kuharibika kwa jina la Yesu. Unapomsifu Mungu leo maadui zako wanayenyuka na kuwa majivu kwa jina la Yesu. Watapata hofu na uonga na kukaa kimya kwa jina la Yesu.


Shaloom
Pastor Lambati Ilete
Power of God Fire Church                                                                                                                                                                                                          Simu: + 255 753 230 680 + 255 717 538 499

No comments: