MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Saturday, November 26, 2016

KUNGUSHA FALME NA MAMLAKA YA GIZA


Na Bishop Dankton Rudovick Rwekil

Mungu anapotaka kubariki mtu kuna mambo yatatokea. Katika vipindi vilivyopita tuliona katika Yoeli Mungu anaachilia ndoto maono, lakini nilisema mtu anapofikia wakati wa maono maana yake unaanza kufanya kazi.

 Mungu anakuambia maisha haya,au utajiri huu au maono haya  utayatimiza katika mji huu. Siyo kwamba miji hiyo itakuwa aina watu ila watu watakuwepo na Mungu anawatoa hao na kukuweka wewe katika mji huu, Biashara hiyo , kazi hiyo na pengine huduma hiyo.

Unaweza ukasema Mchungaji mbona maombi haya ni hatari, ya mtu kuachia mimi nikapokea sikia fedha na dhahabu ni mali ya Bwana anampa nani Mungu ndiye anajua, Mungu anachokutaka wewe ni kwenda vitani upigane na uchukue chakwako.

Mungu akawaambia wana wa Israeli mtaingia Kanaani lakini walipofika wakakutana na majitu, maana yake yale majitu yalikuwa yamekalia ule mji, yalitoka na wana wa Israeli waliingia kanani yao.

Nawe kuna mambo lazima uyafanye ili uingie kwenye hiyo kazi ambayo Mungu amekupangia. Yapo mambo kama nane ambayo leo tutayaangalia;

Fungua na mimi Yeremia 1:10 “angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.”

Jambo la Kwanza

Mungu alikuwa anaongea na Yeremia kwa habari ya maono yake anamuambia tazama leo nimekuweka juu ya taifa. Mungu anapokupeleka sehemu yoyote ile ujue lazima utakwenda kwa mataifa au taifa. Kwa hiyo ujue ni lazima kuna taifa utashirikiana nalo na litaachia Baraka zako. Mungu ananena leo amekuweka juu ya taifa la Tanzania lazima maisha yako yabadilike, lazima biashara yako ije maisha yako yaje kwa jina la Yesu.

Jambo la Pili

 Lakini jambo la pili juu ya wafalme, taifa linapokuwepo kuna utawala unakuwepo. Taifa maana yake ni watu, kwa hiyo kuna watu ambao lazima wakutumikie na wewe uwatawale. Unapoomba upate kibali maana yake kuna watu utashirikiana nao, na lazima Mungu awatiishe na kuwaweka chini yako. Kwenye kustawi au kuongezeka unachoomba omba Mungu akukutanishe na watu sahihi kwa wakati sahihi. Unapoomba Baraka nilikuambia lazima ipite kwenye mikono ya watu.

 Siyo kwamba wanaofilisika wanamakosa,au wale maskini  ni kwamba awajakutana na watu sahihi, muombe Mungu akukutanishe na mtu sahihi. Unakuta mtu kila anapofanya anakutana na kudhulumiwa kwasababu wanakuwa na watu ambao siyo sahihi. Wamekosa watu sahihi ambao wametiishwa kwaajili yao.


Angalia Mfano huu wa Yakobo ambaye alitoka kwao hana ngombe wala mbuzi,na alikwenda kwa Labaani na Mungu akamtiisha Labani. Yakobo alikuwa mtumwa pale anatumika huku Labani akijua anaakili kuliko Yakobo kumbe Bwana alimuweka ili aondoke na utajiri. Labana akamwambia unataka mke tumika miaka saba, na kisha akampa mke tofauti na walivyokubaliana kwa kumuambia ni tamaduni za kwao mkubwa kuolewa kwanza na akamtumikisha tena miaka saba kisha akampa mke wake. Allipata wake lakini hakuwa na mali, Labani akamwambia nitakupa mshara na Mungu akaonekana hapo, na akatoka na utajiri wake.

Falme ni utawala uliopo katika eneo ambalo Mungu amekuweka. Unapoingia kwenye mji au kwenye biashara au kampuni lazima ujue falme au mamlaka inayotawala katika eneo husika ndipo uweze kufanikiwa. Wengi wanakwenda tu kwenye biashara bila kuelewa wale ambao anawazunguka.
Kumbuka utajiri au kuinuliwa auwezi kuinuliwa peke yako, unaponunua au kuuza kuna watu unafanya nao biashara hiyo, ni muhimu kujua falme au mamlaka inayomtawala huyo mtu ili asije kuwa anachukua fedha zako na kuzifanya chumaulete.

