Na Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Mwanzo 1:27-29
Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa
Mungu maana yake vile ambavyo Mungu yupo ndivyo tulihitajika kuwa kama watoto
wa Mungu.
Asili yako siyo kutawaliwa bali
ni kutawala kuna namna ambavyo shetani ilitubadilishia matumizi ya asili yetu.
Ndiyo maana kuna madhara ambayo kama mwanadamu yamekupata kwasababu ya
kubadilishiwa asili yako . Asili ya Mungu ni kuwa navyo vyote maana yake Mungu
aishiwi wala kupungukiwa na chochote . Unapoita nguvu ya uumbaji maana yake
unawakilisha Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, unasema nasema kitu gani ,
Cheki kile kitabu cha Yohana 1:1 na Mwanzao 1:1-2, Utaona namna
ambavyo Mungu aliumba ulimwengu na Roho ya Mungu alitulia juu ya vilindi vya
maji Biblia inasema *“juu ya uso wa
vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”*
Ukiwa na Nguvu ya uumbaji utaweza
kuumba mikono yako iliyopotea na utatawala tena na kumilika sawa sawa na neno la Bwana Mwanzo
1:28. Maandiko yako wazi kabisa kwamba utakapo kany’anga utapamiliki na
kupatawala , sasa yupo adui ambaye amekubadilishia matumizi ya miguu yako ya
awali badala ya kumiliki na kutawala unatawaliwa ndo maana nguvu ya uumbaji ni
maharifa ambayo Mungu ameachilia ili uweze kuumbwa upya.
Kuna namna Shetani amebadilisha malango yako ya Baraka iwe ni kinywa, miguu
au mikono Shetani amevichezea na ndio maana badala ya kumiliki unamilikiwa.
Efeso 3:16-20
Siongelei uumbaji wa nje naongelea uumbaji
wa ndani ambao Yesu alikupokufa na kufufuka alitukomboa kutoka kwenywe utu wa nje.
Naongelea uumbaji wa ndani, Biblia inasema nitabadilisha moyo wa jiwe na kukupa
moyo wa nyama. Maana yake unapewa moyo mpya moyo wa ndani. Napoongelea uovu
siongelei matokeo ya nje naongelea matokeo yale ya ndani kabla haujawaza ndani
ya moyo wako. Ndio maana unapo zaliwa mara ya pili ili si katika mwili wako,
ndugu zako,wazazi, mme wako au mke wako awawezi kujua ili maana ni kitu cha
ndani kati yako wewe na Mungu anayoachilia hiyo nguvu ya uumbaji juu
yako.Naongelea kitu ambacho jirani yako hawezi kukiona kwa macho ya damu na nyama.
Baraka zako ziko kwenye utu wako
wa ndani amabo ndio unabadilishwa wale siyo nje. Tunachokiona nje ni matokeo ya
Baraka zako kutoka ndani yako. Tizama kie kitabu cha 3 Yohana 1:2 Mpenzi
naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako
ifanikiwavyo.
Roho ndiyo ya kwanza kufanikiwa,
maana ndiyo inayobeba matokeo ya nje. Kitu cha kwanza unapopokea nguvu ya
uumbaji ni kurudi kwenye kusudi la Mungu alilokupa. Maana yake unautafuta
kwanza ufalme wa Mungu na kisha hayo mengine ambayo yanatamaniwa Mungu
atakuzidishia.
Kumbuka hili, Roho Mtakatifu
awezi kuachilia Nguvu yake ya uumbaji ndani yako kama kusudi lako siyo kujenga
ufalme wa mbinguni.
Ukisoma *Waefeso 3:20* maandiko
yanasema kuliko yale tuyawazayo, MAANA YAKE ZAIDI YA YALE AMBAYO UNAOMBA WEWE
Mungu anaweza kukupa Zaidi ya hayo.
Ngoja nikuambie jambo moja
unaporudi kwenye kusudi la Mungu siyo kila mara kile ambacho unaomba Baba
atakupa, kuna mengine hatakupa. Unasema nasema kitu gani, Wakati Yesu alipokuwa
katika mwili kuna jambo aliomba kwa Baba na baba akanyamaza kimya kwasababu hayakuwa
mapenzi yake Luka 22:42. Badala yake
alitiwa nguvu katika kikinywa kile kikombe. Hivyo hivyo na wewe kuna mengine
unaweza kuomba na usipewe lakini Bwana akakutia nguvu na ujasiri kuyakabili. Luka 22:43
Utu wa ndani ukikarabatiwa
matokeo ya nje yataonekana Dhahiri. Ndoto zako zinaweza kutimia kama utu wa
ndani umefunyagwa upya, na tena zitatimia Zaidi ya hizo ulizoziona.
Suleimani aliomba hekima ya ndani
ili aweze kuwahukumu watu wa Mungu lakini badala yake Mungu alimshushia na
utajiri na maandiko yanasema wala hakuna mfalme aliyekuwa tajiri kama
Suleimani.
Kama wewe ungelikuwa mfalme
yamkini ungeambiwa omba lolote ungelenga utu wa nje yaani vitu vinavyoonekana
tayari. Unasema nasema kitu gani?, kama una kijana kwenye mtaa wako na anaitaji
kuoa muulize kwanini anataka kuoa au kuolewa? Jibu lake litakuwa raisi sana
kama ameokoka atakuambia anataka kuoa ili asije kutenda dhambi. Inawezekana
kabisa hata wewe wakati unaoa au kuolewa uliwaza hilo, lakini sijui kama
umewahi kuwaza siku mwenzi wako akipatwa na ugonjwa ghafla amelala kitandani
kwa miaka kadhaa kwamba itakuwaje, je itakuwa sababu ya wewe kuoa tena au utamsubiri
apone. Ndoa ni Zaidi ya tamaa za mwili wako au heshima kwenye mtaa wako ni
Zaidi ya watoto.
Ndoa ni hatua ya utumishi ambao
Mungu ametupa. Sijajua kama uliwahi kulitazama ili kwa utu wa ndani kidogo.
Uliwahi kujiuliza kwanini mke wako ni msaidizi wako. Maana yake kuna vitu
ambavyo msaidizi amebeba ambavyo wewe
uwezi kubeba. Na Baba ambaye ni kichwa maana yake kuna vitu ambavyo baba
anaviona kama kichwa ili kuongoza vizuri kwa macho ya ndani kuna namna ambavyo
Roho ameviumba na kuweka ndani yake kama kichwa.
Sasa lazima Roho atengeneze utu
wa ndani ili agano ilo la utumishi liweze kusimama ndani yenu. Kuna mambo
mengine ambayo Biblia imesema kwa upande mmoja na yana nguvu sana kwa mfano
Biblia inasema juu ya mwanamke mpumbavu uivunja ndoa yake kwa mikono yake
mwenyewe Mithali 14:1. Sasa hakuna
mahala kwenye maandiko mwanaume ameandikiwa hivyo, maana yake kuna namna
mwanamke anatakiwa kusimama katika eneo lake na kuhakikisha analinda kile kitu
cha ndani yake. Ni lazima uumbaji upite ndani yako ili kukuumba upya utu wako
wa ndani.
Kama maandiko yanasema nitabariki
kazi za mikono yako, kama mikono yako imeibiwa hata upate billioni moja
itapotea tu kwenye hiyo mikono. Hivyo basi nilazima nguvu ya uumbaji iingie
kazini ili uweze kupokea kile ambacho kiliharibika na kubadilishiwa matumizi
yake ya asili.
Nguvu ya uumbaji inapopita ndani
yako hakuna kitu chochote kitakachokuzuia kusudi la Mungu ndani yako lisitimie.
Kama Mungu akuzuilika wewe kama mtoto wake auwezi kuzuilika kamwe. Mwazo 1:3-25
Namna pekee ya kumuondoa Shetani
katika maisha yako ni kuachilia nguvu ya uumbaji, hakuna bahari ya Shamu
itakayokuzuia kuvuka maana nguvu ya uumbaji iliyoumba maji inaweza kufanya maji
kuondoka na njia ikatokea.
Namna pekee ya kukomboa ardhi
iliyolaaniwa ni kuachilia nguvu ya uumbaji na hakuna namna nyingine . Pepo
linaweza kukaa mahali hapo.
Matendo 1:8
Ili kushuhudia kilicho ndani yako
lazima uwe na Nguvu ya Roho Mtakatifu. Ndiyo maana hata wakati wa kuomba
upinzani wako upo ndani yako, kwenye utu wako wa ndani wala siyo nje yako.
Mwili wako unashindana na kitu cha ndani kabisa Roho yako.
MAOMBI.
Ingia kwenye maombi ya toba
kwaajili yako.
Omba nguvu ya uumbaji katika
maeneo tofauti tofauti kwenye maisha yako ili Roho Mtakatifu aweze kuingia kati
na kuumba upya.
Achilia Damu ya Yesu ya
kunyunyiza juu ya ardhi unayokanyanga. Waebrania
12:24
Komboa Mikono yako na hakikisha
unaomba nguvu ya uumbaji juu ya mikono yako ili Bwana akuumbe upya.
Mpango wa Kusoma Biblia kwa Mwaka
Mmoja (1)
Wiki ya Tisa Siku ya Ijumaa
BishopDankton Rudovick Rwekila
Power of God Fire Church .
Chanika Buyuni, P.
O. Box 1556,
Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: + 255 753 230 680
+ 255 767 677 676
No comments:
Post a Comment