Ni muhimu kujua kwamba ni ufalme upi unaomtawala yule ambaye amekuajiri au unayefanya kazi nao au biashara. Lazima ujue kama anaabudu waganga au ni mchawi usije kukuta anaongozwa na majini na anaanza kuitawla fedha yako. Ni muhimu kujua falme inayomtawala yule ambaye unafanya naye kazi maana ndiyo inayofanya kazi kwenye ulimwengu wa Roho. Wengi tumeishia kupiga mtu asikuloge lakini atujapiga falme zao. Ni lazima falme zinazomuongoza mtu ndizo zipigwe maana ndizo zinamuongoza mtu. Hauwezi kupigana na Yakobo ambaye ndiye mchawi, Yakobo ana shida kuna ufalme ndio unaomuongoza na kumpa nguvu. Tunapigana na Yakobo na mungu wa Yakobo(Mchawi)

Ndiyo maana shetani aishii kukupiga wewe anataka kupiga mpaka nguvu ya Mungu iliyopo ndani yako. Usiishie kupiga majungu kazini kwamba kuna watu wanaopeleka umbea, lazima upigane na zile falme zinazochochea majungu Kumbuka vita yetu si juu ya damu na nyama (Efeso 6:11) Maana yake usipigane na watu ukaacha falme.
Ndiyo maana shetani anapotaka kupigana na wewe lazima haakikishe Roho mtakatifu aliyepo ndani yako, hayupo maana yake anakufanya utende dhambi, na ukitenda dhambi Roho mtakatifu anaondoka na ndipo shetani anakushughulikia. Maana Roho mtakatifu akiwa ndani yako awezi kufanya lolote.

 Kwa hiyo ukitaka kumshughulikia mtu ingia kwenye falme zake, kamata mamlaka yake na madhabahu zake utakuwa umemmaliza.

Jambo la tatu

Kung'oa
 Mungu anamwambia Yeremia Utang’o, maana yake popote unapokwenda lazima ujue zile falme zimepanda mbegu. Unapotaka kufanya biashara na mtu na umekwisha pigana na falme zake lazima uanze kung’oa yale mapando ambayo yalipandwa ndani yake, maana yako mabaya yalipandwa ndani yake. Lazima uanze kushughulika na kung’oa mapando ya utapeli , ya kuzulumu au ya kuharibu biashara, ili aweze kubaki kama mtu mwema. Wengi wanaishia kusema huyu mtu ameokoka hivyo aloghi tena, lakini ndiyo utakuta pando lipo ndani yake. Wengi tunawaona wameokoka na kukiri Yesu ni Bwana lakini ndani wanamapando ya majini, nilazima pando hilo lipigwe.

Uking’oa ufalme wa giza lazima upande ufalme wa Nuru, Mtazame Paulo ambaye pando la ukatili na kutesa kanisa la Bwana lilipong’olewa alijazwa Roho mtakatifu.

Jambo la Nne

Kubomoa
Kubomoa. Maana yake unapomoa ule ukuta, zile fikra , tabia. Ukiombea mtu hata kama amejazwa Roho Mtakatifu kuna wakati anakumbuka yale mawazo ya kale. Ukiokoka umeokoka lakini ukiendelea ta tamaduni zile zile wokovu wako aupo tena, ni lazima zile ngome zivunjwe, ubadilishe marafiki. Maana wale marafiki ambao ndiyo falme zinazokuzunguka wanaweza kuleta pando linguine tena kwenye fikra zako ili apande magugu. Ni lazima ile ngome uizingire kwa moto wa Bwana.

Jambo la Tano

Kuharibu
Mungu akamuambia Yeremia utaharibu, maana yake kazi zote zilizokuwa zimeunuka, yaani ambazo alikuwa anazitumainia,au anafaidi kupitia hizo. Ukiacha bila kuharibu ataona faida ya kwenda kwa wanganga wa kienyeji. Lazima ufike hatua ubige wanganga wake na matunguri yake, na hapo ataona anafanya hasara. Lakini ukimuacha bila kuharibu anaweza kuona faida kwenye tunguri.

Jambo la Sita

Kuangamiza
Akamwambia Yeremia Utaangamiza, kuharibu unaweza kuacha uhai bado hupo. Lakini hatua hii unatakiwa uhakikishe waganga wote aliowatumia wanaangamia. Nakuonyesha tu kwanini bado unavita, inawezekana ulingoa lakini haukuharibu, au uliharibu lakini ujabomoa.

Jambo la Saba

Kujenga
Ukishamaliza haya yote Biblia inasema utajenga. Maana yake ukijenga hakuna tena wa kugusa nyumba yako, Biashara yako n.k. Angalia Mungu alichomwambia Yeremia angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Jambo la Nane .

Kupanda
Mungu anakuruhusu sasa kupanda, maana tayari hakuna nzige wala madumadu. Wengi wetu tunapanda wakati bado atujangoa na tunaishia kulaumu.
Wewe ambaye Mungu alikupa biashara na ikaharibika chukua kanuni hii na biashara yako itainuka tena kwa Jina la Yesu.

Lazima ujue kanuni ya biashara yako , masomo yako na elimu yako ilikuwa nini? Kama ulikosema kanuni maana yake bado kuna vitu vinakusumbua kwenye Biashara yako.

No comments: